Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Mkuu mimi sitaki kuamini kama ni ugumu wa maisha tu ila pia na ubinafsi na zaidi kutomtii Mungu katika amri zake maana kuna sehemu zinasema usidanganye,mimi ni Mkristo ila napinga kabisa huu udanganyifu unaofanywa na hawa wanaojiita mitume.......jamaa wananikera sana......

Apostles wa miaka hii ni wezi tu
 
mhn! kazi ipo sijui nitweza kuchangia vizuri.
lakini kwa kuanzia yote yanawezekana watu wanatakiwa waelewe kunatofauti kubwa kati ya ufufuo aliofanya Yesu na huu wa misukule.
misukule ni watu ambao kiukweli hawajafa katika ulimwengu wa roho wapo wanatumika kuzimu kwa shughuli za watu
hivyo kwa imani wanaweza kurudi kwakuwa wapo hai na ni watu wengi mno wanakufa kwa namna hii kuliko watu wanavyoweza kufikiri
hivyo zikifanyika ibada za maana hawa watu wanaweza kurudi. na kwa bahati nzuri hawa wanaeleza vizuri kuwa wanafufua misukule sio wafu tabu iko wapi.
lakini katika mikutano hii lililo la maana si maajabu yanayotokea lakini ni jinsi gani unaweza ukafunguliwa kwa neno la MUNGU na kuaacha njia zako mbaya hili ndio muhimu ( kama mtu anaenda kwenye makanisa kwa kufuata miujiza atamaliza makanisa na anaweza asifunguliwe kwa kuwa muda wa kumfungua hazami katika nafsi yake kwa imani na yeye akafunguliwa.
kiukweli kila mtu anaweza kufanya hayo kama atakaa kwenye uwepo wa MUNGU.
1NOVEMBA karistatic mtoni kijichi watakuwa na semina hizi kwa watu wote zitaanza jioni hebu nenda kajifunze kitu na kicha watakufundisha ni jinsi gani unaweza kujifungua mwenyewe bila hata kuwekewa mkono.
sijajipanga vizuri lakini jana nimemaliza mkutano wa Damu ya Yesu na nimeona ni kwa jinsi gani watu wamefunguliwa iliyofanyyika dodoma nitawapa maelezo siku zijazo kama nilivyofanya kwenye maumivu ya ndani kwa wale waliofatilia kuna kitu walipokea.
tabu yetu tunapenda mno tamthilia kiasi kwamba tunahitaji kuziona hata madhahabuni
 
Mimi ni Mkatoliki lakini ninayeamini YESU aliyesema kwa imani hata milima itang'oka sembuse haya?
Pondeni wachungaji lakini acheni kulimit uwezo wa Mungu.
Mleta mada ungesema huamini kama wale misukule kweli nisingeshangaa lakini futa kauli ya kutoamini miujiza kwavile huoni kanisani kwako.Mimi kwenye mikutano ya Karistimatic nimeshuhudia miujiza mizito hivyo sishangai uwezo wa Mungu.
Mim ninataka

hao wachungaji wanifanyie Miujiza nipate Pesa na niwe Tajiri wa Dollar Billioni 1 nitaamini kama ni kweli

hao Wachungaji wana uwezo wa kufanya miujiza. Hakuna kitu cha miujiza wala nini uongo mtupu. Bwana Yesu alisema hivi

Mathayo, Chapter 7

[SUP]7:15[/SUP] Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

[SUP]7:16[/SUP]
Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

[SUP]7:22[/SUP] Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

[SUP]7:23[/SUP] Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu

Kwa Ushahidi wa aya hizi 4 za Biblia hakuna cha hao Wachungaji kufanya miujiza ni Manabii wa uongo kama alivyosema

Bwana YESU. Bwana Yesu tu ndio aliyepewa uwezo wa kufanya miujiza ya kufufuwa watu waliokufa walibakia hawa

wachungaji wanafanya mambo ya uchawai wa Ki Nigeria tu hakuna cha miujiza hapo ni mambo ya uchawi tu.

Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..
Sijui umeandika Baada ya kusikia maneno ya mitaani au umedodosa kitoka Kwa wahusika. Unaweza chekelea kuanzisha post Yenye kashfa ukafurahiwa Na Kuungwa mkono Na wengi lakini maskini unajinajisi Na kulitusi usilolijua..
 
ujue kuna vitu vingine hata huwa havihitaji elim au upeo mkubwa kuvitambua hata kama mnajifanya mnaimani kiasi gani
kiukweli kuna mambo yanatendeka kwenye nyumba za ibada ni laana tupu na machukizo kwa mwenyezi mungu.

hivi hata siku 1 ulisha wahi sikia hao wanao fufuliwa au kuponywa huwa wanafahamika katika maisha ya kawaida?
wewe unamajilani wangapi au ndugu wangapi walio pewa huduma hiyo akama sio kushuhudia tuuu watu usio wafaham kila siku?
inamaana hao ndugu wanao fufuliwa kila siku katika umati huo mzima wakanisa huwa wanakuwa hawana hata ndugu? na je huwa wanatoka wapi?

acheni kucheza na mungu kwa malengo yenu ya kujiingizia vipato
 
hata upumbavu ni unajisi pia....kama kuna unalolijua na lililodhibitishwa hapa juu ya ufufuo wa misukule wanaofufuliwa na Gwajima uweke hapa huo ushaidi wako, na utuambie hao misukule waliofufuliwa huwa wanapelekwa wapi
Na utuambie pia kama kuna ndugu zao waliojitokeza kusema kuwa ni watu wanaowajua...
 
