Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

BAWASIRI/PILES AU HAEMORROIDS

JIFUNZE MAANA HARISI YA BAWASIRI,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE,KINGA NA MATIBABU YAKE

Nikawaida sana kwa baadhi ya watu kuona aibu kusema kuwa wanaķabiliwa na baadhi ya magonjwa na matokeo yake ni makubwa kwao
-Mojawapo ya magonjwa hayo ni hili la leo.

BAWASIRI ni neno la kiswahili ambalo wengi hawalifahamu,wengi wanafahamu kitalaam HAEMORROIDS au kwa kiingereza PILES.
-Tatizo hili husababishwa na kuvimba,kuharibika na kuondoshwa katika eneo lake kwa mishipa ya damu katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

UTAJUAJE KAMA UNA DALILI ZA BAWASIRI
-Kinyesi kunuka damu wakati wakujisaidia
-Maumivu au usumbufu wakati wakujisaidia
-Mara nyingine kinyesi kuvuja chenyewe
-Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
-Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
-Unapojisaidia kinyama kuchungulia

AINA ZA BAWASIRI

1} BAWASIRI YA NJE
-Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa,na huweza kuambatana na maumivu pamoja na kuwashwa Kwa ngozi katika eneo hilo.Mara nyingine mishipa hiyo ya damu(vena)hupasuka na damu huganda na kusababisha aina ya Bawasiri ambayo kitalaam inaitwa thrombosed Haemorroids

2} BAWASIRI YA NDANI,
-Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa,na huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa haitambui pindi inapo wapata.Hutoka na kuvimba na kuharibika kwa vimshipa vya aina ya atery za ndani ya mfereji wa haja kubwa.

-Aina hii imegawanyika katika madaraja au hatua 4
》》DARAJA LA 1
-Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida

》》DARAJA LA 2
-Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo
》》DARAJA LA 3
-Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu anaweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo
》》DARAJA LA 4
-Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo

NI NINI HASA VYANZO VYA UGONJWA HUU

-Tatizo sugu la kuharisha
-kupata kinyesi kigumu au kutopata zaidi ya siku mbili
-Ujauzito
-Uzito kupita kiasi {obesity}
-Mazoezi yakunyanyua vitu vizito sana
-Kufanya ngono kinyume na maumbile
-Umri mkubwa na mambo yanayoongeza shinikizo katika utumbo mpana kama kukaa muda mrefu mahali pamoja
-Matumizi ya vyoo vya kukaa kuliko vyakuchuchumaa
-Kujisaidia kwa muda mrefu wakati wa haja kubwa

NI NINI HUTOKEA BAADA YAKUWA NA UGONJWA HUU

madhara yake
i}-Mtu kunuka kinyesi
ii}-Kutokwa na kinyesi bila kujijua
iii}-Saratani ya utumbo
iv}-Upungufu wa nguvu za kijinsia
v}-Upungufu wa damu mwilini (Anaemia)

AINA ZA VIPIMO
-Kipimo cha shahada kwa njia ya puru (Digital rectal examination)
-Kipimo cha njia ya haja kubwa cha kutizama moja kwa moja (Proctoscope)
-Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Namna yakuifanya bawasiri ipungue/kupunguza maumivu/uvimbe

-Hutegemea na umri wako na namna ugonjwa ulivyojijenga na kudumu, unaweza kuhitaji dawa moja au mbili au hata tatu kwa pamoja.
-Wasiliana na daktari kwanza kabla ya kuamua kuzitumia dawa.

Dawa za bawasiri kwa mazingira ya nyumbani zilizo kuzunguuka

1.
Habbat-Sawdaa na Asali

Changanya gm 500 za unga wa Habbat-Sawdaa na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila baada ya masaa manne. Ukimaliza kulamba kunywa glasi moja ya maji ya kunywa ya joto la kawaida.

