Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

jamani me pia nilipata tatizo hilo hilo, baada ya kumwelezea doctor kuwa kuna kinyama kinauma hatari yani wakati wa kukata gogo na kipo kwa nje kidogo basi pale wakati naendelea kumwelezea na yeye akaniambia hilo tatizo mara nyingi hata wabeba vyuma huwa linawakuta na ndio nikamwambia hapo hapo doctor kama ulimeniona vile, nakumbuka kuna dawa alinipa ya kumeza na kupaka akaniambia hiidozi ni kiboko tatizo lako lazma liishe hapo na dozi ya kupaka ilikuwa ni ucku tu ukiwa unataka kulala, basi ndani ya siku 5 mchezo ukaisha na ndio ntolee mpaka leo, hospitali niliyoenda ni sinza palestina na nilitibiwa na bima tuu. Ila tatizo nimesha sahau na dawa yenyewe ilikuwa inaitwa nn.

Mkuu tuangalizie kwenye makabrasha yako mkuu tupate jina la hiyo dawa angalau na sisi wa huku nyasa tujikomboe. Maan niko na anko analamika hilo tatizo na hatukupata dawa madhubuti ya kutibu baada ya kwenda hospital.
 
nenda hospitali mkuu humu utakutana na kina dr. ndoodi wakuanzishie dozi ya mizizi ya vitunguu bure
 
Ninapenda kuwafahamisha kuwa wenye tatizo hili linaloongelewa hapa sasa kuna tiba mbadala, Aunt Zainab Natural Super Clay imesaidia sana wanaoota vinyama sehemu hizo za siri na hata mwilini.

Aunt Zainab's Natural super Clay ni dawa 100% asilia na haina madhara wala side effects mwilini, kwa watu wazima watoto wadogo na hata wajawazito.

ILicha ya tatizo hilo la bawasiri, inasaidi sana kwa magonjwa yote ya ngozi.

Pitia hapa: https://www.jamiiforums.com/jf-doct...na-zaidi-aunt-zainabs-natural-super-clay.html

https://www.jamiiforums.com/matanga...ural-unaolainisha-ngozi-sasa-unapatikana.html
 
