Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Bawasiri sio lazima ufanyie operation kuna ndugu yangu ilimsumbua sana lakini alipopata tiba ya asili hadi sasa ana mwaka wa nne haijamrudia tena zipo dawa za asili bila operation.
 
Bawasiri sio lazima ufanyie operation kuna ndugu yangu ilimsumbua sana lakini alipopata tiba ya asili hadi sasa ana mwaka wa nne haijamrudia tena zipo dawa za asili bila operation.
Ni dawa gani alitumia mkuu?
 
Mkuu je kwa bawasiri ya ndani inayotoka wakati wa kujisaidia na kurudi yenyewe baadaye (daraja la pili), mafuta hayo yaweza saidia pia?
 
Ngoja nami nitest hii kitu. Shukran mkuu kwa somo
 
dawa yake ni ipi, je mtu akifanyiwa upasuaji inachukua siku ngapi kupona?
hii kitu ni kweli inatesa sana, Dawa nilizoshuhudia watu wa karibu wametumia na kupona ni mbili, lakini naamini kuna dawa nyingi za kuponesha huo ugonjwa.

Dawa hizo ni :
* Mafuta ya nazi kama ni kinyama kilichoota kwa nje na huwa kinauma sana. (paka kila siku asubuhi na jioni)

* Mafuta ya Nyonyo (castor oil) haya nayo paka asubuhi na jioni. utapona kabisa.

Note: mimi sio daktari nimeshauri tu kwa kuona watu wa karibu yangu wakipona.

Ahsante.
 
Habari wakuu,

Nimekuwa nikinywa sana maji, kula mboga za majani na matunda. Naomba kama mtu ambaye alishawahi kuumwa bawasiri/hemorrhoids na akapona kabisa, anijuze alifanya nini akapona.

Ahsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
tumia utomvu wa ndizi kupakaza eneo lenye tatizo siku 5-7 utakua umemaliza tatizo
 
Samahani, je kwa bawasiri ya ndani, dawa yake ni ipi mkuu?
 
Habari za asubuhi wakuu humu ndani. Samahani naomba msaada kwa mtu yeyote anayejua tiba asili inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la bawasiri/ uvimbe / maumivu sehemu ya haja kubwa anifahamishe kabla mambo hayajaharibika zaidi..
 
Habari naomba uni PM namba za huyo mtu mwenye dawa please
 
nilitumia utomvu wa mgomba kwa kupakaa ndani ya siku tano bawasiri kwisha kabisa
 
Wahanga tumieni dawa inaitwa CONSTRELAX na NOVEL DEPILE CAPSULES. Ni virutubisho na vinatibu.
 
Ni muda sasa hili tatizo linanisumbua ,ilianza kama kinyesi kinakua cha pingilipingili kigumu.kikiwa kimechanganyikana na damu,wakati wa kunya ni shida,maumivu makali sana,,wakati mwingine muwasho ile mbaya nikaenda hospital nikapewa dawa tatizo likapotea.pia kuna dawa za kienyeji nilikua natumia .
Hali imejirudia,niliweka kioo kuangalia nikaona nyuma ya mfereji wa tundu la mkundu kuna kanyama kameota,kana fanana na ngozi tu ya kawaida,nisipo kunya nikakaa kama siku mbili pale panaacha kuuma,nikinya baada ya nusu saa maumivu yanaanza kwa ndani ,na pembeni pamevimba kama jipu ,na zaidi ya wiki sasa,nifanyaje ndugu zangu?,namawazo sana,je ntapona kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…