Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

hili somo kali sana afadhali limenipumguzia hasira ya bunge lakatiba! mkuu hii elimu inanifumbua sana macho na kunipa mwanga zaidi tafadhali usinichoke!
1. nini kinafanya tuone mwezi mchanga, nusu na mwezi mzima
2. mgawanyo wa siku katika miezi ulizingatia nini (naongelea mwenye kalenda) na hapa naangalia dhana ya kiswahili kutumia neno mwezi na kwa nini wazungu hawaiti moon bali month!
3. kwamba mwezi kwa nini hauitwi nyota na je kuna miezi mingine ambayo sisi hatuioni?
pamona mkuu
 
Mtazamo binafsi kuhusu ufo na aliens:

Hivi nyie watu ndege za wachawi mnaziweka kundi gani? Nadhani kila mtu anawafahamu magagula, msijifanye wa mjini sana au kwamba mmesooooma!

Usiku vyombo vyao huonekana kama vimondo (meteorites), lakini vinakuwa chini zaidi, kwa vyovyote rada zina detect picha flani lakini inashindwa kueleweka ni kitu gani, pia rada zinashindwa kuvinasa, unafikiri watafikia conclusion gani... (intelligent aliens flying with miraculous objects !)... Chezea wachawi wewe!
 
Mwezi hauna muanga wake. Mwezi ni miamba na vumbi tu. Mwezi huchukua siku 28 kuizunguuka dunia yetu. Jua linapowaka kwenye uso wa mwezi sisi ndio tonaona mwanga wake kama mbalamwezi. Wakati huu mwezi unaizunguuka dunia kuna wakati sehemu yote inayomulikwa na jua tunaiona hapa usiku - hii ndio full moon au mwezi mzima. Lakini kadri inavyoizunguuka dunia si sehemu yote inayomulikwa inaelekea kwetu na ndivyo unavyobadilika kutoka mwezi mchanga, nusu na mzima.

2. mgawanyo wa siku katika miezi ulizingatia nini (naongelea mwenye kalenda)?
Kalenda tunayoitumia sasa ilianzishwa na mtawala wa kirumi Julius Caeser (Julian calender ya mwaka 46 BC) na baadae kufanyiwa marekebisho kidogo na mpwa wake mfalme Augustus. Ilipofika mwaka 1582 pope Gregory aliifanyia marekebisho ya mwisho ile Julian calender na kuwa na kalenda tuitumiayo sasa (Gregorian calender).

Sasa kwa kifupi tu tangu enzi ya Julian calender walijua kuwa kuna siku 365.25 katika mwaka. Walizigawa hizo siku katika miezi 12 na siku zake kama ifuatavyo (kuanzia Januari hadi Disemba J, F, M, A, M, J, J, A, S, O, N, D) 31, 29/30, 31, 30, 31, 30, 31, 30, 31, 30, 31, 30. (February ilikuwa na siku 29 na mwaka mrefu ilikuwa na siku 30)

Mwezi wa Julai uliitwa kufuatia jina la Julius Caeser na akajipendelea kwa kuufanya uwe na siku 31. Mfalme Augustus alipokuja na kuona mwezi wenye jina lake August una siku 30 akasema haiwezekani nae basi akaufanya mwezi wa August uwe na siku 31 na kubadilisha siku za miezi iliyofuatilia. Pia aliifanya Februari iwe na siku 28/29. Hiyo miezi imebakia hivyo mpaka sasa.

Kwa hiyo kalenda yetu ya sasa (J, F, M, A, M, J, J, A, S, O, N, D na siku 31, 28/29, 31, 30, 31, 30, 31, 31, 30, 31, 30, 31) ni matokeo ya marekebisho ya Julius Caeser na mfalme Augustus. Pope Gregory mchango wake ni kujua kuwa mwaka una urefu wa siku 365.2425 (au siku 365, saa 5, dakika 49, sekunde 12)

3. na hapa naangalia dhana ya kiswahili kutumia neno mwezi na kwa nini wazungu hawaiti moon bali month!
Kuna kalenda zinazotegemea kuonekana (kutoka) kwa mwezi. Kwa mfano kalenda ya Kiisilamu (Hijri) ina miezi (moons) 12 na siku 354/355 kwa mwaka. Nadhani hapa ndipo sisi waswahili tulipopata neno mwezi kumaanisha month.

