Ufyatu 100%: Sababu zinazotolewa hazina mantiki au mantiki hazina sababu?


Hoja yako inayohusisha Utawala uliopita na wa sasa ni nje ya mada kabisa.

Nami naungana na aliyekupinga kwa hoja kwamba utawala wa sasa haupaswi kurudia makosa ya uliopita, kufanya hivyo ni dalili za udhaifu. Wahenga walinena Kufanya kosa siyo kosa, kosa ni kurudia kosa.

Hivyo basi, wasiopenda mkataba wa IGA, kama mimi, tunauambia utawala wa sasa, KWA SAUTI KUBWA, watakosea sana kuipa DPW kuendesha bandari kwa mgongo wa nchi yake tofauti na makampuni ya nje yanayowekeza nchini kibiashara. Na ukiusoma huo mkataba (IGA), unaoiteua DPW, kwa umakini, unaipa mamlaka na madaraka makubwa.

Mkataba wa IGA utupiliwe mbali na DPW iwekeze bandari kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo za uwekezaji
 
Umeandika utumbo gani huu Mzee, mbona siku hizi umekuwa na akili kama za Kingwendu tu.
 
Kwanza hujui unaongea nini. Sisi hatuogei uwezo wa DP. Sisi tunaongea mkataba tu ambao hata mtoto wa form four hawezi kusign pia mazingira.
 
Nikwambie kitu..sikupingi kabisa mtazamo wako huu... unaweza kuwa uko sahihi ..
Na nimependa ulipoeleza kuwa Wasisaini mkataba wa Dpworld Kwa sababu ulizo zieleza....
Umeongea with integrity hata kama tunaweza "tusikubaliane"..

Niko more concern na wale wanaopinga Dpworld Kwa sababu Tu ni waarabu...wao hawataki hata kusema kipengele kipi libadilishwe kipi kitolewe wao mradi ni waarabu basi wapigwe chini...kwangu hao ndo watu wanao tumia dini kushambulia serikali.... especially walipokuwa kimyaa kabisa wakati Magufuli anafanya lolote Kwa utashi wake...
Otherwise you could be right..
 

Rais anadelegate authority kwa mawaziri na mwanasheria mkuu.
Rais anaweza pia kudelegate resposinsobility.

Lkn analaumiwa kwa kuwa yeye ndie accountable.

Lkn nduguzetu wanaomnywea mbege rais ili wapige mayote wakimkosoa rais kama yeye ndie responsible personnel aliyesaini mkataba.

Kumbe waliosaini ni walewale catholic supremacy wa nchi hii.

Hawaguswi.

Na wanywa mbege ni kama wamepatwa na ugonjwa wa Stockholm.

Stockholm syndrome
 
Ungepambana na hoja yake,sio personal attack
 
Kosa la kwanza halihalalishi kosa la pili... ni ujinga uliotukuka kuamini katika kuendeleza makosa... Magufuli hayupo tuletee angalau mkataba mmoja kati uliyotaja tuuchambue tuuone kama unaujinga kiwango cha huu wa bibi yako.
 
Chuki zako za kidini zinaharibu hoja yako, sio wote walio wakristo wanaupinga huo 'mkataba wenu' na vice versa pia.


jifunze kuvumilia imani za wengine na jenga hoja bila chuki, Tz ni secular state.
 
Nyie mmeshindwa kufanya kazi ya kuiendesha bandari kwa ufanisi
Sana sana mmekalia uwizi tu hapo na uvivu
Mwacheni dp world aiendeshe huko mbeleni mtaaona
Hiyo mwendokasi tu mradi unaenda kimkandamkanda tu

Ova
 
Kuna wafanyakazi bandari pale wanakuambia wao hawaugusi mshahara wanaishi kwa pesa za dili pale.
Mfanyakazi bandari akiienda kula lunch anarudi saa nane alafu saa kumi anaondoka sasa dpworld unafikiri atakubali upuz huo [emoji1]

Ova
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sijui unatumia kiungo gani kufikiri kwa sasa[emoji134][emoji134][emoji134]
 
Hata mimi siungani na wanaopinga uwekezaji wa DPW kwa sababu ni Waarabu au waliousaini ni wa Tanzania visiwani. Ila mazingira ya uandaaji wa huo mkataba na nguvu inayotumika vinasababisha wajadiliaji hoja ya kuupinga wanahusisha udini na upande wa Muungano.

