Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Ingekuwa ni hivyo basi Wakenya wote wangekuwa wameshatangulia mbele ya haki,Kenya ni mwendo wa dona tu,haya makapi (unga mweupe/uliokobolewa)yanaliwa TZ
 
Sasa itabidi Watanzania wote wahamie USA ili waweze kula FDA approved dona, which is a good thing if you really think about it.
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Peleka uongo kule babu zetu walikula dona na hawakuwa na cancer
 
Sasa mbona hauhaelezea vzuri?.
Inamaanisha mahindi yote ya dona yana hiyo sumu ya aflatoxin? Na pia hii ishu ya sumu kwenye kiini imegunduliwa recently au toka zamani ipo.?
Kama toka zamani basi pita hivi.
Dadavua.
 
Dr.ndodi anasema panya wana akili kuriko binadamu,wao panya wakula kiini chenye protein wakati binadamu wao watoa kiini..sasa wewe tena unakuja unasema dona ni sumu..sayansi ipo kutishana tuu nakumbuka kuna mtaalam mmoja wa mambo ya hewa alikua anatembea na mtungi wake kajifunga mirija na mask usoni akidai binadamu wengi wanavuta hewa yenye bacteria wengi wasioonekana kwa macho..ipo siku katika tafiti zenu mtakuja kusema kufanya mazoezi kuna madhara sana..
Kuna mazoezi ambayo hayatajiwi kwa aina fulani ya watu hasa watu wenye umri kuanzia 35 na kuendelea.
 
WADAU TUJIFUNZE KUSOMA NA KUPANUA WELEDI WETU KATIKA KUCHANGANUA BAADHI YA MAMBO, SIYO KUKURUPUKA TU NA MADA KAMA ZA NAMNA HII:

KUHUSU Aflatoxin (Nimecopy na kupaste toka Wikipedia), someni kwa faida ya hii thread.

Aflatoxins are poisonous and cancer-causing chemicals that are produced by certain molds (Aspergillus flavus and Aspergillus parasiticus) which grow in soil, decaying vegetation, hay, and grains. They are regularly found in improperly stored staple commodities such as cassava, chili peppers, corn, cotton seed, millet, peanuts, rice, sorghum, sunflower seeds, tree nuts, wheat, and a variety of spices. When contaminated food is processed, aflatoxins enter the general food supply where they have been found in both pet and human foods, as well as in feedstocks for agricultural animals. Animals fed contaminated food can pass aflatoxin transformation products into eggs, milk products, and meat.

SASA TAHADHARI YA UNGA WA DONA INATOKA WAPI? ilitakiwa uelezee hiyo toxicity inafikaje kwenye unga (siyo dona pekee) na njia za kufanya kujikinga kwa faida ya wana jamvi siyo kupost tu. Kama hujui kitu ni bora kuuliza kuliko kujifanya mjuaji.....
kwa hyo wewe reference yako kubwa ni Wikipedia...sons vizuri michngo ya watu na kunareference nzuri zimetolewa...changanya na Wikipedia yako...usipoelewa basi wewe utakua ni jipu....itabidi Kigwangala aje akufanyie ziara ya kushitukiza
 
Hii taarifa itapokewa kwa mtazamo tofauti na wadau wa dona vs sembe

IMG_20160211_WA0021.jpg

IMG_20160211_WA0022.jpg

IMG_20160301_WA0003.jpg

Daah!...kama na dona sumu basi hakuna chakula tena

Ila hata kama kuna huyo "aflatoxin" kwenye dona bado virutubisho vya dona vinaweza kua ni vingi kuliko hiyo sumu

Na kabla ya kusonga ugali ule uji hua unachemka kwa centigrade nyingi sana hiyo sumu bado inabaki salama?
 
Ingekua kuna sumu zamani hyo wangekufa sana. Tulia we naona unataka kupiga dau watu wakoboe upate pumba.
 
Hebu weka chanzo cha habari yako tafadhali.
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Babu yako kala dona, bibi yako kala dona, shangazi zako na wajomba zako wamekula na kukulia dona. Hiyo sumu haikuwaona. Au inabagua? Acha hizo. Kama hutaki kula dona kaa pembeni sisi twala. Unaogopa aflatoxin mbona kila siku unaosha kirungu huogopi ngoma?
 
Kabla sijakuuliza maswali Mengi...
Kwanza Hongera kwa POST NZURI...
Pili..hiyo sumu unajua inakaa muda gani kwenye mahindi?
Tatu Kwani ni mahindi yooote yanawekewa hiyo Dawa,all sources?
Nne yaani hiyo dawa inakaa kwenye Kiini tuuuuu?
Tano Je ni madawa yote kwa mimea ni hatari? mbona binadamu tunatumia "Superflaxon"
Sita...ni Kiwango gani ndo kinadhuru?
Ahsante Mkuu

Aflatoxin ni chemikali/sumu inayozalishwa Na vimelea vya aina ya fungus ambaye huota Na kustawi kwenye mbegu baada ya kuvuna halafu zisikaushwe kitaalamu. Hii sumu ndio moja ya vyanzo vya saratani. Haina maana ukila chakula au kinywaji chenye hii sumu ni lazima uugue. Kwa hiyo sio dawa ya kuweka Bali hutokea kwa sababu ya mchakato usiozingatia utaalamu ambavyo ndivyo tufanyavyo kwa mbegu zote huku kwetu!
 
Mkuu, unahoja nzuri sana. Hakika unga wa DONA una virutubisho vinavyohitajika mwilini. Japo la muhimu ni kuosha mahindi vizuri kabla ya kusagwa ikiwa yamewekwa dawa ya kuhifadhia.

Ukweli ni kwamba Unga wa SEMBE ni makabi tuuu.
 
visivo na sumu vimebaki viwili tu: k na O 2!
 
Wakuu alichosema huyu jamaa mleta mada sio kigeni kwangu maana niliwahi kusikia kitu kama hicho. Nilisikia kwamba ugali wa dona la mahindi linatengeza sumu ikiwa utakuwa unakula kila siku pamoja ya kwamba unga wa dona una virutubisho vya kutosha. Pamoja na hayo, unga wa sembe ni hatari zaidi.
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
ngoja ni google nirudi...........
 
Back
Top Bottom