Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Mkuu Gidbang heshima kwako kwanza kwa kuwa na bwawa lenye ukubwa huo kwani huo ni mtaji tosha sana kwenye biashara ya ufugaji wa samaki.

Kulisafisha hlo bwawa ni kazi rahisi mno kwani unachotakiwa kufanya kwanza ni kutoa hao samaki wote na vyura waliomo either kwa kutumia net au kwa kutoa maji yote then uwatoe. Njia ya pili ni nzuri kwani hautopata tabu ya kuanza kuwavua kwanza then ndo utoe maji yote.

Baada ya kutoa maji na hao viumbe waliopo, inatakiwa uliache kwa muda wa kama siku moja au mbili then safisha kuta za bwawa kwa kuondoa kama kuna majani yameota ndani kwenye kuta za bwawa. Baada ya hapo toa udongo (tope kwenye sakafu ya bwawa ) kiasi cha sentimeta ishirini.
Baada ya kufanya hayo yote mwaga lime ( chokaa ) kwenye sakafu ya bwawa ili kuua vijidudu vidogo vidogo vinavyoweza kuwepo kwenye bwawa na liache likauke bila kuweka maji kwa muda wa wiki mbili hadi tatu ili kuhakikisha kuwa hakuna aina yoyote ya kiumbe au mmea uliobakia kwenye bwawa.

Baada ya hapo then unaweza kuendelea na taratibu zinazofuata kwenye ufugaji wa samaki katika bwawa lako.

Ahsante!
 
Niliamua kufanya utundu kidogo,
Mwaka huu mvua ilinyesha vizuri na hivyo kambale walizaliana sana. Sasa mimi nikapiga mbiu kwa madogo kule Mkuranga karibu na shambani kwangu kwamba nanunua kambale. Nimepata kambale wengi sana, na bado nawakusanya. Kasheshe ni chakula. Mdau mmoja alinitembea na kunihakikishia kunipa formula ili nitengeneze chakula changu mwenyewe, hasa floating pellets.

Hawa kambale pori wako vizuri.

Mkuu unaonaje ukitumia technogy ya Periphyton kwa kusimika mianzi kwny bwawa.
 
Wadau mimi nina fuga samaki aina ya sato na vifaranga nilichukua SUA..mpaka sasa wana kama miezi 6.5 lakini uzito wao sio wa kuridhisha sana kwani 1 anafika gramu 150 mpaka 190..nina mabwawa 4 yote yanasamaki.Je uzito huu na umri wao ni sawa kweli..wataalam naomba msaada

Pole sana kijana walitakiwa wawe na 250-500g, hapo kuna kitu umebugi:

1. Kama ni mixed sex wameshazaliana na kuwa overpopulated kwaiyo wanashindania chakula na hewa. SOLUTION: Fanya polyculture na kambale.

2. Au tangu ulipowaweka uliweka wengi kuliko uwezo wa pond lako. SOLUTION: Wapunguze wawe 3-4 fish/m2

3. Inawezekana hurutubishi. Kama hujui unatakiwa kurutubisha angalau mara mbili kwa mwezi.

4. Tz hakuna mbegu bora za samaki wa kufuga zilizoboreshwa ni tatizo kubwa. Hao samaki wanavuliwa na kuzalishwa.

Kumbuka data za ukuaji tunazopeana ni kutoka mbele ambako wao wameziboresha mbegu zao sasa hapo ni sawa uchukue takwimu za ukuaji wa kuku (broiler) ulaya alaf ww uzilazimishe zifikiwe kuku wako wakienyeji.

Usikate tamaa njia ipo.
 
Mkuu unaonaje ukitumia technogy ya Periphyton kwa kusimika mianzi kwny bwawa.

Asante kaka,

Hiyo kitu niliona kwenye mabwawa ya Caritas, na sasa nimeshaotesha mianzi kwa ajili hiyo siku za usoni. Kuna mahali nimepata mianzi ya kununua,nitafanya hivyo.
 
Nawasalimu wote, mimi niko Arusha ninajianda kufuga samaki na kuku naombeni mchango wa ushauri hasa kwenye samaki
 
Asante kaka,

Hiyo kitu niliona kwenye mabwawa ya Caritas, na sasa nimeshaotesha mianzi kwa ajili hiyo siku za usoni. Kuna mahali nimepata mianzi ya kununua,nitafanya hivyo.

Unaweza pia kutumia miti yoyote ilimradi isiwe na sumu na isiyooza kirahisi ktk maji kumbuka italazimika kuwa kwnye maji kwa kipindi chote hadi uvune ie 6-8 months.

Ni mbinu inayotajwa kuonesha mafanikio makubwa sana ndgu.
 
Asante sana, mianzi ipo mingi nitaitumia hiyo.

Be blessed.
 
Asante sana, mianzi ipo mingi nitaitumia hiyo.

Be blessed.

Amen. Kila la kheri ndg naamini utafanikiwa maana umechagua spp nzuri sana (kambale) kwa ufugaji wa kibongo. Changamoto kubwa ipo kwa wale wafugaji wa tilapia/perege/sato kila kona ya nchi wanalia na kudumaa kwa samaki atleast wanaochanganya sato na kambale wamepata faraja.
 
Kuna kitu nimesahau,
Hujaniambia nafasi kati ya muanzi mmoja na muanzi wa pili.
 
Kuna kitu nimesahau,
Hujaniambia nafasi kati ya muanzi mmoja na muanzi wa pili.

