Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Usidharau hiyo hali, muone daktari si kwa kukutisha lakini inaweza kuwa dalili za saratani ya utumbo mkubwa.

Kula matunda na kunywa maji litre mbili au zaidi kwa siku.

Kula chakula chenye fibre kama makande, mharage, mchicha kisamvu wali wa brown au mkate huo wa brown.
Kwa maelezo yake jamaa anaumwa bawasiri!!

Aende hospital tu wakamfanyie upasuaji
 
Ni muda sasa hili tatizo linanisumbua ,ilianza kama kinyesi kinakua cha pingilipingili kigumu.kikiwa kimechanganyikana na damu,wakati wa kunya ni shida,maumivu makali sana,,wakati mwingine muwasho ile mbaya nikaenda hospital nikapewa dawa tatizo likapotea.pia kuna dawa za kienyeji nilikua natumia .
Hali imejirudia,niliweka kioo kuangalia nikaona nyuma ya mfereji wa tundu la mkundu kuna kanyama kameota,kana fanana na ngozi tu ya kawaida,nisipo kunya nikakaa kama siku mbili pale panaacha kuuma,nikinya baada ya nusu saa maumivu yanaanza kwa ndani ,na pembeni pamevimba kama jipu ,na zaidi ya wiki sasa,nifanyaje ndugu zangu?,namawazo sana,je ntapona kweli?
Mkuu huo ugonjwa unaitwa bawasiri wahi kupata matibabu usije poteza na nguvu za kiume bure
 
Bawasiri hiyo... Usikae sana chooni haswa vyoo vya kukaa... anza kula vyakula vya maji maji au ukila unywe maji mengi ili upate choo laini... kiuvimbe kitapungua au kuisha kabisa... Maumivu yakizidi muone daktari
 
Ni dalili ya haemorrhoids. Nashauri acha aibu, nenda hosp ukafanyiwe uchunguzi. Waweza kuandikiwa Anusol, dawa za kuchomeka kwenye anus.

Nenda hosp, aibu haitibu.
 
Salaam!! Waungwana nisaidieni kujua tiba ya bawasili.
Matibabu ya mwanzo ya maradhi madogo hadi yale ya kawaida huwa na ongezeko la kula
chakula kilicho na faiba, vinywaji ili kudumisha
haidresheni , dawa za kutibu inflamesheni husaidia kwa maumivu, na mapumziko. Baadhi ya taratibu ndogo zinaweza kutekelezwa ikiwa dalili ni kali au hazistawi kwa mwelekeo wa kudhibiti usiobadilika. Upasuaji hutengewa wanaokosa kuonyesha mabadiliko. Hadi nusu ya idadi ya watu wanaweza kuwa na matatizo na hemoroidi kwa wakati fulani maishani mwao. Matokeo kwa kawaida huwa mema.
 
Sio mtaalamu wa afya but kwa maelezo yake hiyo haikosi kuwa hemorrhoids/anal fissures/anal pilles a.k.a bawasiri, hii husababishwa na constipation,kukaa muda mrefu ktk surface ngumu, anual sex,baadhi ya bacteria nk, ila inatibika kwa namna mbalimbali kutegemea na aina make IPO external and internal haemorrhoids, kwa hiyo jaribu kwenda hospital kubwa kidogo ili wakushauri na aina ya tiba utakayoanza nayo kulingana na hali.......mm mwenyewe nilkuwa mhanga mkubwa but now Mungu mkubwa nimepona
 
Mkuu umeponaje? Msaada tafadhali
 
Du! Pole Sana, mimi kuna dawa za kizungu na za kisuni, ngoja waje
Ndio, nina ile ya ndani inayotoka wakati wa kujisaidia. Haiumi lakini ina miaka kibao. Mwanzo sikujua kama ni ugonjwa hadi nilivyosoma humu jf juzikati tu.
 
Back
Top Bottom