Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Wadau mimi ni muhanga wa hii kitu ilifikia stage nikimaliza kukata gogo kuna kinyama lazima nikirudishe ndani,mwishowe kilitokea kingine kwa nje kikawa kinauma ajabu na kukua kwa kasi ya jabu ndani ya wiki 2 kilishafikia size ya kidole kidogo.Nilijaribu dawa karibu 3 zote ziligoma ikiwemo ile ya kuweka ndani ya tundu,suluhisho ilikuwa ni operation,ni miezi 3 imeshapita niko fiti kabisa ila cha muhimu baada ya operation unatakiwa ujitahidi kula matunda sana hasa papai maana pale chini panakuwa na kidonda na kinauma sana ukipata choo sasa kama choo ni kigumu maumivu yanakuwa makali zaidi.Utapigwa ganzi kabla ya operation,na inapofanyika hakuna utakachosikia ila ukishatoka baada ya masaa kama 3 hivi ndio utasikia maumivu,jitie ujasiri kwani blia hivyo maisha yako yanakuwa ni ya usumbufu sana.
 
Kwa kweli Ugonjwa huu unasumbua na pia japokuwa wahenga walisema mficha maradhi kifo humuumbua,kiukweli ugonjwa huu ni Aibu hata kumuelezea jirani yako wa karibu.

Ni Ugonjwa Ambao watu wengi Hujiskia Aibu hata kwenda hospitali kutibiwa mimi nikiwa mmojawapo Wana JF,Huu ugonjwa kwa kweli humfanya mtu kufedheheka na kujiona yupo tofauti na watu wengine, kwani hufikia mda hata kukaa chini napo ni Tatizo, yakubidi mda wote uwe umelala, kwani hata kukaa tu ni sababu zinazopelekea ugonjwa huu kuongezeka na maumivu makali.

Ugonjwa huu niliupata December 2014, Wakati nikiwa nafanya kazi katika kiwanda kimoja hapa Dar, Na sababu kubwa iliyopelekea kujikuta naupata ugonjwa huu ni kufanya kazi nikiwa nimesimama kwa muda mrefu, yaani masaa 12.

Hivyo kufanya kazi kwa muda mrefu kulinisababishia (Anal muscles) au misuli ya mkundu, kupata pressure ambayo ilipelekea kutokea uvimbe au kijinyama sehemu ya haja kubwa, kitaalam huitwa EXTERNAL HEMORRHOIDS.

Kwa kweli kabla ya kupata ufahamu wa ugonjwa huu nipipatwa na uwoga mkubwa na aibu, hata wazazi wangu nilishindwa kuwaelezea kwani nilijua huu sii ugonjwa wa kawaida, na mda mwingine nilifikia hatua ya kupenda kuishi peke yangu kwani sikutaka mtu yeyote ajue.

Kwani haikuwahi kunitokea katika maisha yangu na nilidhani si ugonjwa wa kawaida na yawezekana mimi ndio mtu wa kwanza kunitokea, na mda mwingine niliogopa kumueleza mtu yeyote kwa kudhaniwa kuwa tayari nishajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kiukweli niliogopa sana hivyo nikafanya siri kwani bado ndani ya wiki mbili tokea niupate huu ugonjwa uvimbe bado ulikuwa mdogo na wala haukuwa na maumivu yoyote kwa kipindi kile.

Wana Jf Jinsi mda ulivyokuwa unazidi kwenda na uvimbe uliongezeka, na maumivu yaliongezeka, hata kukaa chini kwa dakika moja nilishindwa mda wangu wote niliutumia kulala tu, hata kazi niliacha kwani sikuweza tena kufanya Kwa kuwa bado nilikuwa najiskia aibu kuweka wazi ugonjwa huu.

Siku moja niliamua kutafuta ufumbuzi wa tatizo langu kwenye mtandao, Niliingia google, nikasearch (UVIMBE SEHEMU YA HAJA KUBWA) hapo ndipo nilipogundua kumbe huu ni ugonjwa unaosumbua dunia nzima na wala sio mimi peke yangu, mitandao, blogs, na hapa jf nilipata elimu ya huu ugonjwa kwani umeshawasumbua na unawasumbua watu wengi sana .

Wana JF japo nilijua kuwa huu ugonjwa unajulikana na unatibika mahosipitalini, lakini bado niliogopa kwani kwa elimu niliyoipata hapa Jf.

Hatua za ugonjwa huu nilizofikia mimi ni (SURGERY) UPASUAJI tu ndio ulihitajika kuondoa tatizo kwani uvimbe uliongezeka na ukatoka kwa nje, na hali hii wanaita thombosed hemorrhoid, yani ugonjwa tayari umeshakomaa .

