Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ndugu yangu hebu isome Biblia vizuri na uielewe....hiyo nukuu uliyotoa ni O.P.

Mathayo 10:

7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.


Soma kuanzia 5 mpaka hiyo 8 utaona Yesu anawaagiza watu gani?
Na kwanini tena aje aseme yeye ndio Ufufuo na uzima?
 
Hili swala haliitaji kuhudhuria mikutano yake au huduma Zake au kuwaita waumini wake watupatie majibu!
Kwa yeyote anaeufahamu ukweli wa Maandiko kwa hili hawezi kushindwa kulitolea majibu!
Hakuna cha Ufufuo wa Misukule au nini! Usanii mtupu!

Wewe unapaswa kubishana na biblia sio mimi. watu8 kajitahidi kukuwekea maandiko lakini umeamua kubishana tu! Pengine unaabudu Miungu sio Mungu hivyo napoteza muda tu hapa.

Yesu alimfufua Razaro na kutuhaidi sisi pia tukiamini tutafanya zaidi ya hayo hivyo kama wewe huamini ni uhuru wako wa kuabudu lakini usijifanye Mkristo while Ukristo huujui na hutaki kuujua zaidi ya mabishano tu.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu hebu isome Biblia vizuri na uielewe....hiyo nukuu uliyotoa ni O.P.

Mathayo 10:

7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

wala hawawezi kukuelewa.
Maana uwezo wote wanaamini ni wa shetani na siyo Mungu tena
 
Ndugu yangu hebu isome Biblia vizuri na uielewe....hiyo nukuu uliyotoa ni O.P.

Mathayo 10:

7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

Mkuu hivi unaelewa juu ya ufufuo wa Gwajima?
mfano mdogo tu, misukule iliyofufuliwa Arusha hiyo hiyo ndiyo imefufuliwa moshi..

Misukule hawana origin yoyote ile, bado unataka niamini?
 
Wewe unapaswa kubishana na biblia sio mimi. watu8 kajitahidi kukuwekea maandiko lakini umeamua kubishana tu! Pengine unaabudu Miungu sio Mungu hivyo napoteza muda tu hapa.

Yesu alimfufua Razaro na kutuhaidi sisi pia tukiamini tutafanya zaidi ya hayo hivyo kama wewe huamini ni uhuru wako wa kuabudu lakini usijifanye Mkristo while Ukristo huujui na hutaki kuujua zaidi ya mabishano tu.

Mi nilidhani hoja ya Mungi uliielewa pale mwanzo..
inakuwaje tena unaanza kushikamana na maelezo ya watu8? anayetumia refference ya biblia ambayo kila mtu anaweza kuitafsiri kwa jinsi anavyoweza na bado akaeleweka?

lets sticky into reality mkuu!

umeambiwa misukule iliyofufuliwa huko Arusha ndiyo inayoonekana Moshi kwa ufufuo tofauti..
usanii mtupu, afu bado tuamini kuwa YESU anatumika hapo?
 
Last edited by a moderator:
Mi nilidhani hoja ya Mungi uliielewa pale mwanzo..
inakuwaje tena unaanza kushikamana na maelezo ya watu8? anayetumia refference ya biblia ambayo kila mtu anaweza kuitafsiri kwa jinsi anavyoweza na bado akaeleweka?

lets sticky into reality mkuu!

umeambiwa misukule iliyofufuliwa huko Arusha ndiyo inayoonekana Moshi kwa ufufuo tofauti..
usanii mtupu, afu bado tuamini kuwa YESU anatumika hapo?

Narudia tena toka mwanzo nimesema sipo humu kudhibitisha misukule ya Gwajima ni kweli au feki.Msimamo wangu upo wazi post zote.

Unasema hutaki reference ya biblia sasa unataka reference gani? Anyway ebu tafsiri hayo maandiko aliyoweka watu8 unavyotaka wewe tuone! Tumia nukuu hiyo hiyo utoe tafsiri yako hapa!
 
Last edited by a moderator:
Narudia tena toka mwanzo nimesema sipo humu kudhibitisha misukule ya Gwajima ni kweli au feki.Msimamo wangu upo wazi post zote.

Unasema hutaki reference ya biblia sasa unataka reference gani? Anyway ebu tafsiri hayo maandiko aliyoweka watu8 unavyotaka wewe tuone! Tumia nukuu hiyo hiyo utoe tafsiri yako hapa!

Kumbuka pia, anachofanya huyo jamaa ni kufufua misukule na siyo wafu..

Possibly hata huyu jamaa ni mchawi thats why anafanya mambo ya kichawi yaliyojaa mazingaumbwe!!

injili za miujiza kwa sasa nyingi ni za kisanii kaka!
angekuwa
anavunja nguvu za giza zinazosababisha hiyo misukule kidogo angeeleweka!!
 
