Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

Nilidhani uzi huu watakuja critical thinkers na kuanza kuchambua matukio ya hivi karibuni ili tuone lipi linafaa kuwekwa kwenye ugaidi na lipi halifai.

Mpaka sasa sijaona isipokuwa post mbili tatu zimeanza lakini hazikumalizia.

Hivi matukio yepi ya hivi karibuni tunaweza kuyahusisha na ugaidi?
Hali imezidi kuwa tata....ugaidi tupo nao, ingawa ni kwa kiwango cha chini...lkn kuna tatizo jingine.
Wanasiasa kuanza kutumia matukio kama "nyenzo" za kisiasa zaidi, na wakti mwingine ktk tafsiri tofauti, na hivyo kuinajis dhana nzima, na harakati za umma kukabili ugaidi... wanasiasa wanatugawa ktk umoja wetu stahiki kuzungumzia tishio..
 
Kitu pekee kinachohitajika ili uovu uenee ni watu wema kutofanya chochote...

"The only thing necessary for the triumph of evil is for good men to do nothing"
Mbona sijaona "watu wema" wakifanya chochote kuhusu mauaji ya wana CCM wa Kusini?
 
Hata uvamizi wa Mawingu Media ni tukio la ugaidi,na kwa kuwa Kiongozi wa uvamizi alionekana dhahiri then Gaidi Mkuu anajulikana
Wacha kupinda pinda

Mkuu wa Mkoa siyo mara yake ya kwanza kwenda studio zile. Huwezi kuuita ule ugaidi labda useme marafiki wana uhasimu wao.

Tuwe wa kweli na tufikiri kwa kina, kama ule ni ugaidi vipi kuhusu wana CCM wanaouliwa Kusini?
 
Wewe ndo hujui, huo si ugaidi. Ugaidi una lengo la kushinikiza serikali/taasisi flani kufanya au kuwapa wanachohitaji. Sasa hawa wa tz wanahitaji nini maana hawajajitokeza.

Wewe hujaelewa wanachohitaji? Kwani Ben saa nane, Nape, Dr. Ulimboka, Absalum Kibanda na Roma walifanya kosa gani? Rejea kwenye faili zako
 
Mkuu wa Mkoa siyo mara yake ya kwanza kwenda studio zile. Huwezi kuuita ule ugaidi labda useme marafiki wana uhasimu wao.

Tuwe wa kweli na tufikiri kwa kina, kama ule ni ugaidi vipi kuhusu wana CCM wanaouliwa Kusini?

Acha kumsafisha rc kwani yeye amekufa? Kwanini unajibu kwa hisia, una hakika kama unayosema ndiyo lengo lake? Mbona asijibu yeye hadharani kama ikiwa hilo ndo lengo lake? Kimsingi maadili ya nchi hayapo tena, mbaya zaidi watu mnashabikia na kuutetea huo uchafu unaoendelea nchini.
 
Kukaa kimya ni kukubaliana na tendo husika hivyo kelele zinasaidia,hata MKATOLIKI amepatikana kwa sababu ya kelele
 
Bibie nimeshindwa kukuelewa kabisa yaani watu wanauwawa,wanateswa,wanapotezwa halafu unataka tunyamaze?hapana lazima tuongee sana.
 
"Kutekwa" huwa ni vitani, hao waliotekwa walikuwa vitani?

Au unatekwa kwa watu kutaka "ransom", hao unaosema waliotekwa kuna "ransom" iliyokuwa "demanded"?

Hao unaosema walitekwa hao wala hawaingii katika kigezo cha ugaidi. Ugaidi ni kama matukio ya Kusini, ugaidi ni kama kutumia hao waliotekwa kusambaza habari za kutisha watu.

Tukio la Roma, hili baada ya kumsikiliza Ally leo nimeona kumbe ni mtu anaemtukana Rais, unamtukana Rais unategemea vijana wanaompenda wakuachie tu? Wacha Rais hebu mtu akutukane wewe tu mbele ya marafiki zako tuone kama utamuachia au marafiki zako watamuachia bila ya kumuadabisha.

Huo siyo ugaidi.
Kumbe wale wanaochukuliwa na kutakiwa kuongea ama kufanya yale watesi wao watakayo kumbe huwa si mateka!!! ( maana mateka si lazima vitani bali mtu yeyote atwaliwaye bila ridhaa yake) Kwa mujibu wa Ally hana hakika kama ni ROMA ama nani? Ikiwa Rais katukanwa mbona hatuoneshwi ushahidi? Au... au... au.....???
 
Kumbe wale wanaochukuliwa na kutakiwa kuongea ama kufanya yale watesi wao watakayo kumbe huwa si mateka!!! ( maana mateka si lazima vitani bali mtu yeyote atwaliwaye bila ridhaa yake) Kwa mujibu wa Ally hana hakika kama ni ROMA ama nani? Ikiwa Rais katukanwa mbona hatuoneshwi ushahidi? Au... au... au.....???


Kama Roma?

Kama jibu ni ndiyo, huyo msikilize Ally Kessy, kesi yake imekwisha.

