Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ndugu bora ungeniambia magonjwa!
Mradi mkubwa kama huwa mwewe ndo anakupashida, you are not serious!
 
Hongera kwa ufugaji wenye mafanikio lakini pole sana kwa huyo adui kipanga kama wanavyomuita wadau.. nazani ni wakati wa kutafuta njia sahihi ya kuwafungia kuku wako kwani kesha watambua walipo na atakuwa anarudi kila muda kuku athiri... inabidi uumize kichwa kujua jinsi ya kuwalinda kuku wako mkuu
 
Wakuu, nimeanza tena ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mara hii natumia mfumo
wa NUSU HURIA nimeanza na kuku 15 mwaka Jana mpaka sasa wako 369
Nimeuza kuku 271 kwa bei za kati ya Tsh 17,000 mpaka 23,000 namshukuru
Mungu nimeweza kupunguza ukata.

Mwakahuu kuna ttizo kubwa limejitokeza nashindwa jinsi ya kulikabili, Kuna ndege
Mdogo kwa umbo anafanana sana na njiwa, anakamata vifaranga balaa. Tena
anakamata wale vifaranga wakubwa ambao wanajitegemea. Ndani ya wiki mbili
hizi amekamata vifaranga 18.

Sijajua jinsi ya kumdhibiti yaani huyu mshenzi ananipa hasira si mchezo.
mkuu wapake rangi hao vifaranga
 
mimi huyu mshenzi(kipanga) nilifanikiwa kumuangusha na kumuua papo hapo. Nilitafuta wavu wa kamba ya manira, kisha nikatengeneza kitu mfano wa kizimba cha goli, baadhi ya vifaranga hua nawaweka pale wacheze na kula msosi. Ule wavu kwakua una nyuzi nyembamba sana kiasi cha yule bwana akiwa angani anapiga doria yeye hawezi kuuona ila anaona vifaranga tu. Basi alikuja speed kama ndege vita, kilicho mpata anakijua mwenyewe lakini mimi nilimkuta pale pembeni ya mtego akiwa hoi taaban.
 
Ivi nikweli mnafikisha kuku wote hao mana mimi natotolesha vifaranga hadi 50 lkn vyote huisha na kufa tu wanalegea tu .mara adondoke unamsimamisha anaendelea vzr lkn ujue atakufa tu .nmekata tamaa na ufugaji kabsa.npeni mbnu wadau.
Marufuku kukata tamaa pambana mkuu
 
daaah yaani ningekwa mimi namsaga kabisa anakuwa ujiuji.....
 
Dawa ni hii

Wapake rangi ya Ukili au ile rangi inayopakwa kwenye Mikeka yaani wapake kiwiliwili chote, kuna rangi nyekundu,blue manjano au yeyote ile hii itamfanya kuku aonekane kiumbe cha Ajabu
fc914dc56828ab49a721ece007f1ee43.jpg
cec46d97edd1722ea647eba139c0a8bd.jpg

eti kiumbe wa ajabu ha ha ha ha ha
 
Ivi nikweli mnafikisha kuku wote hao mana mimi natotolesha vifaranga hadi 50 lkn vyote huisha na kufa tu wanalegea tu .mara adondoke unamsimamisha anaendelea vzr lkn ujue atakufa tu .nmekata tamaa na ufugaji kabsa.npeni mbnu wadau.
Ufugaji una changamoto zake unatakiwa uwe na mtaji na wataalam wa mifugo ndio wawe rafiki zako. Vifaranga vinahitaji chanjo na chakula cha kukuzia pia madawa kuku wanapougua. Miaka hii kuacha Mungu akutunzie vifaranga wako utaisoma namba
 
Aseee hongera kiongozi ......hivi kuku wako wameshawai kutokwa na vidonda vya usoni vile? Na ulitumia dawa gan maana naona wangu wanaanza kuzingua
Hiyo itakua na ndui nenda kwa dr wa mifugo awachanje.
 
Kwenye sehemu wanaposhinda zungusha nyaya kwajuu. Kama unaweza pata utumbo wa kanda za mziki ukizungusha hapo kipanga au ndege yoyote akija ni ama atakwama kutua au wakati wa kuondoka atatatizika sana hadi umkamate.
 
