Mkuu Gidbang heshima kwako kwanza kwa kuwa na bwawa lenye ukubwa huo kwani huo ni mtaji tosha sana kwenye biashara ya ufugaji wa samaki.
Kulisafisha hlo bwawa ni kazi rahisi mno kwani unachotakiwa kufanya kwanza ni kutoa hao samaki wote na vyura waliomo either kwa kutumia net au kwa kutoa maji yote then uwatoe. Njia ya pili ni nzuri kwani hautopata tabu ya kuanza kuwavua kwanza then ndo utoe maji yote.
Baada ya kutoa maji na hao viumbe waliopo, inatakiwa uliache kwa muda wa kama siku moja au mbili then safisha kuta za bwawa kwa kuondoa kama kuna majani yameota ndani kwenye kuta za bwawa. Baada ya hapo toa udongo (tope kwenye sakafu ya bwawa ) kiasi cha sentimeta ishirini.
Baada ya kufanya hayo yote mwaga lime ( chokaa ) kwenye sakafu ya bwawa ili kuua vijidudu vidogo vidogo vinavyoweza kuwepo kwenye bwawa na liache likauke bila kuweka maji kwa muda wa wiki mbili hadi tatu ili kuhakikisha kuwa hakuna aina yoyote ya kiumbe au mmea uliobakia kwenye bwawa.
Baada ya hapo then unaweza kuendelea na taratibu zinazofuata kwenye ufugaji wa samaki katika bwawa lako.
Ahsante!