Huyo kesi yake bado haina vigezo vya kuingia kwenye ugaidi
 
Ilishazoeleka kwa Tanzania likitokea tendo la kugaidi basi waliofanya uovu huo ni waislam

Ndio maana hadi leo jamii ya kiislam inanyanyasika kwa kufunguliwa kesi za kigaidi ambazo hazina ushahidi. MF kule Arusha kulitokea shambulizi la kigaidi ktk mkutano ambapo kiongizi wa Vatican alikuwepo. Na ktk tukio lile alionekana kijana aliyesadikiwa kufanya tukio akikimbia aliwa amevaa kanzu. Ili tu ionekane aliyefanya Yale ni muislam. Lkn alipokamatwa ilifahhamika anaitwa joseph na kesi yake hatujui iliishia wapi.
Aina hii ya ugaidi inaitwa false flag terror, aina hii ya ugaidi INA historia yake tokea wakati wa Hitrer. Hitler alipotaka kuwauwa wayahudi alitumia false flag terror. Baada ya usiri mkubwa juu ya nani yuko nyuma ya ugaidi huu sasa Ukweli utadhihiri.

Hawa watu wasiofahamika wanaofanya ugaidi ukekaji na utesaji je hawahahamiki

Nukuu ZITTO nipo tayari kutoa ushahidi
 
FaizaFoxy-Huyu naye aliyeua Askari wetu saba kwa mkupuo naye ni gaidi?Ni kwa sababu ni Tanzania tu.Nilikuwa naangalia magazeti ya leo.Karibu yote ni siasa tu.Gazeti moja au mawili ysmeandika tena si kwa uzito.Shooting ya polisi Saba at a time ni habari kubwa kwa wanaotambua umuhimu wa Askari.Kuna vurugu mkoani pwani vyombo vya habari viko bize na siasa na habari za Simba na Yanga..
 
Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni ugaidi (terrorism).

Lengo la ugaidi ni kuwatia watu hofu na kufikisha ujumbe kwa wengi kwa njia ya hofu.

Matukio yanayoongelewa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao yote ya kijamii mpaka nchi za nje kwa sasa ni hayo, kuanzia watu kutekwa, kutolewa bastola hadharani, mauaji ya Kusini huko, watu kukutwa kwenye viroba, kupotea kwa watu na mengi mengineyo, yote yanaashiria ugaidi.

Magaidi hujitokeza na kusema sisi ndiyo tuliyoyafanya hayo ili waogopwe au matakwa yao yatimizwe au hukaa kimya na kuwachochea kivingine kwa lengo hilo hilo.

Matukio ya ugaidi yanapotokea pia hujitokeza wengine ambao hutumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wao kwa njia tofauti.

Kwa yanayotokea Tanzania, ukweli ni kuwa, kuna wanaofanya huo ugaidi wa kutisha na kuna wanaotumia huo gaidi kama ni fursa kwao kufikisha ujumbe wao ama kwa kuongezea ugaidi mwingine au kwa kuendeleza hofu kwenye jamii na vyombo husika.

Watanzania tunachotakiwa kufanya ni kukaa kimya na kufunga hii mijadala yote na kuwacha kuripoti matukio yote ya kigaidi ili kushindana na ugaidi.

Gaidi kama matukio yake hayaongelewi kazi yake inakuwa haijafanikiwa.

Au leta mawazo yako ni njia gani zitumike kutatuwa hili tatizo "linalotukabili".

Kwa muono wangu, kila tunapoyaongea na kuyasambaza ndiyo furaha ya magaidi na ndiyo lengo lao, wengi wajawe na hofu.

Kwanini? Mie sijuwi.
Mkuu wacha urongo na chokochoko,ushaambiwa kelele zenu abiria hazina maana,wacha roli lisonge
 
Wewe ndo hujui, huo si ugaidi. Ugaidi una lengo la kushinikiza serikali/taasisi flani kufanya au kuwapa wanachohitaji. Sasa hawa wa tz wanahitaji nini maana hawajajitokeza.
Hiyo ndio definition ya ugaispd toka kwa jamiifirum member!!!! Kweli elimu ni muhimu sana ,acha kukalili mkuu uwe pia unajifunza.
 
Hata aliyemtolea Nape bastola ni gaidi?
Walioenda kuvamia Clouds pia ni magaidi wa alshabab au islamic state? basi kama ni hivyo basi serikali yetu inashirikiana na magaidi.
 
Huu ugaidi ndio umeshaingia tayari.Tahadhari ni muhimu.
Kama Clouds media ilivamiwa kigaidi,na wahusika hawajachukuliwa hatua!Unatarajia Huu ugaidi upo rooted wapi!
Kama saa hizi Kagame ni rafiki yetu mkuu,unatarajia nini hapa.
Twafaa
 
Gaidi hajawahi komeshwa kwa kukaa kimya,lazma mapambano yawepo,gaidi ni mnyama na adui mwenye roho mbaya....anakuua ndani ya dakika 1,nae ni kupambana nae
 
Back
Top Bottom