Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

nipm nikupe contact za afisa uvuvi mtaalam sana ye nimstaafu kwa sasa wengi anawafanyia hizo kazi but yupo Iringa town

mkuu nimeku pm. Je umepata? na shida sana na huyo bwana samaki.
 
Kuna sehemu ukilima msimu wa kwanza wakiona mazao unayopata hawakutaki tena, wanaanzisha zengwe wanasema huyu tajiri wa Dsm anatuletea fujo.

Hiyo ilinikuta sehemu. Kilosa/Mvomero pia wanamtindo huo, wanakupa bonge la pori/msitu bure, wanakwambia safisha na ulime. Sasa ukishasafisha lile pori vizuri wanazusha kasheshe kwamba lile eneo limeuzwa kimakosa kwa hiyo si halali wewe kulifanyia kazi. unaweza kumng`oa mtu nywere kwa mikono.
 
Hiyo ilinikuta sehemu. Kilosa/Mvomero pia wanamtindo huo, wanakupa bonge la pori/msitu bure, wanakwambia safisha na ulime. Sasa ukishasafisha lile pori vizuri wanazusha kasheshe kwamba lile eneo limeuzwa kimakosa kwa hiyo si halali wewe kulifanyia kazi. unaweza kumng`oa mtu nywere kwa mikono.

Pande za huko ndio zao sana tena wanaweza kukupa sehemu ingine yenye visiki uanze upya kukwatua.
 
Ninaangalia movie na nimevutiwa sana na ufugaji wa samaki kwenye eneo dogo sana.

Je kuna mdau yeyote Dar aliye na ujuzi na hii sector ningependa kuanza ufugaji wa samaki.
 
samaki wa sato na sangara wanafaa sana kwenye maji ya jinsi gani naikiwa nataka kufuga hapa dar es salaam nahitaji kuwa na eneo la ukubwa gani na maji ya ujazo gani bwawani ili niweze kufuga samaki aina ya sato na sangara?
 
Bwawa la samaki limapaswa kujengwa vp ili kuwa na Tij? ukubwa gani wa bwawa unatakiwa ili kuwa na biashara yenye kipato kizuri?
 
samaki wa sato na sangara wanafaa sana kwenye maji ya jinsi gani naikiwa nataka kufuga hapa dar es salaam nahitaji kuwa na eneo la ukubwa gani na maji ya ujazo gani bwawani ili niweze kufuga samaki aina ya sato na sangara?

Sato/perege na Sangara wanaweza kufugwa katika maji baridi (maji yasiyokuwa na chumvi kama vile ya mto, maziwa,kisima na dawasco. Ukubwa wa eneo inategemea malengo yako na uwezo wako:ufugaji kwa ajili ya kula bwawa linaweza kuwa 10m by 10m; ufugaji wa kibiashara bwawa ni vema likaanzia 20m by 20m na kuendelea mpaka 1ha;unaweza kufanya intensive farming katika eneo dogo la 20m kwa kuweka matanki mengi na kuweka samaki wengi lakini unahitahi mtaji wa kutosha kwa ajili ya maji, umeme na chakula.

Ujazo wa maji inategemea na ukubwa wa bwawa lako: kwa mfano bwawa la miti 20 kwa 20 lenye kina cha 1.5m utahitaji maji 1800cubic meter (1,800,000 litres)
 
Bwawa la samaki limapaswa kujengwa vp ili kuwa na Tij? ukubwa gani wa bwawa unatakiwa ili kuwa na biashara yenye kipato kizuri?

Ujenzi wa bwawa unaendana na hali ya udongo wa eneo lako: Eneo la udongo wa mfinyanzi bwawa ni la kuchimba tu na kujaza maji kwa ajili ya taratibu nyinginezo.

Eneo la mchanga bwawa litachimbwa, ili kuzuia upotevu wa maji litajengewa na matofali na kusakafiwa au kuwekwa nylon sheet. Kwa kawaida bwawa linakuwa na kina cha 0.8m-1.5m, ukubwa inategemea na uwezo (20x30m -1ha linafaa kibiashara).

Bwawa linakuwa na sehemu ya kutolea maji ambapo unaweka PVC pipe 4inch-10inch au kujenga mlango wa zege au mbao.
 
Mkuu hizo karatasi za kujengenea bwawa huwa zinapatikana wapi? na je zipo za ukubwa gani? Nataka kujenga bwawa karatu, ila Udongo nazani ni wa Mfinyazi ni ule mwekundu uno nata kama gundi wakati wa Mvua, vipi inhitajika nylon hapo?
 
1.Mkuu naomba uniambie ni species zipi zinazo kubali kwenye hali ya baridi sana ambazo nikifuga zinalipa,muda wa ukuaji na chakula?2.magonjwa ya samaki ni yapi?

Mkuu sehemu za baridi trout fish ni the best (anapatikana Tanzania, wengine kwetu hawapo). Samaki huyu anakuwa kwa kwa muda wa miezi 6 kufikia umri wa soko. Hata hivyo, unaweza kufuga tilapia ingawa ukuwaji wake utakuwa taratibu wakati wa kipindi cha baridi.

