Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

..............jamani na taka kuuliza kuwa hawa misukule walirudia hali yao ya binadamu wa kawaida au walibaki misukulee? Je walirudi kwenye familia zao au mchungaji aliondaka nao?..inafaa tuwe makini sana na wachungaji siku hizi maana hata neno la mungu linatutahadharisha kuhusu manabii wa uongo.....
 
NAMPENDA JESUS, YEYE ALIKUWA AKIMFUFUA MTU ANAWAMBIA NI SIRI MSIMWAMBIE YOYOTE,,,,LAKINI SIKU HIZI NINA SHAKA SANA NA HUU MTINDO WA KUPELEKA KTK VYOMBO VYA HABARI,,NAHISI WANAFANYA MARKETING ..................
:faint2:
 


Nimefurahi kwa ufafanusi na maelezo yako. Nikiri nimebarikiwa nayo kwani kuna jambo limeongezeka katika ufahamu wangu ninapoendelea kutafakari neno la Mungu kwa kuuomba msaada wa Roho Mtakatifu.

Ila maadamu Yesu mwenyewe aliamua kuweka mkazo kuwa watakaju kwa jina langu na mtawajua kwa matendo yao basi hatuna budi kumuomba huyu Yesu mwenye atupe ufahamu na uwezo wa kutambua ni miujiza na matendo yapi yanayo fanywa kwa jina lake bali hayana kibali chake, yana kibali cha manabii wa uongo, maana hili la maanabii wa uongo kulitumia jina la Yesu halina ubishi lilitabiriwa na Yesu mwenyewe.
 

Amen umenena, shetani anahila bwana. Hebu fikiri Adam na Hawa kwenye bustani ya eden. Kwa amiri ya Mungu mwenyewe usile, lakini shetani alimlaghai Hawa, Hawa akamshawishi Adam. Itakuwa sisi wa kizazi cha dot.com. Ni kwa neema tu, Mungu tunakuomba utupiganie.
 
NAMPENDA JESUS, YEYE ALIKUWA AKIMFUFUA MTU ANAWAMBIA NI SIRI MSIMWAMBIE YOYOTE,,,,LAKINI SIKU HIZI NINA SHAKA SANA NA HUU MTINDO WA KUPELEKA KTK VYOMBO VYA HABARI,,NAHISI WANAFANYA MARKETING ..................
:faint2:

Kwa huu mdahalo unavyoendelea hapa, mpendwa usishangae kuambiwa wakati wa Yesu kulikuwa hamna Tv.

Niseme tu nataka nimjue Yesu, ni jue neno lake, Upendo wake na Wokovu wake.
 
watu wamegeuza dini kuwa biashara na suala la kufufua misukule ni usanii tu, hakuna lolote.
 

Hakuna misukule hata mmoja aliyedhibitika kurudia katika hali yake ya kawaida!

na mbaya zaidi hao misukule hawana hata origin
 

wewe huna tofauti na wanao waua Albino ili watajirike !..........:frusty:
 
Kwa huu mdahalo unavyoendelea hapa, mpendwa usishangae kuambiwa wakati wa Yesu kulikuwa hamna Tv.

Niseme tu nataka nimjue Yesu, ni jue neno lake, Upendo wake na Wokovu wake.

Teknolojia ya tv siyo ya siku nyingi sana
 
Ni bora tujue basi hao misukule wamerudi kwenye familia zao?na next sunday tuwaone wakihudhuria misa wao na family zao ili watu wawe na uhakika kwamba huo haukua usanii.
 
Kuna jamaa mmoja aliniuluza mbona wale wanaodondoka wakisafiri na ungo hakuna anayedondokea kichwa. Mpaka leo bado natafuta jibu.
 



Sitetei hayo unayopinga ila naona unapungukiwa mashiko ya hoja, mtu kufufuka sio lazima awe amekufa mda mfupi uliopita na hakuna sayansi inayozungumzia ufufuo ndugu, ni imani tu
 
Sitetei hayo unayopinga ila naona unapungukiwa mashiko ya hoja, mtu kufufuka sio lazima awe amekufa mda mfupi uliopita na hakuna sayansi inayozungumzia ufufuo ndugu, ni imani tu

Mwili uliokufa hauozi?
 
Ni vizuri kabla hatujahukumu watu wafanye homework yao. Si tuna waandishi wa habari humu akina Mathias Byabato Fred Katulanda ? Kwa nini wasiende kuwahoji hao watu na kufanya uchunguzi kujua ukweli wa claims? Uzuri wa Ukristo mambo yanafanyika hadharani na unaweza kuchunguza na kuujua ukweli refer miujiza na kufufka kwa Yesu, miujiza ya mitume et al. Kila kitu kilikuwa public.

Hapo tutakuwa na jibu la uhakika lisilo na shaka Mungi
 
Last edited by a moderator:

Utakutana na visingizio lukuki mkuu kwenda kuwahoji misukule..
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli hakuna mtu mwenye uwezo wa kumrudisha mtu aliyekufa, ila msukule sio mtu aliyekufa.
WATU ZAIDI YA 20
WARUDISHWA
KUTOKA KWENYE
MISUKULE HUKO
ARUSHA KWENYE
MKUTANO WA MCH. GWAJIMA. Habari inatoka Gospel Media News
 
Ugumu wa maisha umetufanya Wakristo tuonekane kama mapunguani/hamnazo.

Mkuu mimi sitaki kuamini kama ni ugumu wa maisha tu ila pia na ubinafsi na zaidi kutomtii Mungu katika amri zake maana kuna sehemu zinasema usidanganye,mimi ni Mkristo ila napinga kabisa huu udanganyifu unaofanywa na hawa wanaojiita mitume.......jamaa wananikera sana......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…