Kwa kweli Ugonjwa huu unasumbua na pia japokuwa wahenga walisema mficha maradhi kifo humuumbua,kiukweli ugonjwa huu ni Aibu hata kumuelezea jirani yako wa karibu,ni Ugonjwa Ambao watu wengi Hujiskia Aibu hata kwenda hospitali kutibiwa mimi nikiwa mmojawapo
Wana JF,Huu ugonjwa kwa kweli humfanya mtu kufedheheka na kujiona yupo tofauti na watu wengine,kwani hufikia mda hata kukaa chini napo ni Tatizo,yakubidi mda wote uwe umelala,kwani hata kukaa tu ni sababu zinazopelekea ugonjwa huu kuongezeka na maumivu makali
Ugonjwa huu niliupata December 2014,Wakati nikiwa nafanya kazi katika kiwanda kimoja hapa Dar,Na sababu kubwa iliyopelekea kujikuta naupata ugonjwa huu ni kufanya kazi nikiwa nimesimama kwa muda mrefu,yaani masaa 12,
Hivyo kufanya kazi kwa muda mrefu kulinisababishia (Anal muscles) au misuli ya mkundu,kupata pressure ambayo ilipelekea kutokea uvimbe au kijinyama sehemu ya haja kubwa..kitaalam huitwa EXTERNAL HEMORRHOIDS
Kwa kweli kabla ya kupata ufahamu wa ugonjwa huu nipipatwa na uwoga mkubwa na aibu,hata wazazi wangu nilishindwa kuwaelezea kwani nilijua huu sii ugonjwa wa kawaida,na mda mwingine nilifikia hatua ya kupenda kuishi peke yangu kwani sikutaka mtu yeyote ajue,kwani haikuwahi kunitokea katika maisha yangu na nilidhani si ugonjwa wa kawaida na yawezekana mimi ndio mtu wa kwanza kunitokea,na mda mwingine niliogopa kumueleza mtu yeyote kwa kudhaniwa kuwa tayari nishajihusisha na mapenzi ya jinsia moja,kiukweli niliogopa sana hivyo nikafanya siri kwani bado ndani ya wiki mbili tokea niupate huu ugonjwa uvimbe bado ulikuwa mdogo na wala haukuwa na maumivu yoyote kwa kipindi kile
Wana Jf Jinsi mda ulivyokuwa unazidi kwenda na uvimbe uliongezeka,na maumivu yaliongezeka,hata kukaa chini kwa dakika moja nilishindwa mda wangu wote niliutumia kulala tu,hata kazi niliacha kwani sikuweza tena kufanya
Kwa kuwa bado nilikuwa najiskia aibu kuweka wazi ugonjwa huu
Siku moja niliamua kutafuta ufumbuzi wa tatizo langu kwenye mtandao,Niliingia google,nikasearch (UVIMBE SEHEMU YA HAJA KUBWA)
hapo ndipo nilipogundua kumbe huu ni ugonjwa unaosumbua dunia nzima na wala sio mimi peke yangu,mitandao,blogs,na hapa jf nilipata elimu ya huu ugonjwa kwani umeshawasumbua na unawasumbua watu wengi sana
Wana jf japo nilijua kuwa huu ugonjwa unajulikana na unatibika mahosipitalini,lakini bado niliogopa kwani kwa elimu niliyoipata hapa Jf,Hatua za ugonjwa huu nlizofikia mimi ni (SURGERY) UPASUAJI tu ndio ulihitajika kuondoa tatizo kwani uvimbe uliongezeka na ukatoka kwa nnje,na hali hii wanaita thombosed hemorrhoid,yani ugonjwa tayari umeshakomaa
wana jf,kiukweli baada ya kupitia ushuhuda wa watu ambao walishawahi kufanyiwa upasuaji ,hapa tz na hata Nchi za wenzetu,wengi walilalamika kuwa matibabu yake ni gharama,upasuaji wake una maumivu makali,na ugonjwa huu hujirudia tena baada ya kufanyiwa upasuaji,wengi pia waliotumia dawa za hospitali hazikuwasaidia
ugonjwa huu kwa waliotumia dawa za vidonge na creams za ANUSOL HC,Wengi hawakupona bali ugonjwa ulipungua,na ni wachache ziliwasaidia
Wana jf nimalizie tu na hatua nlizopitia hadi kupona ugonjwa huu bila kufanyiwa upasuaji
1.MTANGULIZE MUNGU KWANZA
2.CHEMSHA MAJI YA UVUGU UVUGU CHANGANYA NA CHUMVI WEKA KWENYE BESENI KALIA KWA MDA USIOPUNGUA DAKIKA 15
3.BADILISHA AINA ZA VYAKULA ULIVYOKUWA UNATUMIA MWANZO PENDELEA KULA
(A)Matunda kwa wingi
(B)MBOGA ZA MAJANI
(C)VYAKULA VISIVYOKOBOLEWA
(D)MAZIWA
(E)VYAKULA LAINI
(D)VIAZI

USITUMIE VYAKULA HIVI
(A)PILIPILI
(B)NYAMA NYEKUNDU
(C)CHAI/KAHAWA,VINYWAJI VYENYE GESI KAMA SODA,BIA nk.
(D)USITUMIE VYAKULA VILIVYOKOBOLEWA/NGANO KAMA,chapati,mandazi,keki,unga uliokobolewa,nk

4.USIKAE WALA KUSIMAMA KWA MUDA MREFU
5.TUMIA MAFUTA YA CASTRO OIL,au mafuta nyonyo pakaa sehemu yenye uvimbe,mafuta haya hupatikana kwenye madikuka ya dawa asili
6.HAKIKISHA SEHEMU YENYE TATIZO PANAKUWA PAKAVU NA PASAFI,hata ukitoka msalani jifute na kitambaa kikavu,kusibaki unyevu unyevu
7.PENDELEA KULA PUNJE MBILI AU TATU ZA KITUNGUUU SWAUMU KILA SIKU
8.FANYA MAZOEZI MADOGO MADOGO MARA KWA MARA