Kuna Jambo Moja Naomba niliweke sawa na Ikiwezekana Mlifanyie kaz

Mwewe Kipanga waonekana ndo Maadui wakubwa
Lakini nataka niwajuze hata hawa ndege wa kawaida (waso madhara) pia wana matatizo yao na Kubwa kabisa ni Kueneza Magonjwa Hususan kwa Vifaranga
Kwa maana watatua watakula na vifaranga Chakula ulowawekea Wata changia Maji Watajisaidia hii ni njia mojawapo ya kuleta Magonjwa

Tiba
Kwa sie tulo jirani na Wavuvu basi Hununua Nyavu (Mitego) yao kwa bei rahisi (reject)
Kisha tunaifunga vzr juu ya Sehem wanayolia Vifaranga

Hivyo Chini kuna Uzio wa Nyavu na juu kuna Uzio wa Mtego

Hapo Haingii kipanga Mwewe wala Ndege wa Aina yoyote yule

9fb5d390f4e16dfef6f16a96a310d3f9.jpg
 
Ninaomba elimu zaidi namna ya kuwatunza vifaranga mpaka wafikie umri wa kuitwa kuku kwani tangu nimeanza kufuga sijawahi kufanikiwa kufikisha zaidi ya kuku 50,sijui ninakosea.

Wanaweza wakaanguliwa vifaranga mpaka 80 kwa wakati mmoja lakini baada ya muda mfupi vifaranga wote wanakufa,Leo anaweza akafa kifaranga mmoja kesho 2,kadri siku zinavyozidi kuongezeka na idadi ya vifaranga vinavyokufa nayoinazidi kuongezeka mpaka vinaisha vyote.

Vifaranga vikianguliwa baada ya Kama wiki 2 kupita pengeni vinaweza vikamaliza hata mwezi mmoja baada ya hapo vinateguka miguu na kuanza kutambaa Kama vimeteguka kiuno na haipiti hata siku moja tangu kuonyesha dalili hizo vinakuwa vimesha kufa.

Kama havitakufa kwa ugonjwa wa kuteguka miguu na kutetemeka utakuta vimeshusha mabawa Kama vimevaa koti,wakati mwingine vinapatwa na mafua yasiyoisha hata nikivipa fullban vipi pamoja na vitamin haviponi mwisho vinaishia kufa.

Sijui ni utaratibu gani ambao ninaweza ni kautumia pamoja na tiba ambayo ninaweza nikaitumia kwa ajili ya kumaliza tatizo hili kwa kuku Hawa wa kienyeji ambao ninawafuga kwa mfumo wa ufugaji nusu huria.
 
Ninaomba elimu zaidi namna ya kuwatunza vifaranga mpaka wafikie umri wa kuitwa kuku kwani tangu nimeanza kufuga sijawahi kufanikiwa kufikisha zaidi ya kuku 50,sijui ninakosea.

Wanaweza wakaanguliwa vifaranga mpaka 80 kwa wakati mmoja lakini baada ya muda mfupi vifaranga wote wanakufa

Mkuu kama uko Serious Ukipitia Jumbe zote ziloandikwa ktk uzi huu
Basi utayaona Mapungufu yako na Utajirekebisha
Ila kama Unataka majibu ya Jumla
Basi zingatia Yafuatayo

Chanjo usafi wa banda joto stahiki lishe bora
 
Mimi nimezingatia yote nabado mwezi uliopita mia na sita(110) vimeisha vote sikuambua hata moja na kuku nao wamekua kama wamesusa kutaga katika kuku 20 wametaga watano tu nime atamisha wa3
 
Wapatie chonjo zote kama chanjo ya kideli(new castle disease), fowl pox( nduli),Ngumboro pamoja na dawa minyoo na kuweka safi mazingira ya banda

Haya mkuu:
Kideli = Kideri
nduli = ndui
Ngumboro = gomboro. Ukienda dukani ulizia dawa za magonjwa hayo sio majina uliopewa na huyo mtaalam
 
Back
Top Bottom