Wana JF, kiukweli baada ya kupitia ushuhuda wa watu ambao walishawahi kufanyiwa upasuaji ,hapa Tanzania na hata Nchi za wenzetu, wengi walilalamika kuwa matibabu yake ni gharama, upasuaji wake una maumivu makali, na ugonjwa huu hujirudia tena baada ya kufanyiwa upasuaji.

Wengi pia waliotumia dawa za hospitali hazikuwasaidia ugonjwa huu kwa waliotumia dawa za vidonge na creams za ANUSOL HC. Wengi hawakupona bali ugonjwa ulipungua, na ni wachache ziliwasaidia.

Wana JF nimalizie tu na hatua nlizopitia hadi kupona ugonjwa huu bila kufanyiwa upasuaji.

1 .MTANGULIZE MUNGU KWANZA.

2. CHEMSHA MAJI YA UVUGU UVUGU CHANGANYA NA CHUMVI WEKA KWENYE BESENI KALIA KWA MDA USIOPUNGUA DAKIKA 15.

3. BADILISHA AINA ZA VYAKULA ULIVYOKUWA UNATUMIA MWANZO PENDELEA KULA;
(A) MATUUNDA KWA WINGI.

(B) MBOGA ZA MAJANI.

(C) VYAKULA VISIVYOKOBOLEWA.

(D)MAZIWA.

(E) VYAKULA LAINI.

(D) VIAZI.

USITUMIE VYAKULA HIVI

(A) PILIPILI.

(B) NYAMA NYEKUNDU.

(C) CHAI/KAHAWA,VINYWAJI VYENYE GESI KAMA SODA,BIA nk.

(D) USITUMIE VYAKULA VILIVYOKOBOLEWA/ NGANO KAMA,chapati, mandazi, keki, unga uliokobolewa,nk

4. USIKAE WALA KUSIMAMA KWA MUDA MREFU.

5.TUMIA MAFUTA YA CASTRO OIL,au mafuta nyonyo pakaa sehemu yenye uvimbe, mafuta haya hupatikana kwenye maduka ya dawa asili.

6. HAKIKISHA SEHEMU YENYE TATIZO PANAKUWA PAKAVU NA PASAFI, hata ukitoka msalani jifute na kitambaa kikavu, kusibaki unyevu unyevu.

7. PENDELEA KULA PUNJE MBILI AU TATU ZA KITUNGUUU SWAUMU KILA SIKU.

8. FANYA MAZOEZI MADOGO MADOGO MARA KWA MARA.

Wana JF ,wengi tutumie kipi hapo na uache kipi kati ya hivyo Lakini niwaambia.
 
Pole, Mimi Nina ulcers, sasa Mara nyingi huwa napata constipation, kuna kipindi nikaanza kuhisi kama kinyama kinaota...naona hii ilitokana na kupasuka na kuvilia damu kwa anal muscles kwa sababu ya pressure nlokuwa naaply wakati wa haja...

Nlichofanya nlitafuta majani ya mnyonyo nikawa nayaweka kwenye moto kisha nabandika pale kwenye kiuvimbe...yani kilinywea na kiliisha...bila kusahau kubadili aina ya vyakula.
 
Pole mkuu, Mimi ugonjwa huu niliugua lakini kwa kuwa huwa naamini katika tiba mbadala nilitafuta katika makablasha yangu, kuna matibabu kibao moja wapo ambalo lilikuwa rahisi kwangu kufanya ni matumizi ya vitunguu saumu.

Ponda ponda kitunguu saumu kiasi jipachike huko kwenye ungonjwa kinauma sana! Kaa nacho kwa masaa mawili unakitoa, matibabu yanadai nifanye Mara mbili kwa wiki moja lakini nilifanya kwa siku mbili tu kilipotea na Nina miaka sasa hakijawahi kujirudia
 
Hivi hiyo Bawasiri inaweza kuja kwa njia ya haja kubwa kwa nje kuchanika? Yaani inakuwa na maumivu katika hivyo vimchaniko mpaka mtu anaogopa kujisaidia !
 
Kuna tatizo limempata rafiki yangu la kuoto kwa vinyama sehemu sa siri, tatizo ilo lilimuanza kwa kuota kama
vipele ila vikaanza kukuwa kisha kutengeneza kama vinyama.

Ambavyo kwa juu vimejitengeneza kama vijistari kwa kuachiana, ni vinamuasha kwa muda kisha vinaachia.