Sijui umeandika Baada ya kusikia maneno ya mitaani au umedodosa kitoka Kwa wahusika. Unaweza chekelea kuanzisha post Yenye kashfa ukafurahiwa Na Kuungwa mkono Na wengi lakini maskini unajinajisi Na kulitusi usilolijua..

Naona kunahaya maswali pia aliyauliza huyu mkuu hapa...hebu jibu unitoe huo unajisi.....

ujue kuna vitu vingine hata huwa havihitaji elim au upeo mkubwa kuvitambua hata kama mnajifanya mnaimani kiasi gani
kiukweli kuna mambo yanatendeka kwenye nyumba za ibada ni laana tupu na machukizo kwa mwenyezi mungu.

hivi hata siku 1 ulisha wahi sikia hao wanao fufuliwa au kuponywa huwa wanafahamika katika maisha ya kawaida?
wewe unamajilani wangapi au ndugu wangapi walio pewa huduma hiyo akama sio kushuhudia tuuu watu usio wafaham kila siku?
inamaana hao ndugu wanao fufuliwa kila siku katika umati huo mzima wakanisa huwa wanakuwa hawana hata ndugu? na je huwa wanatoka wapi?

acheni kucheza na mungu kwa malengo yenu ya kujiingizia vipato
 
tuwache kuingiza neno la mungu
kwenye ushabiki usiokuwa na mpango Mungikama unakataa kitu kataa kwa neno mimi neno la mungu linaniambia nikimwamini nitafanya zile kazi yesu alikuwa anazifanya tena na kubwa zaidi ya hapo sioni koza kunyanganya mchawi mtu na kuleta kwa yesu
kwani watu wanaopinga tu kwa akilizao ndio mwisho wa akili zao

Haya mambo yanakanganya, kuna hoja hapa JF iliyokuwa inataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu, mnyinda hukujitokeza, naamini kuna baadhi ya watu wanashindwa kufanya logical and critical analysis ya matendo ya hawa wachungaji/makasisi/masheikh na hata waganga wa kienyeji, wanakimbilia kusema maandiko yamesema. maandiko yasituondolee uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo, daima tulinganishe maandiko na reality, kwangu mimi Mungi ameibua mambo ya msingi sana. Ingekuwa ni jambo la maana sana iwapo ungefanya utafiti na ulete majibu ya maswali ya Mungi badala ya kumponda kuwa analeta ushabiki.
 
Last edited by a moderator:

Jambo ambalo mimi bado najiuliza ni kwamba Mchungaji Gwajima alifanya mikutano Arusha, ikasemekana aliwafufua watu wa Arusha, maana katika hali ya kawaida sijui kama anakuja Arusha kufufua watu wa Burundi. Ili imani ya watu ikue katika habari ya ufufuo, na kwakuwa hata Arusha wapo waliokufa, angefufua watu wa Arusha ili kuwajengea watu imani.
Mpaka sasa najiuliza wale misukule 20 waliofufuliwa Arusha wako wapi?
 
mimacho.jpg
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..
 
Jambo ambalo mimi bado najiuliza ni kwamba Mchungaji Gwajima alifanya mikutano Arusha, ikasemekana aliwafufua watu wa Arusha, maana katika hali ya kawaida sijui kama anakuja Arusha kufufua watu wa Burundi. Ili imani ya watu ikue katika habari ya ufufuo, na kwakuwa hata Arusha wapo waliokufa, angefufua watu wa Arusha ili kuwajengea watu imani.
Mpaka sasa najiuliza wale misukule 20 waliofufuliwa Arusha wako wapi?

CC; Eng. Y. Bihagaze
 
Last edited by a moderator:
kuna mengi yakufanya zaidi ya kuigiza na misukule..
Kuna mafundisho mengi sana ambayo watanzania wanayahitaji katika kujikwamua na umaskini..
Umasikini wa kwanza ni fikra,tukiweza kujikwamua hapo ndio umasikini mwingine unaondoka kiulaini kabisa.Ndio maana wanachofanya wanaojiunga jeshi ni kuondolewa kwanza uraia kwa njia ya kubadilisha fikra zao,ili wajione ni wanajeshi na baada ya hapo,anakuwa mtii kwa kila atakaloambiwa.Hivyo lazima kwanza tuanze na fikra ikiwa mojawapo ni hii ya Imani.
 
kazi ipo nasema! WAMFUFUE NA NYERERE AJE KUREKEBISHA MAUJINGA YALIJAA CCM SASA HIVI! kuanzia div 5 mpaka safari za mkulu nje ya nchi ambazi hazina idadi, puuuuuuuuuuuuuuuuuuu1
 
ni ubunifu tuu ndugu yangu. Hakuna umaskini mbaya kama wa fikra hakika. Na akumbukwe huyu mzee Religion is the opium of the poor
 
kazi ipo nasema! WAMFUFUE NA NYERERE AJE KUREKEBISHA MAUJINGA YALIJAA CCM SASA HIVI! kuanzia div 5 mpaka safari za mkulu nje ya nchi ambazi hazina idadi, puuuuuuuuuuuuuuuuuuu1

aisee wanasema kuna tofauti kati ya wafu na misukule..nadhani nyerere ni mfu na siyo msukule..
 
Back
Top Bottom