Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Wakuu habari zenu!
Mi ninatatizo hili na sijui ni kwa nini ninalo ila nataka nijue kama kuna tiba yake maana linanitia wasiwasi mno.
Natanguliza shukrani wakuu...

Mkuu Nikhili, ebu rudia kuuusoma uzi wa jinsi ya kujieleza kwa daktari hapo juu, nahisi utaweza kusaidia sana hata kama si kwa daktari ila unafupisha kiasi iweze kuleta hata muungano wa mawazo. ila wewe umeelezea hivi kwa ufupi kila mtu ataanza kukuelezea tu kitu kinachohusiana na damu, unaona hata mtaalamu Mzizimkavu ashateremka nondo za tatizo lake mwingine pia atakuja na tatizo lingine na kulishusha mpaka chini kwa maelezo mwisho hataweza kukusaidia wewe,mie na hata wengine. Ila kwa kifupi kinyesi kuchanganyikana na damu si dalili nzuri kwa kusema ivo tuuu....na unatupa maswali zaidi kuliko majibu ya kusaidia mfano naanza...lilianza lini, je damu inaanza kabla ya choo, au baada ya choo au inachanganyika kabisa kama ulivyosema, je kuna maumivu yoyote unayasikia kabla .wakati na baada ya kujiasaidia, au hata muda wote, je unahisi maumivu au uvimbe wa tumbo, je ushawahi kutapika damu au manjano, je ushawahi umwa kichocho,au kuongezewa damu au kunywa pombe kali kwa muda mrefu, au unahisi na manjano ya macho.......kwa kifupi atleast useme yale unahisi yanaweza kusaidia ili kupunguza maswali na watu waweze kulenga tatizo zaidi..ila narudia tena damu kutoka na njia kubwa mara nyingi si dalili nzuri maana kuna magonjwa mengine yanahitaji medical attention na kufanya invstigation zaidi na za haraka...pole kwa maelezo
 
Huu ni USHUHUDA wa kweli: Kwa wale wenye tatizo la bawasiri au piles KITUNGUU SWAUMU kinatibu. Ilikua kama jaribio tu but it works.
 
Huu ni USHUHUDA wa kweli: Kwa wale wenye tatizo la bawasiri au piles KITUNGUU SWAUMU kinatibu. Ilikua kama jaribio tu but it works.
  • Mkuu ungetoa mwangaza kidogo.
  • Je ni kiasi gani cha kitunguu kitumike?
  • Je ni kwa muda gani?
Karibu.
 
Mkuu huna maumivu sehemu yoyote ya Tumbo? Manake sababu ni nyingi
1. vidonda vya tumbo au peptic ulcer or gastric ulcer
2. stomach cancer
3. colon cancer nk..so nivizuri ukajieleza vizuri kwani damu haiwezi toka bila kua na sehemu inayovuja ndani! Tatizo lako linaweza kua kubwa kuliko unavyofikiri so ni vizuri ukaenda hospital kubwa eg KAIRUKI or Regency kwa vipimo zaidi ! Apa wote tutakupa expirience tu lakini vipimo ndo kila kitu na BAWASIRI sidhani kwan maumivu yake kwenye INYE ni nomaaa
 
jamani mimi ndo natatizo hilo limeanza jana nashindwa hata kutembea vizuri. Sasa hicho kitunguu swaumu unafanyaje?
 
1. Menya punje ya saumu, moja mara tatu kwa siku utafune na umeze 2. Kamua juice ya saumu apply penye uvimbe kila baada ya kuoga. 3. Pamoja na hayo, kunywa maji mengi na tumia matunda sana kama papai. Inshala Mungu atajalia. (Bado naifanyia utafiti hii dawa)
 
huu mziki sio wenyewe kabisa! hatari kwanza ni aibu kutangaza kwenye jamii (it need heart kwenda duka la dawa kumwambia mdada muuzaji kuwa mgodi hautoi vizuri na umevimba) nini sasa kwa daktari si huwa hatuendi?
ngoja tujaribu ila tiba halisi itabaki kuongeza mbogamboga na matunda pia maji mengi halafu kungunguza red meat hasa nyama choma na vyakula vya ngano yaani chapati imo
 

Nimeteseka sana na hiyo kitu na kutumia dawa nyingi ila nimekuja kupona kwa papai na maji mengi pamoja na kupunguza matumizi ya nyama na vyakula ambavyo vinapelekea kupata choo kigumu.

Kwa urahisi dawa nzuri ni kunywa maji mengi, kula papai mara nyingi iwezekanavyo (Papai linasaidia kulainisha chakula so hata ukila nyama ukala na papai kubwa haina shida) pia mtori na ndizi za kupika pamoja na mbivu ni chakula kizuri sana kwa kusaidia kupunguza bawasiri
 
kitaalamu linaitwa MELAENA: production of black feces: a condition characterized by the production of black stools that are caused by bleeding into the bowel and the subsequent chemical changes in the blood effected by the bowel fluids.

Tafuta dawa inaitwa SYLATE ambayo its generic name ni Etamsylate..Itakusaidia.
 


