Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ok nafikiri Hapo tuko Sawa! Unajua mauti ya pili ndio hiyo ya kuzingatia kwasababu mauti hii ya kwanza ni Kama kulala tu usingizi! Kitu cha kuangalia katika mauti hii ya kwanza ni kufa katika tumaini la uzima wa milele au ni kufa katika dhambi!

Kwa Sasa kutokana na watumishi Hawa wa dini kufanya miujiza mikubwa Je kuna ata mmoja anaweza kukufua Wafu? Maana Maandiko yako wazi na Tumeona wale kumi na wawili wakiagizwa kufanya makuu! Sasa kwa kipindi hiki tunaweza tukawa na watu Kama Hao?

Kuwa na watu kama hao kwa sasa ni ngumu kidogo mkuu!
mi huwa nashangaa sana kuwaona kina TB joshua wakijeweka kundi moja na kina Paulo wa enzi zile
 
Kuwa na watu kama hao kwa sasa ni ngumu kidogo mkuu!
mi huwa nashangaa sana kuwaona kina TB joshua wakijeweka kundi moja na kina Paulo wa enzi zile

Kwa Lugha rahisi tunaweza kuwaita Manabii wa uongo sasa Kwani kwa sasa hatuwezi kua na watu Kama wale!

Vipi Kuhusu Imani zetu Maana Kama hatuwezi kua na watu Kama wale ina Maana kwa walimwengu wa Leo Imani zetu ziko chini sana ya kiwango na kwa Maana hiyo uzima wa milele kuuona ni kazi!?
 
Ni kazi kubwa sana kuuona huo uzima wa milele kwa kupitia hawa watumishi wafufua misukule! cha muhimu ni kila mtu kukomaa kwa imani yake haswa ile ya mwanzo..
 
Taarifa yako haipo sahihi hata kidogo.

1. Kwanza mkutano wa Injili haujaanza bado mjini Moshi hadi tarehe 20/10/2013

2. Watu waliofikwa na majanga makubwa ya kuchukuliwa misukule. Kanisa huchukuwa jukumu la kuwahudumia Kiroho na kumwili hadi wafikie kiwango cha kusimama wenyewe kwa maombi.

si ajabu shule umeenda, halafu una comment huu ujinga !
Haishangazi, maana mna nunua picha dukani kisha mnatundika sebuleni halafu mnawaambia watoto wenu: huyu ni BWANA WETU !
 
si ajabu shule umeenda, halafu una comment huu ujinga !
Haishangazi, maana mna nunua picha dukani kisha mnatundika sebuleni halafu mnawaambia watoto wenu: huyu ni BWANA WETU !

umekumbusha mbali sana mkuu!
ni kipindi cha muvi ya YESU, akili fupi nyingi huamini yule ndiye YESU
 
Ni kazi kubwa sana kuuona huo uzima wa milele kwa kupitia hawa watumishi wafufua misukule! cha muhimu ni kila mtu kukomaa kwa imani yake haswa ile ya mwanzo..

Mkuu Samahani kwa maswali Yangu!
Tunaweza ifikia Ile Imani ya mwanzo iwapo ata Hawa wanatuongoza hawana huo uwezo Kama punje ya mbegu ya Aladari? Tunaweza kweli?

Ndio Maana Mimi wakati mwingine Hua naamini Ufufuo Upo kwa Yule mtoa uhai! Sisi sio watoa uhai na Imani zetu ni chini sana Kama ulivyosema kua ni kazi. Sasa tutaweza Vipi kufufua watu ingawa Maandiko yametupa nafasi ya kufanya hivyo?
 
maandiko hayazungumzi juu ya kufufua misukule!
labda kama wafu na misukule inamaana moja
 
Kuna mtu alisema wanaombea wagonjwa na wanapona,sasa swali la kujiuliza kwanin wasiwe wanaenda hospital moja kwa moja? Na kama umate umate si watapewa na ndugu wa wagonjwa?

Si na mikocheni walikua wanafufua misukule?iliishia wapi?
 