Msaada wenu mwenye kujua ilo tatizo na msaada wa kimatibabu pia.
 
FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba

JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI?
~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe

~Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
~Tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50

AINA ZA BAWASIRI

Kuna Aina mbili za bawasiri

(A) BAWASIRI YA NDANI
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili

Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa

Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika
(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia
(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe
(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi

(B)BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

CHANZO CHA TATIZO
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷

KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
KUHARISHA KWA MUDA MREFU
TATIZO LA KUTOPATA CHOO
MATATIZO YA UMRI
KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
UZITO KUPITA KIASI
MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU

DALILI ZA BAWASIRI
Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI

Matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa ya alo sinaca na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo

Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZSZOKOBOLEWA
KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU

MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI

Kupata upungufu wa damu (anemia)
Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
Hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
Kuathirika kisaikolojia
Kukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na maumivu makali

Nashauri Ufike Hosp Mapema sana kabla ttz halijawa kubwa
 

Usikariri mkuu....hemorrhoids ni vinyama vinavyoota sehemu ya haja kubwa.....kutokana na mdau aavyojieleza nadhani amepata maambukizi ya kirusi hpv (human papilloma virus) ndio inasababisha uoto huo kwenye sehemu za siri..

Mdau kamuone daktari maana hpv husababisha kansa ya shingo ya uzazi (cervical cancer )
 
Naomba unisaidie maana mtoto wangu analo tatizo hili nikaenda hospitali wakanipa anusal yaan ameshatumia sana na hospitali wakaniambia hawajawah kumfanyia upasuaji mtoto mdg hivi ila nijitahid kumpa mbogamboga, matunda kwa wingi pamoja na maji mengi.... plz nisaidie
 
Mkuu aminas, kama alivyosema e-doc na mwalu mimi pia nafikiri hizo ni genital warts ambazo mkimuona daktari wa wakina mama sio tu ataweza kuzitibu lakini ataangalia kama hivyo virusi vimeathiri sehemu zake nyingine za uzazi.

Maelezo ya cc12 yanahusu sana matatizo aliyosema Annah Mosha na mgazanyau. Kuchanika kwenye sehemu ya haja kubwa mara nyingi huletwa na constipation - choo kigumu. Jaribuni kumpa huyo mtoto vyakula vitakavyolainisha choo chake kikubwa.

Hemorrhoids pia zinaweza kusababishwa na constipation au uzazi na hizi vimbe mara nyingi zinakuwa ni mishipa ya damu inayofutuka kwa ajili ya kujikaza wakati wa haja kubwa au uzazi na baadae huchanika na kutoa damu. Hemorrhoids ambazo sio mbaya sana unaweza kutumia suppositories na hupona kirahisi lakini kama ni chronic basi mgonjwa atahitaji operation. Kwa vyovyote vile nendeni mkawaone madaktari.

Mimi sio daktari bali nimewauguza wanafamilia wengi wenye matatizo hayo.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu mim sio Daktari ila nashauri Uende Hosp pamoja na mwanao matibabu yapo na ugonjwa unaitibika usiende mwanyamali alafu ukasema wameshindwa nenda hosp kubwa kama Tumbi KMCMC kama hizi ndogo ndogo zimeshindwa
 

Mkuu mim sio Daktari ila nilisoma tu mahali na nilichosoma naona kama kinarelate na maeleza ya huyu dada
 
Mkuu mim sio Daktari ila nashauri Uende Hosp pamoja na mwanao matibabu yapo na ugonjwa unaitibika usiende mwanyamali alafu ukasema wameshindwa nenda hosp kubwa kama Tumbi KMCMC kama hizi ndogo ndogo zimeshindwa

Nilienda St. Joseph -Soweto then KCMC ndo walioniambia hivyo... nimemuachia Mungu ila najitahid kumpa vitu/vyakula nilivyoambiwa kwa ajili ya choo
 
Nilienda St. Joseph -Soweto then KCMC ndo walioniambia hivyo... nimemuachia Mungu ila najitahid kumpa vitu/vyakula nilivyoambiwa kwa ajili ya choo

Mkuu ebu Mtafuta huyu mtu anaweza kukusaidia 0689538628 ttz lako
 
Msaada jamani leo ni siku ya pili nipo tu ndani sehemu ya haja kubwa upande mmoja imevimba na kutokeza nje hali inayoniletea maumivu sana je kuna mwenye kujua dawa anisaidie
 
Nenda hospitali ndugu utapata dawa hali hiyo hutokana na matatizo mbalimbali kwenye misuli ya sehemu za puru na ugonjwa huitwa bawasiri.Muone daktari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…