Si jambo jema mwanadamu Kuuwekea Mipaka uwezo wa MUNGU, na hata hivyo MUNGU hapangiwi cha kufanya na mawazo ya mtu, na ndiyo maana anasema mawazo yenu sio mawazo yangu aseme BWANA, lakini swala la utendaji kazi la MUNGU liko wazi sana tena sana kwa maana MUNGU JEHOVA anafanyakazi na wanadamu, ili miujiza itokee kwa ukubwa wowote lazima awepo mwanadamu au kitu kingine chochote ambacho macho ya ulimwengu wa mwili yakiona yataamini kitu kimefanyika. Hivyo mawe, upepo, mvua, paka, njiwa, punda na nk MUNGU anaweza kuvitumia. Mfano MUNGU aliwa kumsemesha Baalamu kwa kutumia punda.Yehova hataki Balaamu alaani watu wake. Basi anamtuma malaika mwenye upanga mrefu akasimame njiani amzuie Balaamu. Balaamu hawezi kumwona malaika, lakini punda anamwona. Basi punda huyo anaepa-epa huyo malaika, na mwishowe analala njiani. Balaamu anakasirika sana, na kumpiga punda wake kwa fimbo ili aendele na safari kwa ajili ya kuwalaani Israel.
Nimeweka mfano huu ili mtoa maada ajue Huwezi kumzuia MUNGU kufanya chochote, hivyo ni vibaya sana kumpunguzia uwezo MUNGU hasa kama unaamini yeye ndiye aliyeumba vyote, na kama huamini kwamba MUNGU yupo na ndiye aliyeumba kila kilichopo pia basi huna sababu hata moja ya kushangaa misukule ikirudishwa hamna cha zaidi kwako.
Mnaoamini fahamu haya. Dunia ipo kwenye kasi kubwa ya kugombea utawala na umiliki, shetani anapigana vita na watu wake wamiliki kila kilichopo duniani ili dunia ihame kutoka mikononi wa mwanakondoo na iangukie mikononi mwa mwa joka, na ndo maana propaganda nyingi zinazuka juu ya kazi ya Uamsho wa MUNGU ili nuru isiwazukie watu na yatimie maneno haya 1.Hosea 4:6 kwamba, Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Isaya 42;22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.
2 Wakorintho 4 : 4 - ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura.
Bahati mbaya sana kwa kukosa ufahamu watu wengi wamekuwa washabiki either wa MUNGU au wa shetani, na kibaya zaidi wengi wa waaminio hatawajibu wao hawaujui, wakati majeshi ya adui yansonga mbele watumishi wa BWANA hata wakipata kibari cha kuachia kamuujiza nako kanaingia kwenye mjadala, kwanini kanaingia kwenye mjadala yaangalie tena maneno niliyo yaweka hapo juu kwa msaada wa YESU.
Agalizo, hiki nikipindi cha kutafuta maarifa na hakika hutapotea, acheni kuwachia watumishi kufanya kila kitu kwa ajili yako na ndiyo maana level ya ufahamu inakuwa tofauti sana kati ya mtumishi na mwamini kiasi kwamba unashindwa kupima roho na wawazo ya kiongozi wako ili uwezekwenda naye sambamba hivyo unatenda dhambi nyingine ya kumsema ovyo.
Mwisho nimalizie kwa kuandaka hivi. usipo waamini watumishi sio rahisi sana kuiona mbingu, kwa sababu MUNGU amewapa ufahamu na maarifa ya kuwaonyesha watu sehemu ya kupita ilikuyafikia mambo aliyo wakusudia. hata kama hutuna manabii, waalimu, wachungaji na wainjilisiti bora haimainishi kwamba umuhimu wao haupo bali ni upungufu ambao utaona matokeo yake katika jamii ya KIMUNGU. hivyo sio jukumu kulaumu kwanini hatuna ni kutafuta njia ya kupona ili awepo kwa sababau ni mpango wa MUNGU wawepo. mfano rahisi ukienda hospitali daktari hayupo unaumwa, haimaanishi kutokuwepo kwa daktari shida yako na umuhimu wake umeshaisha either wewe utaendelea kuwa mgonjwa na hata kufa na suluhu ni kutafuta daktari, matokeo ya kutokuwa na daktari utayaona kwenye jamii ambayo ni taifa la wagonjwa na wanaokufa, na ndivyo ilivyo kwenye mabo ya KIMUNGU.
Nilitamani niishie hapo, lakini Roho Mtakatifu amenisukuma niongeze hili, askari wote wajua vita ikiwakali adui hutafata kujua silaha zako bora ziko wapi, weredi wako ni akina nani na mastadi wako wa kupanga vita ni akina nani, atawawinda hao mpaka awamalize, akishindwa kuwamaliza yeye ndo kaisha na vita inaisha na yeye anakuwa ameshindwa, akiwashinda basi yeye kashinda. Fahamu hili hakika, Kwenye vita ya MUNGU na shetani Juu ya umiliki na utawala watumishi hao akina Gwajima, Kakobe, Malasusa, Pengo, Mze wa Upako, Mlm Mwakasege na wengine wengi ndio wapiganaji wa mbele wa kundi la MUNGU Tanzana, hivyo pote mbali vita wanayokusidia wewe na nchi lakini wao wenyewe wapigwa ile mbaya ile nuru isije kwako maana wakishinda na wewe umeshinda, na bahati mbaya hata wewe umeingia kwenye mtego wa kupigana upande wa adui juu yao.Nakwasabaubu MUNGU alijua ufalme wake haufarakani alisema ukiona chochote WAOMBEE maana alijua wako mstari wa mbele wa adui risasi wanazokwepa ni nyingi kuliko zako. Nakusihi sana Ombea sana mtumishi wako ili anapopigana vita ushindi uje juu yake, yako na taifa lako ili tutawale na kumiliki pamoja na Kristo.