Boss naomba nikupe mfano kisha tunaweza kukubaliana kutokukubaliana......
Mfano: Wewe Kalamu una kampuni yako inaitwa Kalamu group of companies ltd inayohusika na vyakula na Mungu akafungua milango ukapata tenda ya kusuply chicken wings(Pure breed) kwenye hoteli kubwa za nyota tano kwa bei nzuri kwa mwaka mzima, ukasain contract ukawa na eneo lako la eka moja ukaamua kuwafuga hao kuku na pale wanapokuzidi ukachukua kwa wafugaji wengine. Je Mm Tsh nikikuambia ufugaji wa kuku hauna faida utanielewa?
Hapa ndipo unapochanganya na kuchanganyikiwa mwenyewe.
Wewe ni mfuga kuku, 78, au hata 500, potelea mbali. Hiyo ndiyo kazi yako.
Kwa hiyo tuseme wewe ni mfugaji mdogo wa kuku, kwa kiasi hicho unachofuga.
Kuna gharama unazoingia tokea hao kuku wanaingia nyumbani/shambani kwako. La hasha, gharama unaanza kupambana nazo pale tu unapoanza kuwa na wazo la kufuga, kwa sababu kutakuwa na maandalizi, kabla ya hao vifaranga/kuku hawajaingia hapo shambani kwako.
Na gharama zitaendelea kuongezeka kila siku, hadi siku ya mwisho utakapokuwa umewauza wote.
Sasa, ninakuomba uchambue gharama hizo kwa uangalifu mkubwa kabisa na uziweke pembeni. Usisahau, au kuacha kuweka gharama hata ndogo tu, inayohusiana na ufugaji wako huo. Kwa mfano, usidharau kuiorodhesha ile shilingi mia tano uliyotumia kwenda kutafuta matakataka au masalia ya chakula, au hata matumizi tu ya simu yako kutafuta wapi utapata wanunuzi wa kuku wako.
Kwa hiyio wewe kama mfugaji mzuri, eneo hilo la kumbukumbu zako za ufugaji umelimudu vizuri.
Sasa nenda kwenye mauzo ya hao kuku.
Ninavyokuelewa hapa unavyojieleza ni kwamba umepata tenda ya ku'supply' hotel? Kwa hao kuku 78 au 500; ukapata tenda? Au kuna kazi nyingine unaifanya ambayo ni mbali kabisa na ufugaji? Kama hivyo ndivyo, basi usichanganye, hizi ni kazi mbili tofauti, na kila moja yake inajitegemea katika maswala ya biashara, na faida kila moja inachambuliwa mbali na nyingine.
Sasa, katika kazi ya ufugaji, hakikisha hao kuku wako 78, au 500 unapowauza, iwe ni huko hotelini, au kwa walanguzi wenye tenda huko mahotelini, mauzo yake yaweke pembeni, na uyalinganishe na gharama zako za ufugaji. Unapolinganisha Mauzo na matumizi, hapa ndipo utajua kama umepata faida ya kazi yako ya ufugaji, au la.
Na nikuhakikishie, kwa mara nyingine tena, kuwa katika kuku wako hao wa kienyeji 78, ay 500, iwe unauza mayai, au unawauza kwa nyama, pamoja na hata ukiuza manyoa na mavi yake kama mbolea, hutaambulia faida yoyote ile kwa hali ya soko letu ilivyo kwa sasa hivi.
Kama kuna huyo mlanguzi atakayekuja kununua kuku wako, kwa bei ya hsara kwako na kwenda kuwauza hao kuku huko mahotelini kwa hiyo tenda unayozungumzia, hapo ssasa, huyo mnunuzi wako anaweza akaingiza faida kwake, na siyo kwako wewe mfugaji.