Nawasalim wote......
Baada ya kumaliza degree ya kwanza ya ugavi na manunuzi nimekuwa nikijaribu kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kijasiliamali na sasa nimeamua kuongeza mradi kwa kufuga nguruwe,
Wanajamvi wenye kujua kuhusu namna nzuri ya kuwahudumia nguruwe tafadhalini sana nijuzeni iliniongeze tija ktk mradi huu.
Tafadhalini ushauri ukizingatia yafuatayo utakuwa ni wenye tija zaidi japo simkatazi mtu kunisaidia zaidi;
1,chakula (kipi kizur na ratiba gani nzur kulishia)
2,madawa (kila baada ya muda gan,dawa Zipi)
3,breeding (muda na mbegu ipi ingefaa kupandishia)
4,kitu gani cha ziada nikifanya nguruwe wangu watanilipa zaid (kuongeza uzito na umbile la nguruwe)
Natanguliza shukuran zangu za dhati...!!!