Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu wapake rangi hao vifarangaWakuu, nimeanza tena ufugaji wa kuku wa kienyeji. Mara hii natumia mfumo
wa NUSU HURIA nimeanza na kuku 15 mwaka Jana mpaka sasa wako 369
Nimeuza kuku 271 kwa bei za kati ya Tsh 17,000 mpaka 23,000 namshukuru
Mungu nimeweza kupunguza ukata.
Mwakahuu kuna ttizo kubwa limejitokeza nashindwa jinsi ya kulikabili, Kuna ndege
Mdogo kwa umbo anafanana sana na njiwa, anakamata vifaranga balaa. Tena
anakamata wale vifaranga wakubwa ambao wanajitegemea. Ndani ya wiki mbili
hizi amekamata vifaranga 18.
Sijajua jinsi ya kumdhibiti yaani huyu mshenzi ananipa hasira si mchezo.
Marufuku kukata tamaa pambana mkuuIvi nikweli mnafikisha kuku wote hao mana mimi natotolesha vifaranga hadi 50 lkn vyote huisha na kufa tu wanalegea tu .mara adondoke unamsimamisha anaendelea vzr lkn ujue atakufa tu .nmekata tamaa na ufugaji kabsa.npeni mbnu wadau.
mimi huyu mshenzi(kipanga) nilifanikiwa kumuangusha na kumuua papo hapo. Nilitafuta wavu wa kamba ya manira, kisha nikatengeneza kitu mfano wa kizimba cha goli, baadhi ya vifaranga hua nawaweka pale wacheze na kula msosi. Ule wavu kwakua una nyuzi nyembamba sana kiasi cha yule bwana akiwa angani anapiga doria yeye hawezi kuuona ila anaona vifaranga tu. Basi alikuja speed kama ndege vita, kilicho mpata anakijua mwenyewe lakini mimi nilimkuta pale pembeni ya mtego akiwa hoi taaban.
Dawa ni hii
Wapake rangi ya Ukili au ile rangi inayopakwa kwenye Mikeka yaani wapake kiwiliwili chote, kuna rangi nyekundu,blue manjano au yeyote ile hii itamfanya kuku aonekane kiumbe cha Ajabu![]()
![]()
Ufugaji una changamoto zake unatakiwa uwe na mtaji na wataalam wa mifugo ndio wawe rafiki zako. Vifaranga vinahitaji chanjo na chakula cha kukuzia pia madawa kuku wanapougua. Miaka hii kuacha Mungu akutunzie vifaranga wako utaisoma nambaIvi nikweli mnafikisha kuku wote hao mana mimi natotolesha vifaranga hadi 50 lkn vyote huisha na kufa tu wanalegea tu .mara adondoke unamsimamisha anaendelea vzr lkn ujue atakufa tu .nmekata tamaa na ufugaji kabsa.npeni mbnu wadau.
Hiyo itakua na ndui nenda kwa dr wa mifugo awachanje.Aseee hongera kiongozi ......hivi kuku wako wameshawai kutokwa na vidonda vya usoni vile? Na ulitumia dawa gan maana naona wangu wanaanza kuzingua
Kuku wakishaugua usiwape chanjo ila watibu kwanza, ukiwapa chanjo utawamaliza wote.Hiyo itakua na ndui nenda kwa dr wa mifugo awachanje.
Ninaomba elimu zaidi namna ya kuwatunza vifaranga mpaka wafikie umri wa kuitwa kuku kwani tangu nimeanza kufuga sijawahi kufanikiwa kufikisha zaidi ya kuku 50,sijui ninakosea.
Wanaweza wakaanguliwa vifaranga mpaka 80 kwa wakati mmoja lakini baada ya muda mfupi vifaranga wote wanakufa
Mimi nimezingatia yote nabado mwezi uliopita mia na sita(110) vimeisha vote sikuambua hata moja na kuku nao wamekua kama wamesusa kutaga katika kuku 20 wametaga watano tu nime atamisha wa3Mkuu kama uko Serious Ukipitia Jumbe zote ziloandikwa ktk uzi huu
Basi utayaona Mapungufu yako na Utajirekebisha
Ila kama Unataka majibu ya Jumla
Basi zingatia Yafuatayo
Chanjo usafi wa banda joto stahiki lishe bora
Wapatie chonjo zote kama chanjo ya kideli(new castle disease), fowl pox( nduli),Ngumboro pamoja na dawa minyoo na kuweka safi mazingira ya banda
Hongera sana mdau, nimekupenda bure! Mungu wa mbinguni azibariki kazi za mikono yako!Ni vifaranga mkuu na huwa nawaweka kwa muda fulani huku nikitumia mitungi
maalum ya kuwapa joto View attachment 511933
Mkuu lete mrejesho sasa maana upo kimyaaa!!!NimewaanIshia leo Mkuu