Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Naweza kupata wapi watoto nifuge???Nisaidien kwa hilo kama vp mtu ani PM
 
Mkuu.

Una muda gani kwenye huu ufugaji wa nguruwe?

Una ufanyia mkoa/wilaya gani? (kama hutojali)

Binafsi nimeshahamasika toka kitambo kujihusisha na kilimo hasa ufugaji wa hawa wanyama pamoja na kuku.

Issue ni kwamba nimekuwa nakatishwa tamaa Sana pale ninapowatembelea wakulima/wafugaji wenyewe maana huwa wanaorodhesha challenges kibao mno.

Anyways,shukrani sana kwa ku-share nasi.
 
Ahsante sana kwa kutupa uzoefu ambao hata wanaoshinda na ma - lecturer hawapati. mkuu mm naomba nikusumbue kidogo kuhusu wastani wa gharama ya chakula kwa nguruwe mmoja toka kanazaliwa mpaka mda wa kuuza anaweza akafyonza shilingi ngapi? kama nanunua vyakula mashambani na kuchanganya mwenyewe. mana nipo mbioni kuanza haka kamradi. ukinipa wastani wa mmoja mimi nitajua kwa nguruwe wengi ni kiasi gani natanguliza shukrani mkuu

Kaka nadhani nimeeleza hapo juu. Inategemea unawalisha nn na unanunua wapi chakula.
Kwa around morogoro kwa mfano,kwa formulation ya chakula ninayotumia.
Mwezi 1-2: ananyonya
miezi2-3: anakula around 0.5-1kg/siku,sawa na tshs.3000-6000
miezi 3-5: anakula 2k/siku,sawa na tshs.24,000
Mwezi wa 6 na kuendelea anakula 2kg/siku sawa na tshs12,000

Total=tshs42,000 kwa kadirio la juu. Ofcourse kuna gharama zingine za transport(kama zipo),chanjo(ambayo ni kidogo),mishahara kwa wafanyakazi.
 
Neybro,
Inategemea unafugia wapi na unahitaji wangapi.mi na prefer kuuza wakubwa though unanunua wadogo wengi (at least 10)tunaweza kukuuzia.utahitaji kuwafuata shamba au kama upo dar tunaweza kuwaleta kwa kulipia usafiri.nafugia morogoro,kabla hujafika mikese,160km kutoka dar.kuna faida kubwa kufuga nje ya makazi ya watu.
Bwana Ndagla,
Tuna miezi 18 kwenye ufugaji huu na tunafanya vizuri!
Kaka sijui business gani utafanya isiyo na challenge.Labda ungeweka wazi challenge gani unazojua ili tukusaidie way around.
 
Naomba kujuzwa ujengaji wa,banda la nguruwe kwa kutumia mabao. Nahitaji vipimo
Thank you
 
Kaka asante sana kwa hizi info hakika umesema kweli maana hata mimi mwenyewe ni mfugaji na mfanyabiashara wa hawa wanyama. labda la kusisitizia kwa wadau ambao nao wangependa kuanza mradi wa aina hii ni kuwa ni muhimu kujenga relationship na daktari wa wanyama hao ambaye anaweza kuwa anapita mara moja moja kwa ushauri lakini muhimu zaidi ni kuwa hata ikitokea nguruwe akaugua ghalfa ni rahisi kumpata na pia kijana wako wa shamba pia awe na mawasiliano nae ya moja kwa moja incase shida inatokea na wewe haupatikani/ upo mbali.

Kuhusu formula ya kuanzia nawashauri watumie hiyo 8a maana mimi wakati nimeanza sikupata ushauri mzuri sana hivyo nilianza na 8b so ilinigharimu miezi mingi ya kufuga ili kuweza kupata mbegu. but ili kuweza kumudu gharama za uendeshaji kabla sijapata mbegu ilibidi niwe nanunua nguruwe lets say 10 wa miezi miwili then kati ya hao natenga majike wawili wazuri wa mbegu then hao nane ninawanenepesha baada ya miezi minne nawatoa/nawauza. Maana lengo langu ilikuwa ni kuwa na majike ya mbegu kama 16 ambapo ingeniwezesha kuzalisha nguruwe 2-3 kwa mwezi (basing on the size ya banda langu)

Siri kubwa ya mafanikio ipo kwenye gharama ya chakula maana hiyo inachukua kama 75% ya gharama za uendeshaji. but the business is good and enjoyable na kama eneo lako ni maeneo mjini (karibu na makazi ya watu) unaweza fanya utaratibu wa kuwa na biogas yako hivyo hautakuwa na usumbufu wowote kwa majirani na nishati utaipata pia (Kuna mradi fulani ulikuwa chini ya CAMARTEC huku Arusha walikuwa wanatengenezea watu mitambo ya biogas at a throw away price so na mimi nilibahatika)

Welcome to the club guys.........
 
Upendo kwanza,
Ahsante kwa input nzuri.nadhani wadau watakuwa wamekupata.
Bwana ngamba,
Nguruwe wa kawaida hadi miezi 6 anahitaji 1.5square metre ya eneo.kwa mfano 2mx3m wanaweza kukaa nguruwe 4.overall ukimpa nafasi zaidi,anakua vizuri zaidi.wenye mimba wanahitaji nafasi zaidi .nakushauri tembelea wafugaji kupata design nzuri.kuna namna nyingi za kujenga banda.pia google search,kuna document nyingi kuhusu hilo
 
Malafyale na upendo kwanza big up kwa maelezo mazuri.
Mara nyingi uwa tunatoa maelezo ya mradi fulan bila kuwa makini na yakutosha matokeo yake una sababisha maswali mengi na muhimu ambayo yalibidi yatolewe maelezo kabla hata swali halijaulizwa.
 
Nawasalim wote......
Baada ya kumaliza degree ya kwanza ya ugavi na manunuzi nimekuwa nikijaribu kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kijasiliamali na sasa nimeamua kuongeza mradi kwa kufuga nguruwe,
Wanajamvi wenye kujua kuhusu namna nzuri ya kuwahudumia nguruwe tafadhalini sana nijuzeni iliniongeze tija ktk mradi huu.

Tafadhalini ushauri ukizingatia yafuatayo utakuwa ni wenye tija zaidi japo simkatazi mtu kunisaidia zaidi;
1,chakula (kipi kizur na ratiba gani nzur kulishia)
2,madawa (kila baada ya muda gan,dawa Zipi)
3,breeding (muda na mbegu ipi ingefaa kupandishia)
4,kitu gani cha ziada nikifanya nguruwe wangu watanilipa zaid (kuongeza uzito na umbile la nguruwe)

Natanguliza shukuran zangu za dhati...!!!
 
Last edited by a moderator:
Threads the kitimoto na nyingi humu jf.search "nguruwe" utapata kila unachotaka then kwa ushauri tembelea actual wafugaji kadhaa ili kupata one-to-one experience.
 
Kumradhi wa mlengo tofauti na mnyama huyu,Naomba msaada chakula na virutubisho mhimu kumlisha nguruwe akue haraka.
 
Back
Top Bottom