Amani iwe nanyi!Nikitambo sijachangia uzi huu sio kwa sababu sikuwa na interest nao la hasha!Kwa kipindi kile uzi huu ulikuwa kama functionless kwangu kutokana na mazingira yangu hayakunuruhusu kabisa kufuga kibiashara ingawa nilikuwa natamani kufuga.Nikaona ni busara niweke uzi huu mkuu kama hazina hivyo kuamua kujiweka bize kutafuta njia za kujikwamua na mazingira yale,katika njia za kufanikisha hilo nimejukuta kwa miaka miwili iliyo pita nimepitia katika wakati mgumu na maisha yakukatisha tama sana ndugu wana jf hatahivyo,namshukuru MWENYEZI MUNGU kwa sasa ninavyo andika hii post nipo mahali ambapo naweza kufuga na kuwekeza katika miradi mingine,na nimeanza kufanya hivyo kwani hivi sasa nina kuku wakubwa kumi na nne na vifaranga kumi na tatu napia natarajia mnamo tarehere mbili mwezi huu kuwa na vifaranga wengine 25-30 kwani kuna kuku watatu wamelalia mayai thelathini.Nafikiri huu ndio umekuwa wakati wangu muafaka wa kutafuta hazina yangu ambayo ni hii thread,nashukuru kwa sasa uzi una michango mingi tofauti na hapo awali nilipo ishia ulikuwa na pages 13 ila kwa sasa una pages 43 naomba niwapongeze kwa hilo na naomba msikate tamaa kutuelimisha.Nimesomo pages zote na sasa nitaendelea kutoa mrejesho wa maendeleo ya ufugaji wangu ingawa ni mvivu kidogo kuandika ila nitajitahidi kadri ya uwezo kwa hili kuhakikisha nami natoa nilichokipata kwa manufaa ya wenzangu.MUNGU akubariki Kubota MUNGU awabariki Mama Joe,Chasha, Liverpoolfc,MamaTimmy,Guta,Fidel80,Aza,Asigwa,Chamilitary,Ankoeli,Poutry Sayuni na wengine wote ambao nimewasahau.