Last edited by a moderator:
Si jambo jema mwanadamu Kuuwekea Mipaka uwezo wa MUNGU, na hata hivyo MUNGU hapangiwi cha kufanya na mawazo ya mtu, na ndiyo maana anasema mawazo yenu sio mawazo yangu aseme BWANA, lakini swala la utendaji kazi la MUNGU liko wazi sana tena sana kwa maana MUNGU JEHOVA anafanyakazi na wanadamu, ili miujiza itokee kwa ukubwa wowote lazima awepo mwanadamu au kitu kingine chochote ambacho macho ya ulimwengu wa mwili yakiona yataamini kitu kimefanyika. Hivyo mawe, upepo, mvua, paka, njiwa, punda na nk MUNGU anaweza kuvitumia. Mfano MUNGU aliwa kumsemesha Baalamu kwa kutumia punda.Yehova hataki Balaamu alaani watu wake. Basi anamtuma malaika mwenye upanga mrefu akasimame njiani amzuie Balaamu. Balaamu hawezi kumwona malaika, lakini punda anamwona. Basi punda huyo anaepa-epa huyo malaika, na mwishowe analala njiani. Balaamu anakasirika sana, na kumpiga punda wake kwa fimbo ili aendele na safari kwa ajili ya kuwalaani Israel.
Nimeweka mfano huu ili mtoa maada ajue Huwezi kumzuia MUNGU kufanya chochote, hivyo ni vibaya sana kumpunguzia uwezo MUNGU hasa kama unaamini yeye ndiye aliyeumba vyote, na kama huamini kwamba MUNGU yupo na ndiye aliyeumba kila kilichopo pia basi huna sababu hata moja ya kushangaa misukule ikirudishwa hamna cha zaidi kwako.

Mnaoamini fahamu haya. Dunia ipo kwenye kasi kubwa ya kugombea utawala na umiliki, shetani anapigana vita na watu wake wamiliki kila kilichopo duniani ili dunia ihame kutoka mikononi wa mwanakondoo na iangukie mikononi mwa mwa joka, na ndo maana propaganda nyingi zinazuka juu ya kazi ya Uamsho wa MUNGU ili nuru isiwazukie watu na yatimie maneno haya 1.Hosea 4:6 kwamba, Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.

Isaya 42;22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.

2 Wakorintho 4 : 4 - ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura.

Bahati mbaya sana kwa kukosa ufahamu watu wengi wamekuwa washabiki either wa MUNGU au wa shetani, na kibaya zaidi wengi wa waaminio hatawajibu wao hawaujui, wakati majeshi ya adui yansonga mbele watumishi wa BWANA hata wakipata kibari cha kuachia kamuujiza nako kanaingia kwenye mjadala, kwanini kanaingia kwenye mjadala yaangalie tena maneno niliyo yaweka hapo juu kwa msaada wa YESU.

Agalizo, hiki nikipindi cha kutafuta maarifa na hakika hutapotea, acheni kuwachia watumishi kufanya kila kitu kwa ajili yako na ndiyo maana level ya ufahamu inakuwa tofauti sana kati ya mtumishi na mwamini kiasi kwamba unashindwa kupima roho na wawazo ya kiongozi wako ili uwezekwenda naye sambamba hivyo unatenda dhambi nyingine ya kumsema ovyo.

Mwisho nimalizie kwa kuandaka hivi. usipo waamini watumishi sio rahisi sana kuiona mbingu, kwa sababu MUNGU amewapa ufahamu na maarifa ya kuwaonyesha watu sehemu ya kupita ilikuyafikia mambo aliyo wakusudia. hata kama hutuna manabii, waalimu, wachungaji na wainjilisiti bora haimainishi kwamba umuhimu wao haupo bali ni upungufu ambao utaona matokeo yake katika jamii ya KIMUNGU. hivyo sio jukumu kulaumu kwanini hatuna ni kutafuta njia ya kupona ili awepo kwa sababau ni mpango wa MUNGU wawepo. mfano rahisi ukienda hospitali daktari hayupo unaumwa, haimaanishi kutokuwepo kwa daktari shida yako na umuhimu wake umeshaisha either wewe utaendelea kuwa mgonjwa na hata kufa na suluhu ni kutafuta daktari, matokeo ya kutokuwa na daktari utayaona kwenye jamii ambayo ni taifa la wagonjwa na wanaokufa, na ndivyo ilivyo kwenye mabo ya KIMUNGU.

