Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

 
 
DALILI ZA BAWASIRI NA TIBA YAKE
🔴Bawasiri hutokea pale mishipa ya damu inapovimba au kuathiriwa kutokana na mgandamizo unaotokea katika sehemu ya chini ya puru.
Kuna aina mbili ambazo ni :

•Bawasiri ya nje ; Hii hutokea ndani ya ngozi lakini katika sehemu ya nje ya tundu la haja kubwa (Anus)

Bawasiri ya ndani : Hii hutokea katika kuta za njia ya haja kubwa kwa ndani.
••Nini husababisha Bawasiri ?

Tatizo hili hutokea pale kunapokua na mgandamizo mkubwa katika mishipa ya damu (Veins) kuzunguka eneo la tundu la haja kubwa
Hili huweza sababishwa na mambo yafuatayo :
Kukaa chooni kwa muda mrefu
Tatizo la kuwa na haja kubwa ngumu kwa muda mrefu
Kuharisha sana kwa muda mrefu
Kula vyakula visivyokua na nyuzinyuzi
Kulegea kwa tishu maeneo ya tundu la haja kubwa (Hili husababishwa na swala zima la uzee au ujauzito )
Kunyanyua vitu vizito mara kwa mara

Dalili za BAWASIRI YA NJE :
*Muwasho katika tundu la haja kubwa
*Uvimbe mmoja au zaidi pembezoni mwa tundu la haja kubwa
*Maumivu ya njia ya haja kubwa , hasa wakati wa kukaa
*Swala la kujisafisha au kujikuna mara kwa mara kutaongeza tatizo liwe kubwa zaidi. Hali hii huweza kuisha ndani ya siku chache

BAWASIRI YA NDANI :
..Damu kutoka katika njia ya haja kubwa , hasa wakati wa kujisafisha au wakati wa kujisaidia
..Maumivu utayasikia wakati wa haja au unapobanwa na haja kubwa. Mara nyingi ni ngumu sana kuhisi maumivu hadi sehemu iliyoathirika itoke nje ya tundu la haja kubwa , yani kama kinyama hivi kutoka ndani ya puru

NAMNA YA KUJIKONGA
•Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi
•Tumia dawa za kulainisha haja kubwa au virutubisho vyenye nyuzi nyuzi ( Fiber suppliments )
•Kunywa maji ya kutosha kila siku
•Usitumie nguvu kubwa kujisukuma wakati wa haja kubwa
•Usikae chooni muda mrefu (Hasa vile vyoo vya kukalia)
Fika mlimani tower ghorofa ya tatu uliza Dr .Amosi

usisahau kunipigia kura ,ubarikiwe sana *******
 
Je walikuambia imefika stage ya ngapi?
Usiwe na wasiwasi kuna virutubisho lishe(diaterysupplements) ambayo itakayomaliza tatizo lako pasipo upasuaji kwa kitaalamu kama rubber band ligation au hemorrhoidectomy
Kwa mawasiliano zaidi piga +255715059944 na pia utapata huduma za kitabibu bure(free consultation)
Mkuu funguka vizuri hapa "rubber band ligation au hemorrhoidectomy" hizi inakuaje kuaje?? Na mnapatikana wapi?
 
Habari za majukumu members,, samahani nasumbuliwa na ugonjwa wa bawasili(kuota vinyama sehemu ya haja kubwa) karibia mwaka wa pili sasa, mwenye kuweza kunisaidia dawa either ya hospitali au ya kienyeji ili niweze kutumia maana kinanisumbua sana wakati wa kukaa na ninapoenda haja kubwa,, Tafadhali naombeni msaada wenu!
 
Habari za majukumu members,, samahani nasumbuliwa na ugonjwa wa bawasili(kuota vinyama sehemu ya haja kubwa) karibia mwaka wa pili sasa, mwenye kuweza kunisaidia dawa either ya hospitali au ya kienyeji ili niweze kutumia maana kinanisumbua sana wakati wa kukaa na ninapoenda haja kubwa,, Tafadhali naombeni msaada wenu!
Nenda hospital
 
Mkuu, bado haujaeleweka vizur, wewe umejuaje kuwa hiyo Ni bawasili na si ugonjwa mwingine??

Kwa namna unavyosema vinyama vimeota, hii inaashiria pengine sio bawasili, so funguka usaidiwe mawazo kwa kujibu yafuatayo?

Hali hiyo ilianzaje? Wewe shughuli zako za kiuchumi Ni zipi? Umewahi kuugua kikohozi kwa muda mrefu? Je, umewahipata tatizo la kukosa haja kubwa? Kama jibu ni ndio kwa muda gani?? Je, unapoenda haja kubwa unapata maumivu? Haja kubwa inaambatana na damu? Kuna miwasho unapata sehemu za haja kubwa?

Jibu hayo Kwanza tuone, vinginevyo nenda hospital pengine sio bawasili Kama ulivyodhania!!!!
 
Hiyo dawa anauzaje na ni dozi ya siku ngapi mkuu
Mimi nilikua na tatizo hilo, bado natumia dawa inaelekea kupona kabisa. Ni ya kupaka na kunywa.
Haina limit ya siku
20211024_125957.jpg
 
Brother. Uliponaje bawasiri?
Namie nateseka ndugu, naogopa kufanyiwa operation.
Wewe uliponaje. Nisaidie ushauri
Kama ni ya ndani ile inatokeza ukienda haja kubwa basi jitahidi kwanza kutawaza kwa maji siyo tishu wala magunzi. Pili ukimaliza kusafisha eneo lile vizuri basi tumia kidole chako kuisukuma nyama ndani isibaki nje. Ikibaki nje ina maumivu makali sana. Hakikisha unaisukumia ndani kabisa yote. Inasaidia kabisa kuondoa discomforts na utaweza kukaa muda mrefu bila haraka ya operation
 
Otherwise kuna namna ya tiba ya kutumia dawa ya mlingoti, ni ya kufukiza kwa siku kadhaa na inatibu hili tatizo bila haja ya upasuaji
 
Habari za majukumu members,, samahani nasumbuliwa na ugonjwa wa bawasili(kuota vinyama sehemu ya haja kubwa) karibia mwaka wa pili sasa, mwenye kuweza kunisaidia dawa either ya hospitali au ya kienyeji ili niweze kutumia maana kinanisumbua sana wakati wa kukaa na ninapoenda haja kubwa,, Tafadhali naombeni msaada wenu!
kama maumivu na makali sana hayazuiliki nenda kafanye upasuaji tu me nnayo ya ndani ila nkiwa napata choo laini na nkitumia anusol nasahau hata miezi 6 ! dawa nyengine story tu utapigwa hela
 
Back
Top Bottom