4. kwamba mwezi kwa nini hauitwi nyota?
Mwezi hauitwi nyota kwa sababu hauna chanzo chake chenyewe cha mwanga. Mwanga wake ni reflection tu ya muanga wa jua.

5. na je kuna miezi mingine ambayo sisi hatuioni?
Hakuna miezi mingine hapa duniani kwetu. Lakini kuna sayari nyingi tu kwenye solar system yetu zenye miezi zaidi ya mmoja. Kwa mfano sayari kama Jupiter inasadikika kuwa na miezi 67.
 
Mtazamo binafsi kuhusu ufo na aliens:

Hivi nyie watu ndege za wachawi mnaziweka kundi gani? Nadhani kila mtu anawafahamu magagula, msijifanye wa mjini sana au kwamba mmesooooma!

Usiku vyombo vyao huonekana kama vimondo (meteorites), lakini vinakuwa chini zaidi, kwa vyovyote rada zina detect picha flani lakini inashindwa kueleweka ni kitu gani, pia rada zinashindwa kuvinasa, unafikiri watafikia conclusion gani... (intelligent aliens flying with miraculous objects !)... Chezea wachawi wewe!

Tatizo ni kuwa wachawi wetu sio wajasiriamali. Wewe fikiria kama umenunua ungo wako wa kupaa nao basi msongamano wa magari mijini usingekuwepo. Ukisha pata breakfast yako unakaa kwenye ungo wako na kufumba na kufumbua uko ofisini. Hamna jasho wala vibaka.

Kama unao huo utaalamu mkuu tuungane tuufanyie promotion na marketing.
 
Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakini ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au, jua liko umbali wa 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (kwenye constellation ya Centaurus) ambayo iko umbali wa 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa majua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko uzito wa atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haipotei bali hubadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni ya mkulu Albert Einstein kuwa E=mC[SUP]2[/SUP]. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fission) atom nzito kama za Urani (Uranium). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fission ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua kupitia fusion.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary-stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wave-length ya rangi ya bluu.) Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wave-length ndefu (wave-length ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, nyekundu na bluu. Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowasilisha mada yake kwenye kongamano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawasilisha.

I am sorry if this is an overkill.

Ivi kumbe wale waliochora Solar sytem na kutuambia jua ni biggest atom wametudanganya!
 
Vimondo vinatokana na nn,,mana nilisikia kuwa ni vipande vidogo vinavyomeguka toka kwenye nyota,,kwann huwa vinameguka?
Mkuu Kifyatu km una maelezo zaid tuongezee hapo
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni kweli vipindi vya hali ya hewa ya dunia vinatokana na dunia kulizunguka jua? Hii iko vipi?
 
Vimondo vinatokana na nn,,mana nilisikia kuwa ni vipande vidogo vinavyomeguka toka kwenye nyota,,kwann huwa vinameguka?
Mkuu Kifyatu km una maelezo zaid tuongezee hapo.

Hivi ni kweli vipindi vya hali ya hewa ya dunia vinatokana na dunia kulizunguka jua? Hii iko vipi?​

Samahani nimechelewa kukujibu. Shughuli zimepandikizana.

Vimondo (meteorites) havikumeguka kutoka kwenye nyota bali ni masalia ya vipande vya mawe, vumbi na barafu ambayo hayakuweza kujitengeneza na kuwa sayari. Kuna takataka nyingi sana kama hizi kati ya sayari ya Jupiter na Mars. Ukanda huu unaitwa asteroid belt. Mara kwa mara hizi asteroids zinagongana au kuvutwa na Jupiter kama manati na vinatoka katika mzunguuko wake wa kawaida na kuangukia sayari nyingine kama dunia yetu. Mawe haya yanapoingia kwenye anga letu lenye hewa basi yanaungua na tunayaona kama vimondo.

Kuna ukanda mwengine kama huu wa asteroid belt lakini uko mbali sana mitaa ya Pluto unaoitwa Kuiper belt. Saa nyingine vimondo tunavyoviona hutoka huko.