Ni kazi kubwa sana kuuona huo uzima wa milele kwa kupitia hawa watumishi wafufua misukule! cha muhimu ni kila mtu kukomaa kwa imani yake haswa ile ya mwanzo..

Mbona inakuuma sana misukule ikifufuliwa? Nina wasiwasi kuwa unawachukua wewe, wakati watu wanafurahi wachawi kupigwa mpaka wanawaachia watu waliowaiba wewe unachukia, mwanga nini wewe? Na mtakoma mnajifanya dunia ndio yenu hii msijue kuwa ni ya Mungu.

Mungu aumbe watu wake nyie mkawafiche kwenye dali na kwenye uvungu wa nyumba, mwisho wenu umefika.
 
Maisha ya kimwili Si bora Kama maisha ya kiroho! Ni Vema kuponya Roho kwanza kuliko mwili!

Unaiponyaje roho, halafu ukitumia Roho yenye herufi kubwa maana yake ni Roho ya Mungu, roho ya mwanadamu inaanza kwa herufi ndogo.
 
Maneno yenu yanafanana kabisa na wale waliokuwa wakimkebehi Yesu msalabani wakisema na ajiokoe mwenyewe sasa!!! Kama Yesu mwenyewe aliitwa mchawi na kudhihakiwa itakuwa hawa watumishi wake?

Binafsi najua kuna usanii mwingi siku hizi na pia siendi ovyo kwenye makanisa ya kilokole lakini pia sibezi kazi ya Mungu kupitia wachungaji kisa tu kuna wasanii.Kama ni usanii nitafanya utafiti wangu mwenyewe kupitia mafundisho yake na huduma yake ili kupitia matunda ya huduma yake nijue kama kweli ni mtumishi wa Mungu.

Ndg yangu katika Kristo umenena vizuri, utafanya utafiti. Wakati wautafiti wako na kushauri umuombe sana Mungu akusaidie na akupe ufahamu upate maarifa. Maneno ya Mungu yanatuambia kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Tena siku za mwisho kutakuwa na manabii wa uongo. Utawajuaje hawa manabii wa uongo,Yesu mwenyewe anatuambia kwa matendo yao. Sasa jiulize wakati wa Yesu hakukua na wachawi au misukule? Kwanini Yesu hakuhangaika na misukule?
 
Wewe ndio umeuliza vizuri ingawa sina jibu lako kwakuwa sihusiki na huduma ya Gwajima.Umekiri kuwa Yesu anaweza ingawa una mashaka na huduma ya huyu mchungaji kitu ambacho ni cha kawaida kwani hata Tomaso hakukubali kirahisi na Yesu mwenyewe alisema akina Tomaso wapo wengi.

Unaonyesha kuwa unaielewa biblia, unaunajua kuwa Yesu alimtokea tomaso kumtoa mashaka yake. Sasa na watumishi wa leo wanawajibu wakuwatoa mashaka waumini.
 
hivi ule mpango wake wa kumfufua Amina Chifupa uliishia wapi?
 
usishangae haya yanaweza tokea kabisa sikuhizi binadamu tu wanyama sana unambadilisha binadamu mwenzako kuwa mnyama (msukule) na kumtumikisha kazi zako kama punda , ni kweli kabisa baadhi ya binadamu hawafi kwa mapenzi ya mungu bali ni ya binadamu so kumrudisha mtu kama huyo yawezekana
 
Unaiponyaje roho, halafu ukitumia Roho yenye herufi kubwa maana yake ni Roho ya Mungu, roho ya mwanadamu inaanza kwa herufi ndogo.

Umeenda mbali sana kimawazo mkuu!

Sasa mbona sijasikia hao wachawi wakiteketezwa? always ni misukule tuu wasiokuwa na ndugu wala origin yoyote ile,
Wengine wanatoka mochwari,
ref: gwajima akiwa arusha, kuna msukule alisema ametoka mochwari, hapo jiulize alitokaje?

hakuna aliyemwona akitoka? Maigizo igizo tu!
Hakuna ushaidi wa kisayansi kudhibitisha haya maufufuo..
 
Back
Top Bottom