buzitata
JF-Expert Member
- Apr 11, 2017
- 2,370
- 7,900
Nashukuru kwa maelezo yakook sawa!
kwakuwa luka amesema amejihakikisha anachosema kiko sahihi..
(Mwandikiwa wa Kitabu cha Luke)
ambaye alikuwa Theophilo au Theophilus Mwana wa Ananus Mtukufu...
Kama Unasoma Extra biblical History Utagundua kwamba Theophilus amefariki Mwaka 47 AD (Ambaye alikuwa high priest wa Jerusalem from 37-41 AD, ambaye alikuwa mtoto wa Annas (Anna) na Shemeji yake Caiaphas (Kayapha)..)
Na ikumbukwe amefariki miaka kumi au kumi na kitu Tangu Yesu afariki na Ikumbukwe Kitabu cha Luka kimeandikwa Mwaka 90s AD mpaka 100s AD..
Miaka 40 mpaka 50 baada ga Kufariki kwa Theophilus..
Sasa Kama Kitabu cha Luka Kimeandikwa Miaka 50 Baada ya kufariki kwa Theophilus unahisi Ni theophilus Gani aliyekuwa anaandikiwa Ambaye alikuwa kwenye Position ya Uongozi enzi hizo??
huoni kama Ni fabricated Story???
Japo some Churches Historian wana identifies Theophilus kama later high priest yaani Mattathias ben Theophilus, ambaye yeye alitumikia from 65 to 66.
wakisema kwamba Luka alimtaja priest Joseph ben Caiaphas simply kwa "Caiaphas". yaani Kayapha...Thus, the reasoning goes, Luke used this pattern when addressing Theophilus.
Lakini Bado Huyo Theophilus mwingine na Yeye alifariki miaka ya 73 AD Kabla ya Uandishi wa Kitabu cha Luka..
Sasa tuachane na muandishi twende kwenye Context Za kitabu cha luka....je Ni sawa na Context Zingine za Vitabu vyenzake Vya Injili (Synoptic Gospel)? Sidhani....Kwakuwa tunaenda kwenye Contradictory facts twende sawa..
tuanze moja kwa moja kwenye uzao wa yesu!
ukianza kusoma
luka 3:23-24..
"Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri wa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, wa Yusufu,"
" Jesus, when he began his ministry, was about thirty years of age, being the son of Joseph, the son of Heli, the son of Matthat, the son of Levi, the son of Melchi, the son of Jannai, the son of Joseph,"
kosa la kwanza Joseph hakuwahi kuwa na baba anaitwa Heli, na nikupe faida heli ni jina la Kigiriki na joseph hakuwahi kuwa mgiriki..
na najua unaweza ukasema kuwa Heli ni jina la baba wa mama yake yesu yaani Mariam ila nakupa majibu kuwa mariam baba yake anaitwa Joachim na mama yake anaitwa anna ...
sasa kama tulivyosoma...
Baba Yake na Yusuph (ambaye ni Babu yake na Yesu)..
Ukisoma kwenye Mathayo Alikuwa anaitwa Yakobo (Mathayo 1:16) na ukisoma kwa Luka aliitwa ni Eli (Luka 3:23)..
From There the whole Clan ikapotea kabisa..
From eli to Zerubabeli.. Yaani namaanisha Ukoo wote wa Mathayo na ukoo wa Yesu wa Luka uko tofauti mpaka Kwa Zerubabeli....
Na hata Tukianza Kumchambua Ukoo Huo nataka Uwe makini Hapa uweke Akili zako zote hapa..(Si Unamtetea Luka?)..
Hakuna Doubt kwamba Zerubabeli Baba yake Alikuwa Sheatiel (Luka 3:27)..
View attachment 3567949
Lakini Nasikitika kukwambia Kwamba Zerubabeli (Zorobabel) hakuwahi kuwa na Mtoto anaitwa Rhesa wakati wowote ule kama Alivyotuambia Luka..
Soma (1 Mambo ya Nyakati 3:19-20.) Unakuta kwamba Zerubabel alikuwa na watoto watano ila Rhesa sio Miongoni mwa wanae..
Kulikuwa na Meshulamu,Hanania,Shelomithi,Hashuba,oheli,berekia,hasadia,Yushab-Hesedi...
View attachment 3567950
Ambapo kama Msomi mzuri wa Luka 3:27 Utagundua Kwamba Rhesa hakuwa miongoni mwa watoto wa Zerubabeli sasa Luka alimtoa wapi????
Na utagundua kwamba hata Baba yake na Sheatiel kama alivyotajwa kwenye Luka 3:27 Kuwa ni Neri kitu ambacho sio kweli Tukirudi Agano la kale 1 Mambo ya nyakati 3 Na hata kwenye Mathayo 1..
Kwa Mujibu wa Mathayo 1:12 Baba yake na Sheatiel alikuwa anaitwa Yekonia..
View attachment 3567951
Na hata kwenye 1 Mambo ya Nyakati 3:17..
Baba yake na sheatiel alikuwa yekonia Na sio Neri kama Luka alivyosema..
View attachment 3567952
Sasa Jiulize kuwa Huyo Neri Luka alimpata wapi..
Hata hivyo tukienda kuhusu Mwana wa Daudi wote wanafahamu kuwa Yesu Ni Mwana wa Daudi ils swali ni kwamba kwa Mwana yupi wa Daudi ukoo wa Yesu unaandikwa???
Ukisoma kwa Luka 3:31 Atakuwambia Nathan (Kitu ambacho Sio Cha kweli) Ndyo Mtoto wa Daudi Ukoo wa Yesu Ulipotokea..
ukisoma Mambo ya Nyakati 22:9-10
Daudi anathibitisha kuwa Sulemani ndiye aliyechaguliwa kuendeleza kiti cha enzi ambacho baadaye "Mwana wa Daudi" (Yesu) atakikalia.
"Tazama, mwana atazaliwa kwako... jina lake ataitwa Sulemani... nami nitakifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake juu ya Israeli milele."
ila luka yeye akaja akatuambia uzao utatoka kwa nathan..
Ukisoma kwa Luka 3:31 Atakuwambia Nathan (Kitu ambacho Sio Cha kweli) Ndyo Mtoto wa Daudi Ukoo wa Yesu Ulipotokea..
View attachment 3567955
nahisi niishie hapo nakaribisha hoja utakazo kuja nazo tuzijadili ila mpka hapo Luka anaeleza ukoo mwingine sio wa yesu
Ila naomba nikuache na mfano na hoja ndogo
Kwanza kabisa jua uandishi na utunzaji wa kumbukumbu wa zamani ni tofauti sana na uliopo sasa
KAma kumbkumbu zisipotunzwa vizuri baada ya miaka 500 utaibuka mjadala mzito sana kati ya jakaya kikwete na mrisho kikwete ni nani aliwahi kuwa rais wa tanzania
Ambao watasema ridhiwani watakuwa na hoja nzito tena zenye kueleweka pia watakaosema ni jakaya nao watakuwa na hoja za kueleweka na wengine wataamua kusawazisha kwamba wote wamewahi kuwa marais kwasababu miaka ya 2010 tanzania kulikuwa na utawala wa kurithishana hivyo wote ridhiwani na jakaya wamewahi kuwa marais, hao nao hawatakuwa salama itabuka hoja nyingine kumhusu magufuli