Hivi ni kweli vipindi vya hali ya hewa ya dunia vinatokana na dunia kulizunguka jua? Hii iko vipi?

Ni kweli.

Kwa sababu mhimili wa dunia yetu (axis kutoka north pole to south pole) umelala (tilt) kwa nyuzi 23.5 basi dunia inapolizunguuka jua kuna wakati mionzi ya jua inakuwa perpendicular na equator (March 20 na September 22). Wakati huu jua linakuwa kali sana kwa wanaoishi karibu na equator. Walioko kaskazini, kama ulaya, inakuwa Spring (March 20) au Autumn (Sept 22). Ikifika June 21 mionzi ya jua inakuwa perpendicular kwenye tropic of Cancer (23.5[SUP]o[/SUP] North). Wakati huo unakuwa wa kiangazi kwenye nchi za kaskazini na inakuwa winter kwenye nchi za kusini. Hii hali inajigeuza ikifika Desemba 21 wakati mionzi ya jua ikiwa perpendicular kwenye tropic of Capricorn (23.5[SUP]o[/SUP] South)
 
Nimekupata vyema mkuu,,sasa na vile tunavyoonaga angani kinapita kwa kasi huku kinawaka then kinapotea baada ya km sekunde 2 au 3 ndio kimondo chenyewe au? km ni hivyo huwa kinaishiaga wapi
 
Nimekupata vyema mkuu,,sasa na vile tunavyoonaga angani kinapita kwa kasi huku kinawaka then kinapotea baada ya km sekunde 2 au 3 ndio kimondo chenyewe au? km ni hivyo huwa kinaishiaga wapi

Ndio ni vimondo vyenyewe.

Kuna vinavyoungua kabisa na vingine vinaanguka aridhini. Kwa mfano, kimondo kikubwa kilichoanguka Tanzania zama hizo ndio kilichochimbua shimo kubwa sana tunaloliita "Ngorongoro Crater" siku hizi.

Jibu ni kuwa vimondo vinaweza kuungua kabisa au kuangukia duniani. Ukienda kwenye internet (google au search engine nyengine) na kuandika meteorite utapata taarifa za hivi vimondo.

Kuna vimondo vikubwa sana vilivyoanguka Urusi. Hivi karibuni kuna komondo (Chelyabinsk meteor - February, 2013) kilicho anguka na zamani kuna kimondo kingine kilichoanguka huko huko Urusi (Tunguska meteor - June 1908). Naomba utafute taarifa zake na unitonye ukizipata. Hii ndio homework yako ya leo.
 
Mkuu nimevipitia vyote hvyo ila naona hicho cha 2013 hakikua na madhara makubwa km cha tunguska, mlipuko wake ulkua zaid ya km 2000 za mraba, so amazing kwa kweli.
Af nlikua sijui k crater ya ngorongoro ni product ya kimondo,,nackia kuna ambacho kiliangukaga huko mbeya,kipo sehem gani?
 
Umefanya kazi nzuri sana kwenye hii homework yako.

Kimondo kilichoanguka Mbeya sina uhakika nacho lakini nikipata taarifa nzuri nitakueleza.
 
Mkuu Kifyatu usiku wa jana nimeona nyota ambayo inatembea, yan ina move kwa spidi km ya ndege, sasa sijajua km ni nyota ama ni kitu kingine, nimejaribu kupitia google ila sijapata majibu ya kuridhisha,ila NASA wanasema zipo hizo moving stars
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kifyatu usiku wa jana nimeona nyota ambayo inatembea, yan ina move kwa spidi km ya ndege, sasa sijajua km ni nyota ama ni kitu kingine, nimejaribu kupitia google ila sijapata majibu ya kuridhisha,ila NASA wanasema zipo hizo moving stars

Kama uliiona kamanyota lakini inatembea kwa kasi basi hiyo itakuwa ni satellite. International space station huonekana kirahisi sana na inatembea kwa kasi. Nadhani ndio ulioiona.
 
Kama uliiona kamanyota lakini inatembea kwa kasi basi hiyo itakuwa ni satellite. International space station huonekana kirahisi sana na inatembea kwa kasi. Nadhani ndio ulioiona.

Kwahiyo hakuna nyota zinazotembea ?
 
Back
Top Bottom