Hivyo, unaweza ukafanya timing tu. Trout hatuna vifaranga vyake hivyo utalazimika kutafuta mitoni au kuagiza mayai yake nje. Chakula: Kuna chakula cha asili cha samaki ambacho ni phytoplankton na zooplankton (hupatikana kwa kurutubisha bwawa kwa mbolea ya viwandani au ile ya ngombe, mbuzi, kuku nk; pia unaweza kutungeza chakula cha ziada kwa kutumia ingredients kama vile dagaa, pumba, maharagwe ya soya nk).

Magonjwa ya samaki ni species specific lakini kiujumla kuna yale yanayosababiswa na ukosefu wa lishe, deformities, na wadudu kama vile ya fungus, virus na bakteria (siyataji kwakuwa ni species specific).

Hata hivyo kwa Tanzania magonjwa sio tatizo kwakuwa vyanzo vya maji na mbegu bado ni salama.
 
Mkuu hizo karatasi za kujengenea bwawa huwa zinapatikana wapi? na je zipo za ukubwa gani? Nataka kujenga bwawa karatu, ila Udongo nazani ni wa Mfinyazi ni ule mwekundu uno nata kama gundi wakati wa Mvua, vipi inhitajika nylon hapo?

Mkuu hauhitaji nylon hapo, hapo mwendo mdundo tu. Lakini nakushauri kama kuna udongo mwekundu hakikisha unamuona afisa uvuvi wa karatu akacheki hilo eneo kwakuwa kuna udongo mwingine wa aina hiyo unakuwa na Iron ya kutosha ambayo inaweza ikachafuwa maji na kuua samaki.
 
Mkuu hebu anza na utangulizi, yaani hii biashara unaweza kuanza vipi, mahitaji, matarajio ya mapato yake na faida yake kiujumla!!
wengine tuna ardhi tungeweza anzisha biashara hiyo ila swali gani niulize, gharama? aina ya samaki? muda wa kukuza? madawa? aina ya udongo? soko la samaki?n.k
Hebu tuwekee hapa habari kamili kama ile ya ufugaji wa kuku iliyomo humu
Sp
 
Mkuu unaweza kuwa a simple business plan kwa mfano bwawa la 20x30M linaweza kugharimu kiasi gani kujenga (Makadirio tu) gharama ya kununua vifaranga,gharama ya kuvilisha hadi kufikia muda wa soko,inachukua muda gani hadi kuvuna na makadirio ya mapato kwa muda huo itatusaidia sana na wewe binafsi ni huduma gani unaweza kumsaidia mtu na gharama zako
 
Kuna ulazima wa kuweka umeme? je umeme unasaidia nini kwenye sehemu ya kufugia samaki?

Je naweza kufuga bila kuchimba bwawa ardhini? kwa maana ya kuwa na tanki la kawaida? hii itaathiri vp ukuaji wao?
 
Simtank moja kubwa la lita kama 10,000 wanaingia samaki wangapi?

Na hayo makasha kama matanki ya chini yanapatikana hapa kwetu?

Kwa ufugaji wa kawaida, idadi ya samaki kwa cubic meter ni 40. Hivyo kwa tanki kama hilo utaweka samaki 400.Kwa idadi hii utahitaji kufanya water exchange 15-20% kwa kila baada ya siku tatu. Ila kwa yale marefu ambayo utahitajika kukata nusu hivyo itakuwa samaki 200.

Ukitaka kufanya intensive farming katika tank hilo: samaki 120 kwa cubi meter, hivyo utaweka samaki 1200. Kwa idadi hii utahitajika kufanya water exchange kwa kila 1-2 hours na hewa ya ziada au maji yawe yanaingia na kutoka wakati wote bila-hewa ya ziada haitajika.

Yale matanki ulioliza hayapo hapa lakini unaweza kutengeneza. Karibu
 
Tunashukuru sana Mkuu ubarikiwe mimi swali langu ni kuhusu usafirishaji kama mabwawa yapo mbali na soko je ni njia gani salama ya kusafirisha bila samaki kuharibika? Au Lazima uwe na Refrigirated Trucks?
Kama ni umbali wa zaidi ya masaa 6 unahitaji hilo truck. Lakini chini ya hapo unaweza ukawahifadhi na barafu yenye maji kiasi (chilling). Lakini unaweza ukatumia chilling method kwa safari ya zaidi ya masaa 6 ikiwa utafanya timing ya kusafiri wakati hakuna jua. Wataalam wa quality assurance watatusaidia hapa

Mkuu Hewa ya Ziada inawekwaje kwenye bwawa?

Kuna vifaa vinaitwa aerators ( search paddle wheel aerators) ambavyo vinawekwa katika bwawa kulingana na ukubwa wa bwawa; kuna air compressor au liquid oxygen; kuna oxygen generators. Pia, unaweza ukawa na overhead tank ambalo litakuwa linaspread maji katika bwawa wakati wa usiku. Karibu
 
Back
Top Bottom