Umeeleza vyema mkuu, pia tatizo la kukosa choo ama CONSTIPATION upelekea mtu kupata matatizo yaliyoelezwa hapo juu, hii upelekea kutokea kwa mgandamano wa uchafu katika utumbo mpana, kukosa kupata choo jinsi inavyopaswa upelekea kupata matatizo mengi ya kiafya ata kufikia kupata SARATANI YA UTUMBO MPANA au COLON CANCER ambayo inashika nafasi ya nne duniani kwa kusababisha vifo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO. PATA TAARIFA ZAIDI HAPA

Njia za kuzuia tatizo hili ni pamoja na:-

http://bongopicha.blogspot.com/2012/07/colon-cancer-2-saratani-ya-utumbo-mpana.html
Tatizo hili lisipotatuliwa upelekea mtu kuweza kupata magonjwa sugu kama:


  • Saratani ya utumbo mpana (Colon Cancer)
  • Presha (Arteriosclerisis)
  • Kuongezeka uzito (Obesity)
  • Tumbo kujaa gesi
  • Magonjwa ya Ini
  • Figo kushindwa kufanya kazi vizuri,
  • Magonjwa ya ngozi,
  • Kukakamaa kwa mishipa ya damu,
  • Kisukari,
  • Magonjwa ya moyo n.k
Waweza n-PM au TEMBELEA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI.

 
Nenda hospitali ukaangaliwe na upatiwe matibabu, ni ugonjwa unaotibika, upasuaji huwa ndio suluhisho pale dawa zinapokuwa zimetumika na hazina mafanikio, baada ya upasuaji ni vizuri kuzingatia mambo ambayo umeshauriwa hapo juu, ili hali hiyo isijirudie, hasa life style muhimu chakulakula matunda kama papai au maziwa mtindi, mboga za majani, punguza mikate, tafutia suluhu kila mara mambo haya huchangia haemorhoids
  • Kujikamua sana wakati hasa wa haja kubwa.
  • Kubeba vitu vizito( huwapata zaidi watu kama wa sokoni wabeba magunia)
  • Kutokutibia kikohozi cha muda mrefu( Chronic cough)
  • Mengine wadau wamechangia
Pole sana kwa masahibu haya, nawakiisha mchango wangu
 
nakubaliana na mimi49 amekupa ushauri mzuri kabisa dawa unazopewa ni kupunguza maumivu tu binafsi ilinitokea nikiwa mjamzito bt na nilitumia annusol kila siku lkn hakikuisha ila baada ya kujifungua tu kakatoweka so fuata ushauri huo wa mm mambo yatakuywa sawa
 
Last edited by a moderator:
Pole sana dada,piga 0767 289401 Dr.Laizer.Atakusaidia
 
Habari zenu wanajamvi? Jamani mimi nina tatizo, tatizo langu ni kwamba nina kauvimbe kilichopo kwenye tundu ya haja kubwa kwa ndani. Kauvimbe hako kimekaa upande mmoja kwenye round ila kwa ndani hivyo ukitaka kupagusa lazima utumbukize kidole. Kauvimbe haka kananinyima raha kabisa kwani kameufanya mwili wote uwe unauma, ikiwemo homa za mara kwa mara zikiambatana na baridi kali ambalo huanzia tumboni pamoja vidonda mdomoni, kunichosha mwili na vidonda mdomoni. Nimekwenda kwenye hospital mbalimbali na kupata dawa tofauti tofaut lakini bado sijapata nafuu yoyote. Baadh ya dawa nilizotumia ni anusol ambayo huitumbukiza sehemu hiyo ya haja kubwa. Jamani nimekuwa nakosa raha kabisa kwa tatizo hili hivyo kwa mwenye ufahamu wowote juu ya tatizo si vibaya ukatoa mchango wako hapa huenda ukawa na msaada kwangu ili kuondokana na tatizo hili kwani nadharirika pale ninapokwenda hospital na daktari hutaka kunichungulia ili ajiridhishe!
 
pole sana mkuu.

Hilo tatizo linaitwa hemorrhoid ama kwa kiswahili huitwa vikanga. ni tatizo ambalo mpaka kikatwe ndipo kinaisha. ara nyingi sana huwez kumpata mtu sehem ya nyuma (haja kubwa) kama huwa ana pupuu choo kigumu, ama anaingiliwa nyuma(of which naamin wewe sio) choo hiki kigumu hutokana na ukosefu wa maji ya kulainisha like unapata rafegge nyingi lkn hunywi maji ya kutosha.

kwa mwanamama huweza pia kumpata mbelen na kama akivipata hivi basi akizaa mtoto mtoto huwa mgojwa mgonjwa sana na humnyima mtoto mwili yaani huwa mnyongevu. kwa siye tuliozaliwa zamani kuna namna vinakatwa hivi na wabibi kisha wanavipaka dawa za majani vinatoweka kabisa. siku hizi hosp wanakata so mwone daktari wako kwa matibabu zaid
 
Ahsante mkuu gfsonwin kwa ufafanuzi wako mzuri, ila mimi hupata hofu ninapougusa uvimbe huu nahisi umekuwa kama mshipa mdogo hivi uliotokea kwa ndani (mawazo yangu). Kuna daktari mmoja aliniambia kuna kipimo atakifanya mwenyewe alikiita sijui protoscope, alinitumbukiza vibomba flani sehemu ya haja na hatimaye akanipa dawa za kuminya kama kityubu hivi lakini hakuna kilichoendelea. Ila nashukuru na nitaufanyia kazi ushauri wako.
 
Last edited by a moderator:
Kiswahili maarufu ni BAWASIR. huo ni mshipa wa damu ukitoboa inakula kwako maana utatoka damu mpaka basi. Hospitali wanafanya operation ndogo kinatoka. Pia wamasai wanazo dawa za kutibu hayo makitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…