Nilitamani niishie hapo, lakini Roho Mtakatifu amenisukuma niongeze hili, askari wote wajua vita ikiwakali adui hutafata kujua silaha zako bora ziko wapi, weredi wako ni akina nani na mastadi wako wa kupanga vita ni akina nani, atawawinda hao mpaka awamalize, akishindwa kuwamaliza yeye ndo kaisha na vita inaisha na yeye anakuwa ameshindwa, akiwashinda basi yeye kashinda. Fahamu hili hakika, Kwenye vita ya MUNGU na shetani Juu ya umiliki na utawala watumishi hao akina Gwajima, Kakobe, Malasusa, Pengo, Mze wa Upako, Mlm Mwakasege na wengine wengi ndio wapiganaji wa mbele wa kundi la MUNGU Tanzana, hivyo pote mbali vita wanayokusidia wewe na nchi lakini wao wenyewe wapigwa ile mbaya ile nuru isije kwako maana wakishinda na wewe umeshinda, na bahati mbaya hata wewe umeingia kwenye mtego wa kupigana upande wa adui juu yao.Nakwasabaubu MUNGU alijua ufalme wake haufarakani alisema ukiona chochote WAOMBEE maana alijua wako mstari wa mbele wa adui risasi wanazokwepa ni nyingi kuliko zako. Nakusihi sana Ombea sana mtumishi wako ili anapopigana vita ushindi uje juu yake, yako na taifa lako ili tutawale na kumiliki pamoja na Kristo.
 
watu wanaibiwa kweupe,piga pesa Gwajima,watakapo stuka we kitambo ushakuwa bilionea.
a5a8cd6b5dL.jpg



Mtu kama huyu atakuwa ameandaliwa kuletwa kwenye mkutano ili mchuganji ajipatie pesa? aisee!!
 
aisee! Mkuu mawazo yako unayapeleka kama vile inawezekana, ukipiga kelele pale, utaanza kuombewa na wewe kama vile una mapepo..

Ogopa mipango ya watu, inayowapa kula!
ndo kusema hata vijana wa shigongo nawe wameshindwa kufuatilia hii issue ili walete habari za kiuchunguzi.?
 
Mwacheni anatafuta kipato chake kupitia migogo ya wajinga
 
Huwa sipendi kuzungumzia mambo ya imani hasa yanayozungumzia habari ya Yesu Kristo. Lakini kwa hili la kufufua watu imenitia mashaka, kuna watu wengi misukule walijitokeza kwenye mkutano wa Gwajima, baadhi wanasema walikufa miaka 15/20 iliyopita, moja akasema ametoka mortuary alikuwa amekufa wiki mbili zilizopita. Kilichonifanya niwe na mashaka ni jinsi waliofufuliwa hawajulikani kwa mtu yeyote. Nilidhani mtu aliyefufuka angesema yeye ni fulani, alikuwa anafanya kazi sehemu fulani, na ndugu zake ni fulani na fulani, ama balozi wake ni fulani na alikuwa anasali kanisa fulani au msikiti fulani. Bahati mbaya hakuna hata moja aliyejitokeza akajitambulisha.

Mimi nadhani Gwajima alikuja na misukule yake kuwadanganya watu. Kama kweli amefufua watu hebu tujiulize hao watu wako wapi kama siyo amewachukua?

Mungu atupatie maarifa na hekima ya kutambua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Naelewa hofu yako Mungi, jambo ambalo wote tunatakiwa kulifahamu hapa ni kuwa shetani ana uwezo wa kutengeneza a fake death, tukaona mtu amekufa kabisa kumbe amegeuza macho yetu na kuona mtu amekufa kumbe amemchukua (kupitia waganga wa kienyeji na wachawi) na kumuweka kwenye mashamba, viwanda, maduka, masoko, chini ya bahari, to mention just a few.

Ni sheria katika ulimwengu wa roho kuwa kiumbe kinapokuwa katika roho kinauwezo wa kufumba akili za mtu wa kawaida na asiweze kutambua, mfano, Yesu alipofufuka alikuwa na umbo la rohoni na hivyo aliweza kuwafumba akili wanafunzi waliokuwa wanakwenda Emau wasiweze kumtambua na akaongozana nao bila wao kumtambua.

Pia Yesu aliweza kuwatokea baadhi ya wanafunzi akiwa na umbo jingine, hiyo ni sheria ya rohoni ya kubadilisha maumbo ambayo viumbe wa rohoni wanaweza kuitumia. Shetani ni roho pia kwa hiyo anaweza kuwafumba watu akili wakadhani kuwa ndugu yao amekufa kumbe hajafa yupo sehemu anatumika.

Kwa bahati mbaya ukristo wetu umeshindwa kuyafahamu maarifa haya na ndio maana shetani is taking the upper hand kufanya hujuma juu ya mwanadamu.

