Ugaidi Tanzania Unafanikiwa

Duh yaan watu watekwe wauwawe tukae kimya kweli hapana ata shetani atashangaa

Mimi kinachonishangaza ni pale wabunge wetu wanapojadili majanga ya watu kutekwa, kuuawa na wengine kuteswa huko bungeni; serikali wa kupitia kwa Naibu spika inatoa kauli kuwa bungeni sio mahala pa kupeleka malalamiko , wabunge wenye malalamiko juu ya uhalifu huo wapeleke malalamiko yao polisi!!!!! Hapo ndipo ninapojiuliza huu uongozi ni wa kuwalinda watu na usalama wao au ni wa kuwalinda watawala peke yao? Inaelekea huyu naibu spika haguswi kabisa na matatizo haya na pengine anajua kinachoendelea na ndio maana anapuuza!
 
Link Kwanini tukatae kuwa mauaji ya polisi huko Mkuranga sio ugaidi?
 
Gaidi hawezi fanya kitu bila demand na time frame.

Gaidi lazima aseme nataka nifanyiwe hivyi ndani ya muda fulani bila hivyo nitafanya hivi zaidi.

Gaidi gani anaua kimya kimya bila hitaji lolote? Huyo siyo gaidi ni kibaka mamboleo
 
Naibu spika ni rafiki ya watekaji pia majambazi hataki wabunge wajadili uovu wao.
 
Blog za mapishi,nenda ukalale kibibi! Can't differentiate BTW Islam and terrorism... J,Bush

Qur'an 28:55. Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga.
 
Nadhani serekali/polisi inatakiwa kuwa karibu na raia. Kuwa karibu na raia, ni pamoja na kutatua matatizo yanapotokea, kama vile, mauwaji au kutekwa kwa raia nk. Kwahivi sasa, naona hakuna TRUST Kati ya raia na vyombo vya salaama. Raia wana ogopa vyombo vya usalaama na vyombo vya usalaama sidhani kama wanaona hili ni tatizo. Kuaminiana Kati ya raia na vyombo vya usalaama, utasaidia saana kupunguza au kutokomeza ujambazi/ugaidi unao nyemelea nchi yetu.
 
Kuna ugaidi wa aina mbili; na ni kweli, moja ya ugaaidi huo hauleti tija kuutangaza kwa sababu wanaofanya aina hiyo ya ugaidi wanafanya kwa lengo la kutaka kutangazwa! Hivyo basi, unapotangaza, mission inakuwa accomplished!

Kwa mfano, ni kawaida sana kuona ISIS wanakata watu vichwa na kujirekodi kisha ku-release videos husika! Hawa wanafanya hivyo kwa lengo la kutaka publicity na kusambaza propaganda zao! Hawa ukiwaongesha kwenye TV inakuwa umewasaidia kufanikisha malengo yao... kueneza propaganda na hofu!!

Haya yanayotokea Tanzania sioni kama yana ufanano na aina ya ugaidi niliousema hapo juu!!! Hawa ni magaidi waoga na hakuna hata mmoja miongoni mwao mwenye hamu ya kufahamika japo na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa let alone askari polisi! Hawa hawafanyi wafanyayo kwa lengo la kutafuta publicity... inawezekana lengo lao ni kujenga hofu!!!

Kwavile hawana ujasiri wa kutaka wafahamike; kutangaza kwamba hao ni majambazi kunawapa ahueni kwa sababu bado wangependa kutenda uhalifu wao bila kufahamika! Hawa kuwatangaza wazi wazi kwamba ni magaidi kunawajengea hofu kuliko ujasiri kwa sababu wanafahamu Watanzania wanaweza kuvumilia kuishi na jambazi mtaa mmoja kuliko na gaidi anayeishi mtaa wa 7 !!!
 
Sijuwi=sijui
 
Huwezi kutatua tatizo kwa kupretend hamna tatizo.kunakitu kinaitwa "solving problem technique"unakifahamu?
 
Itakuwa walishakaa kimya mno mpaka imefikia hatua hii ni mambo yanajisema yenyewe. Kwanza bado serikali ipo kimya kwa kusema sio ugaid ni majambazi. Hakuna chombo cha serikali kilichoreport ni ugaidi.
 

Kwanza nianze kwa kusema umeandika upumbavu mtupu.

Pili kinachotokea Tanzania si "ugaidi" bali kuna kila dalili serikali ndiyo inayofanya mambo hayo kupitia usalama wa taifa halafu unataka watu wakae kimya huku maisha yao yako hatarini.
 

Sheria ifuatwe basi lakini kuchukua sheria mikononi mwako nnje ya mahakama ni kosa.
 
Ni mjadala ambao inabidi kwanza tujue sababu.

Kuna ugaidi wa kugeuza mtazamo, pia hatujauzungumzia.
Mwalimu unakuja na subtopic, theni unataka wanafunzi waje na full topic well done ss, ilitakiwa uelezee kiunagaubaga ili ueleweke sasa hapa unakiri udhaifu wako. Si ungekuja na mada complete kuhusu huo ugaidi wa kugeuza mtizamo.

HAKIKA TUKIKAA KIMYA MAWE YATASEMA. Wacha watu tufungukeee [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…