Ok nafikiri Hapo tuko Sawa! Unajua mauti ya pili ndio hiyo ya kuzingatia kwasababu mauti hii ya kwanza ni Kama kulala tu usingizi! Kitu cha kuangalia katika mauti hii ya kwanza ni kufa katika tumaini la uzima wa milele au ni kufa katika dhambi!
Kwa Sasa kutokana na watumishi Hawa wa dini kufanya miujiza mikubwa Je kuna ata mmoja anaweza kukufua Wafu? Maana Maandiko yako wazi na Tumeona wale kumi na wawili wakiagizwa kufanya makuu! Sasa kwa kipindi hiki tunaweza tukawa na watu Kama Hao?
Kuwa na watu kama hao kwa sasa ni ngumu kidogo mkuu!
mi huwa nashangaa sana kuwaona kina TB joshua wakijeweka kundi moja na kina Paulo wa enzi zile
Kwa Lugha rahisi tunaweza kuwaita Manabii wa uongo sasa Kwani kwa sasa hatuwezi kua na watu Kama wale!
Vipi Kuhusu Imani zetu Maana Kama hatuwezi kua na watu Kama wale ina Maana kwa walimwengu wa Leo Imani zetu ziko chini sana ya kiwango na kwa Maana hiyo uzima wa milele kuuona ni kazi!?
Taarifa yako haipo sahihi hata kidogo.
1. Kwanza mkutano wa Injili haujaanza bado mjini Moshi hadi tarehe 20/10/2013
2. Watu waliofikwa na majanga makubwa ya kuchukuliwa misukule. Kanisa huchukuwa jukumu la kuwahudumia Kiroho na kumwili hadi wafikie kiwango cha kusimama wenyewe kwa maombi.
si ajabu shule umeenda, halafu una comment huu ujinga !
Haishangazi, maana mna nunua picha dukani kisha mnatundika sebuleni halafu mnawaambia watoto wenu: huyu ni BWANA WETU !
Ni kazi kubwa sana kuuona huo uzima wa milele kwa kupitia hawa watumishi wafufua misukule! cha muhimu ni kila mtu kukomaa kwa imani yake haswa ile ya mwanzo..
Mkuu Samahani kwa maswali Yangu!
Tunaweza ifikia Ile Imani ya mwanzo iwapo ata Hawa wanatuongoza hawana huo uwezo Kama punje ya mbegu ya Aladari? Tunaweza kweli?
Ndio Maana Mimi wakati mwingine Hua naamini Ufufuo Upo kwa Yule mtoa uhai! Sisi sio watoa uhai na Imani zetu ni chini sana Kama ulivyosema kua ni kazi. Sasa tutaweza Vipi kufufua watu ingawa Maandiko yametupa nafasi ya kufanya hivyo?
maandiko hayazungumzi juu ya kufufua misukule!
labda kama wafu na misukule inamaana moja
mbinu za kuyakabili maisha ndizo zinatoa maarifa mapya
Kuna mtu alisema wanaombea wagonjwa na wanapona,sasa swali la kujiuliza kwanin wasiwe wanaenda hospital moja kwa moja? Na kama umate umate si watapewa na ndugu wa wagonjwa?
Ni kazi kubwa sana kuuona huo uzima wa milele kwa kupitia hawa watumishi wafufua misukule! cha muhimu ni kila mtu kukomaa kwa imani yake haswa ile ya mwanzo..
Maisha ya kimwili Si bora Kama maisha ya kiroho! Ni Vema kuponya Roho kwanza kuliko mwili!
Maneno yenu yanafanana kabisa na wale waliokuwa wakimkebehi Yesu msalabani wakisema na ajiokoe mwenyewe sasa!!! Kama Yesu mwenyewe aliitwa mchawi na kudhihakiwa itakuwa hawa watumishi wake?
Binafsi najua kuna usanii mwingi siku hizi na pia siendi ovyo kwenye makanisa ya kilokole lakini pia sibezi kazi ya Mungu kupitia wachungaji kisa tu kuna wasanii.Kama ni usanii nitafanya utafiti wangu mwenyewe kupitia mafundisho yake na huduma yake ili kupitia matunda ya huduma yake nijue kama kweli ni mtumishi wa Mungu.
Wewe ndio umeuliza vizuri ingawa sina jibu lako kwakuwa sihusiki na huduma ya Gwajima.Umekiri kuwa Yesu anaweza ingawa una mashaka na huduma ya huyu mchungaji kitu ambacho ni cha kawaida kwani hata Tomaso hakukubali kirahisi na Yesu mwenyewe alisema akina Tomaso wapo wengi.
Unaiponyaje roho, halafu ukitumia Roho yenye herufi kubwa maana yake ni Roho ya Mungu, roho ya mwanadamu inaanza kwa herufi ndogo.