Kwanini shetani anafake kifo, kuna faida gani kufanya hivyo. Jibu ni kuwa Mungu amewapa watu nyota au viashiria vya mafanikio kabla hata hawajazaliwa, shetani anaweza kuona nyota hizo (kama mamajusi au wachawi walivyoona nyota ya Yesu). Anachofanya anamchukua mtu mwenye nyota hiyo na kwenda kumuweka kwa mtu anayemwabudu yeye ili kupata mafanikio yale ambayo yule aliyechukuliwa alitakiwa kuwa nayo.

Wenye maarifa haya asilimia 95 wanaongoza dunia leo katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kibiashara, kiuchumi, n.k Wewe unaweza kuona meli imezama ukafikiri ni tukio la kawaida kumbe watu wamechukuliwa kichawi na wapo sehemu wanafanya kazi.

Gwajima is one of the very few servants of God in the World wenye maarifa haya. Watu wa Arusha wamethibitisha wenyewe maana for the first time he has preached in Arusha na baadhi ya watu wamewaona ndugu zao. The possibility kuwa watu hao hawafahamiki ni kweli kwa sababu mtu anaweza kufa kichawi Mbeya kumbe amepelekwa Arusha kulima au kufanyishwa biashara, who will know him. Haya mambo ni bayana na siku zinavyozidi kuendelea Mungu atayaweka wazi na ndipo mtakaposhangaa kuona kumbe viongozi wenu wengi wamepanda na kuwa hapo walipo kwa sababu ya these evil and satanic acts.
 
Mkuu hivi unaelewa juu ya ufufuo wa Gwajima?
mfano mdogo tu, misukule iliyofufuliwa Arusha hiyo hiyo ndiyo imefufuliwa moshi..

Misukule hawana origin yoyote ile, bado unataka niamini?

hivi anafufua mbele ya umati,kwa maana ya kubomoa kaburi na kumfukua mtu au anakuja nao kwenye msafara wake?
 
:A S 39: Shetani ni baba wa uongo! ameshindwa na atashindwa kama jinsi ilivyoandikwa uzao wa yule mwanamke utakiponda kichwa chake!!
 
hivi anafufua mbele ya umati,kwa maana ya kubomoa kaburi na kumfukua mtu au anakuja nao kwenye msafara wake?

Hahahaha! haya ndio maswali ya msingi! si kupinga uweza wa Muumba wetu akiamua kufanya jambo ili tuamini yeye ndiye Mungu wa miungu!!
 
Ufufuo wa Misukule; mi ni kizani mtu anakwenda kaburini Na kuoita jina la Mfu alie ndani ya Kaburi jina lake na na kumuamuru.AFUFUKE Kama alivyofanya Yesu pale alipomfufua Razaro!

Kumbe Ufufuo wa Misukule? Yani wale watu kwetu sisi huwa wanawekwa kwenye Dali la nyumba ndani kichawi! Sasa Kama ni Hao watu sina Comment yeyote kwa Hilo Kwani anavyofanya anafaham mwenyewe! Lakini kwa Wafu wa Makaburini mi niko Tayari kuongozana nae nikamuone anaamuru Mfu alie ndani ya kaburi na kufufuka!
 
Mkuu hivi unaelewa juu ya ufufuo wa Gwajima?
mfano mdogo tu, misukule iliyofufuliwa Arusha hiyo hiyo ndiyo imefufuliwa moshi..

Misukule hawana origin yoyote ile, bado unataka niamini?

Mbona maswali yangu pale juu hujanijibu mkuu!!

Binafsi kabla ya kuanza kumzungumzia Gwajima na habari zake nilikuwa naomba tuwekane sawa kwanza

Ndio maana nikaanza kwa kuuliza yale maswali machache pale awali.

NB:
Naomba unijulishe kitu, hivi hii thread ni kwa ajili ya kumdiskasi Gwajima au habari za miujiza za Kristo???

Kama ni kumdiskasi Gwajima basi naomba niishie hapa, unless tunaeleweshana kuhusu nguvu ya Kristo.
 
Soma kuanzia 5 mpaka hiyo 8 utaona Yesu anawaagiza watu gani?

Waliokuwa wakiagizwa ni Thenashara ambao walikuwa wanawakilisha wale wote watakaoliamini jina la Kristo.

Alichoagizwa Petro, Yohana, Filipo na wengineo ndio hicho hicho unachoagizwa wewe uaminiye.

Kama Petro aliambiwa afufue wafu, aponye wagonjwa iweje wewe mwenye imani sawa na Petro ushindwe??


Na kwanini tena aje aseme yeye ndio Ufufuo na uzima?

Maandishi katika rangi nyekundu ndiyo jibu la swali lako:

Yohana 11: 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
 
Back
Top Bottom