Nami naendelea kuuliza (kwa wino mwekundu) bila kujibiwa kuna nini nyuma ya mkataba wa IGA tofauti na mikataba mingine ya uwekezaji kibiashara?

Kama Mkuu The Boss una jibu nipe niondoe hisia na dhana potofu ya Wachingiaji wengi kuwa bandari inauzwa na wasio WaTanganyika.
 
Wewe ulimkosoa kwenye Korosho ulifanikiwa nini zaidi ya kuugulia maumivu mpaka leo. Zaidi unapalilia Udini wako tu.
 
Samia ni smart prezoo,apoteze muda kuwajibu mazezeta ili Hali ana Mambo mengi ya kuifanya ili iweje??

Kukaa kimya ni jibu Kwa mjinga
Mambo mengi ya kuuza Raslimali za Tanganyika kwa Waarabu. Uzeni na korosho
 
Kuna uzi Pascal Mayalla kafafanua kabisa kuwa IGA ni Sawa na MoU... memorandum of understanding tu.. makubaliano ya kidiplomasia zaidi ambayo hayana nguvu yeyote ya kisheria Hadi mtakapoingia mkataba halisi....

Umeuliza why hii inapingwa zaidi?
Hujui kuna watu wataathirika na biashara? Karamagi na Ticts?hakawalipa watu "wampambanie"?
Unaamini ni uzalendo wake Tibaijuka anaenda Hadi kwenye TV kupinga Dpworld? Huyu Tibaijuka aliepewa mgao escrow?? Hajapewa mgao na Karamagi??..

Huoni kuna kundi linatumia nguvu kupinga Dpworld Kwa sababu ambazo haziko clear??
 
1. Kwa kuwa Magufuli alikuwa anafanya makosa haya kibabe na Samia aachwe ayafanye tu sio? Atangaze tu kuwa, naye anakwenda kimagufuli - gufuli ili akabiliwe Kwa style ya kimagufuli pia..

2. Lakini, Ukiachilia mbali hilo, nionavyo mimi, hoja kwa kiasi kikubwa hata sio kampuni hiyo ya DP World imepatikanaje. Hizo hoja zinakuja na kuingia ktk mjadala huu kama "by the way". Kikubwa na kinacholeta ugomvi ni "intent" na "contents" za mkataba kuwa haufai na ni mbaya kiasi cha watu kuanza kuikumbuka Tanganyika yao na wengine kuingiza udini ndani yake...!

Mzee Mwanakijiji Yuko sahihi kukumbusha watu kuhoji mambo ya msingi. Hata hivyo, akumbuke tu kuwa hata hayo anayoona si hoja, lakini kwa namna jambo hili lilivyokaa, ni lazima tu yajitokeze na kuhojiwa. Mathalani issue ya muungano imeguswa na mkataba huu. Katiba ya JMT imeguswa na mkataba huu..

Huwezi kujaribu kushughulikia mambo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kimakosa Kwa kukiuka principles zake Kisha usiamshe hoja ya u - Zanzibari na Zanzibar na u - Tanganyika na Tanganyika..!
 
Kama Magufuli alikuwa anakiuka taratibu za manunuzi basi tumfuate? Hapana, hata kama rais yuko well informed hawezi kufanya kila kitu yeye.

Kama hivyo basi rais awe sehemu ya majaji wa mahakama awe anatoa hukumu kwa vile atakuwa weli informed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…