Ufisadi na ubadhirifu kwenye halmashauri za miji umerudi kwa kasi. Pesa za umma zinatafunwa kama njugu

Kila kitu mnataka Raisi ndio asafishe? inawezekana kweli? naamini madiwani na mbunge wa hiyo sehemu kama wana akili wana uwezo kusafisha halmashauri zao bila matatizo
Wabunge na madiwani ni zao la wizi wa kura, na hao watumishi wa halmashauri wanalijua hilo, hivyo hawawaogopi wezi wenzao.
 

Rais anamuwajibisha mkuu wa wizara. Hakuna mswahili anaeweza fanya kazi bila kusukumwa
 

Bora hizo enzi za kina JK na huyu mama kuliko ule uhayawani uliokuwa unafanywa na rais wa awamu ya tano na genge lake la watu wasiojulikana. Ule uporaji wa fedha za watu kwenye ma bureau De change, korosho kubambikia watu kesi na kodi zilikuwa ni zama za giza. Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule kiongozi muovu bila damu kumwagika.
 
Wizi kwani uliisha lini?

CAG alipoomba document za manunuzi ya ndege ikawa ni taa ya kuondoshwa ofisini.
 
Ulishawahi kuisha lini? Watumishi wa CAG Wanaohongwa na ma Ded ili wawandikie hati safi. Hujui lolote kuhusu halmashauri za TANZANIA. Nyamaza
 
Kwenye Halmashauri uliyopo zimeshaliwa pesa kiasi gani mpaka sasa?
 
Ulishawahi kuisha lini? Watumishi wa CAG Wanaohongwa na ma Ded ili wawandikie hati safi. Hujui lolote kuhusu halmashauri za TANZANIA. Nyamaza
Huoni bado kuna chance ya wananchi ndani ya halmashauri kupigana na huu ufisadi? hongo or no hongo amini wananchi ndani ya halmashauri bado wana nguvu sana kuliko hao wakurugenzi, hope siku wataamka na kujitambua na kwa ufupi nguvu ya0 ipo kupitia madiwani wao
 
Ndugu hakuna wakati ufisadi ulikoma sema tu ulinyimwa taarifa za wazi na wapigaji. Ndio maana uliingia kwenye giza la kuamini kuwa huenda wamekoma kufanya ufisadi. Kupenda uovu ni roho mchafu atokaye kwa baba yao watendao uovu, haikomi kwa Sheria iwayo yoyote ila kwa rehema na neema kutoka kwa Mungu aishie milele. Mungu atupe neema.
 
JPM alizuia!?[emoji848][emoji848][emoji2827] hapana hakuzuia bali aliwabana wengi na kuwapa wachache wake
Logic gani ? Umeandika nini sasa? Kama alifanikiwa kuwabana wengi maana yake alizuia sehemu kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…