Isimike ktk misitari iliyonyooka spacing msitari hadi msitari ni ni mita moja na mti hadi mti ni mita moja pia.
 
Isimike ktk misitari iliyonyooka spacing msitari hadi msitari ni ni mita moja na mti hadi mti ni mita moja pia.

Pale ktk mradi wa samaki wa Caritas niliona spacing kt ya muanzi na muanzi ni ndogo, chini ya nusu futi halafu kati ya msitari na msitari ndio palikuwa pakubwa.Sikupima. Asante mkuu.
 
Pale ktk mradi wa samaki wa Caritas niliona spacing kt ya muanzi na muanzi ni ndogo, chini ya nusu futi halafu kati ya msitari na msitari ndio palikuwa pakubwa.Sikupima. Asante mkuu.

Ni sawa co sheria lakin ujue hiyo mianzi pia inachukua nafas ambayo ilitakiwa kutumiwa na samaki so ukiijaza sana unapunguza eneo la samaki kuishi, kwaiyo isizidi sana wala kupungua. Kuna research article moja nilisoma jamaa akawa anashauri 4 mianzi/m2 inaweza ku-replace kabisa supplimentary feeds.
 
Je niweke ikiwa mibichi au hata mikavu naweza kutumia?
 
Je niweke ikiwa mibichi au hata mikavu naweza kutumia?

Zozote mkuu hao jamaa {sessile organisms} wanachotaka ni hard substrate ili wajishikize na kuzaliana, nchini Israel wanatumia mabomba chakavu. Mbolea utaweka kama kawaida.
 
Wadau wa ufugaji samaki tunakabiliwa na changamoto nyingi . Binafsi naamini tunaweza kutatua baadhi ya changamoto sisi wenyewe bila kusubiri wazungu au wachina ikiwa tutaamua kwa dhati.

Malighafi zote tunazo tunachohitaji ni akili ya ubunifu tu na mtaji ambao naamini baadhi yetu wanavyo.

Mfano: Changamoto ya upatikanaji wa floating pellets inaweza kwisha tukibuni simple and cheap pelleting machine kwa kushirikiana na ndugu zetu wa SIDO kinachotakiwa ni sisi kuwapelekea SIDO wazo letu na details ya kitu tunachokitaka, hawa jamaa hawavumi lakini wamo wamebuni vitu vingi sana vyenye manufaa kwa wakulima eg. mashine ya kutengeneza mkaa kw kutumia vumbi ya mkaa, incubators, water pumps, mashine za kupukuchua mahindi/karanga/kukata viazi, kubangua korosho/kahawa, kuvuna mpunga n.k
 
Naitwa Abdul Lipoiye, napatikana Dar-es salaam Tanzania.

Nimesomea utaalam wa ufugaji wa samaki, uzalishaji wa samaki, utengenezaji wa chakula cha samaki, ujenzi wa mabwawa, utunzaji wa samaki na mabwawa, utengenezaji wa mashine ndogo za usaji nafaka na utengenezaji pelete kwa ajili ya wakulima wadogo waso na uwezo wa kununua mashine kubwa n.k.

Kwa sasa niko nyumbani na ninapenda kushirikiana na wale wote wanaopenda kufuga samaki na kuku wa aina za kiswahili na kizungu kiujumla. Email : manlipoiye@gmail.com. Phone number: 0658-530-884. Kwa msaada zaidi wasiliana nami jf, email na simu pia. have a nice day.
 
Bwana Mtema wa Noti, kiukweli mimi kama mtaalam wa kilimo cha samaki nakwambia ya kwamba hilo eneo halifai kwa sababu chanzo chake cha maji si chauhakika na pia hufurika maji kipindi cha mafuriko inamaana kipindi cha mafuriko utakula hasara bure kutokana na kubomoka kwa kuta za mabwawa na pia kupotea kwa samaki wako.

Kiukweli halifai kwa ufugaji samaki. 0658-530-884.
 
Wadau wa ufugaji samaki tunakabiliwa na changamoto nyingi . Binafsi naamini tunaweza kutatua baadhi ya changamoto sisi wenyewe bila kusubiri wazungu au wachina ikiwa tutaamua kwa dhati. Malighafi zote tunazo tunachohitaji ni akili ya ubunifu tu na mtaji ambao naamini baadhi yetu wanavyo. Mfano: Changamoto ya upatikanaji wa floating pellets inaweza kwisha tukibuni simple and cheap pelleting machine kwa kushirikiana na ndugu zetu wa SIDO kinachotakiwa ni sisi kuwapelekea SIDO wazo letu na details ya kitu tunachokitaka, hawa jamaa hawavumi lakini wamo wamebuni vitu vingi sana vyenye manufaa kwa wakulima eg. mashine ya kutengeneza mkaa kw kutumia vumbi ya mkaa, incubators, water pumps, mashine za kupukuchua mahindi/karanga/kukata viazi, kubangua korosho/kahawa, kuvuna mpunga n.k

mkuu uko sawa kabisa...sasa shida iko kwa hao jamaa wa SIDO wataielewa hiyo machine au ndio wewe itabidi uwafundishe...nikwambie kitu mimi ni mmoja wa wanaofikiria kufuga samaki hasa tilapia......mpango wangu ni kutumia plastick tank shida ipo kwenye wapi nitapata water pump nzuri ya kuingiza hewa kwenye maji, pili ni hiyo machine ya kutengeneza floating pelletes...niko dar uhakika wa maji na eneo dogo la kukaa fish tanks kama tano ninao...msaada kidogo au unanishauri
 
Back
Top Bottom