Wana JF ,wengi r utumie kipi hapo na uache kipi kati ya hivyo
Lakini niwaambie tu ndio dawa pekee zilizomaliza tatizo na kuniepusha na kufanyiwa upasuaji
SIFA NA UTUKUFU APEWE MWENYEZI MUNGU
ASANTENI SANA
 
nilijua unatangaza biashara maana ndio gia za wengi... kwanza pole kwa yaliyokusibu...pia hongera kwa kupona na asante kwa kutujuza tiba...
 
kweli mungu ni.mwema kabisa, wajulisheni na wengine waelimike kupitia hapa,kwani ni tiba rahisi isiyo na maumivu wala gharama na nisalama kabisa
 
Huu ugonjwa ukiuvumilia vizuri nahisi unapona wenyewe miaka ya 1998 niliupata na nikapewa tarehe ya appointment KCMC kwa ajili ya operation. Tena niliomba nifanyiwe mapema wakakataa wakanipa tarehe ya mbele. Ile tarehe ilipofika nikashangaa kauvimbe kanapungua taratibu na baada ya wiki moja kakapotea. Mwaka 2002 kakaanza tena..ila haka hakakuwa kakubwa kama kale ka mwanzo nacho nikakapotezea. Hakakkuendelea sana kakaja kupotea. Hadi leo sijawah kusikia tena.
 
ni kweli yani pia mfumo wa maisha ni muhimu sana kubadilika haswaa kwenye ulaji ,itasaidia ugonjwa huu kutorudi tena
 
Dawa rahisi na ya bure kabisa ya kupona kabisa hilo tatizo ni kumwamini Mungu na kukubali kuombewa katika Jina la Yesu na kuendelea kutenda kama Mungu anavyotaka, nenda kwa yeyote kati ya Mzee wa Upako-DSM, Nabii Joshua-Morogoro, TB Joshua-Nigeria, n.k kwa ajili ya maombezi utapona kabisa na usiache kutoa ushuhuda hapahapa kwenye jukwaa. Asikudanganye mtu madaktari wote duniani huwa wanatibu tu hakuna hata mmoja anayethubutu kusema amemponya mgonjwa, Mungu pekee ndiyo mponyaji.

Ushauri wako ni.mzuri lkn kuna vitu hujaweka sawa.
Kwenda tu kwa mzee wa upako hakuponyi tatizo,nenda kwa Daktari upate tiba then wakati unaendelea na matibabu unamwomba Mungu akuponye.
Maana binadamu tunatibu lakini anayeponya ni Mungu.Kwenda kwa daktari ni muhimu mno
 
Hivi mtu kuwa na uvimbe kwenye tundu la haja kubwa, Je tatizo ni nini na je dawa ya kuondoa hilo tatizo ni zipi?
 
umeshakwenda hospitali???
Nijuavyo hilo tatzo linaitwa bawasiri, mara nyingi linasababishwa na tatzo la kutokupata choo(constipation).
Nenda kwanza hospital ufanyiwe vipimo, ikitokea utahitaji njia mbadala baada ya hapo ni-pm
 
Ninapenda kuwafahamisha kuwa wenye tatizo hili linaloongelewa hapa sasa kuna tiba mbadala, Aunt Zainab Natural Super Clay imesaidia sana wanaoota vinyama sehemu hizo za siri na hata mwilini.

Aunt Zainab's Natural super Clay ni dawa 100% asilia na haina madhara wala side effects mwilini, kwa watu wazima watoto wadogo na hata wajawazito.

ILicha ya tatizo hilo la bawasiri, inasaidi sana kwa magonjwa yote ya ngozi.

Pitia hapa: https://www.jamiiforums.com/jf-doct...na-zaidi-aunt-zainabs-natural-super-clay.html

https://www.jamiiforums.com/matanga...ural-unaolainisha-ngozi-sasa-unapatikana.html

Untie Zainab sasa unautumia kupaka au kunywa?
 
Back
Top Bottom