2.
Aloe Vera Fresh

Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata kama utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu. Jipake nyingi tu na uiache hivyo masaa kadhaa au mpaka utakpaoenda kuoga tena.

Tengeneza pia juisi freshi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi 1 kutwa mara mbili kwa wiki 3 hadi 4. Juisi freshi ya aloe vera ni nzuri kwa kuongeza kinga ya mwili na kutoa taka zote za ndani ya mwili.

3.
Juisi ya limau (lemonade)

Chukua juisi ya limau na upake sehemu iliyoathirika. Juisi ya limau sifa yake kuu hapa ni kuondoa sumu na kuongeza kinga ya mwili kwakuwa ina vitamin C kwa wingi. Pia unywe glasi moja ya juisi hii kutwa mara kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

*Chukua asali nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12, zikate katikati kila moja. Tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji Lita 3, chemsha mpaka limau ziive (zisiive sana), ipua utowe zile nyama nyama za ndani za liamau moja baada ya nyingine, ganda la nje tupa na uchuje kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa lita 2 na nusu hivi.

Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya ile asali nusu Lita na hiyo juisi ya limau Lita 2 na nusu, ongeza maji Safi ya kawaida Lita 2 ili kupata lemonade ya ujazo wa lita 5. Ihifadhi katika friji au kama huna friji andaa kiasi kidogo kidogo cha kutumia siku 3 kisha unaandaa nyingine.

Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 hadi 11 hivi.
Unaweza kuongeza vijiko vikubwa vitatu vya mdalasini ya Unga ndani ya hii juisi ya LEMONADE

4.
Mafuta ya nyonyo

Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne hivi.

Mambo muhimu ya kuzingatia ili upone bawasiri:

-Kula vyakula vingi vyenye faiba {nyuzinyuzi/kambakamba}
-Kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha mwili na kuepuka kufunga choo
-Kula sana mboga za majani na matunda
-Tumia mafuta ya mzeituni (olive oil) kwa wingi kwenye vyakula vyako
-Epuka mapenzi kinyume na maumbile
-Epuka kukaa/kuketi kitako sehem moja kwa muda mrefu
-Usinyanyue vitu vizito kupita uwezo wako
-Usiongeze presha kubwa pindi unapo toa haja

KUHUSU DAWA.
PIGA,/text 0658521921/0624073681

Kwa tiba na ushauri
Bawasiri inatibika



Tembelea Facebook page na usisahau ku like
Ijue Afya yako
Google+
https://plus.google.com/109692402036335850762

E-mail
Afyayajamii92@gmail.com
 
Kama utakuwa tayari ni pm nikulekeze wapi pakupata msaada na hill tatizo halitajitokeza tena dawa IPO hakuna haja ya upasuaji
 
maji ya ganda la mgomba unaponda na kupaka kwenye unyeo kutwa mara tatu kwa wiki mbili.mi nimepona .anusol haikunisaidia pamoja na kuitumia kwa miaka miwili .mgomba just two wiki .maelezo zaidi PM.
VP hali hebu nieleweshe kuhusu dawa ya mgomba kwenye bawasir
 
Wakuu huu ugonjwa wa bawasiri,unaponaje,kwa operation au kuna sindano na vidonge?
 
Wakuu huu ugonjwa wa bawasiri,unaponaje,kwa operation au kuna sindano na vidonge?
Ugonjwa wa bawasili unasababiswa sana na life style...ukifanyiwa operation/au kutibiwa na njia nyingine yeyote..... kama utaendelea na style hyohyo..tatizo litakua linarudia tena na tena...unacho paswa kufanya ni kuepuka kupata choo kigumu wakat wote....angalia aina ya vyakula unavyo vitumia..ndo suluhisho na tiba yako.kama unalo tatizo hilo kwa sasa..tafuta dawa inaitwa anusol suppository ya tube ndo nzuri mi rahis kuitumia...fuata maelekezo ya matumuzi na ukisha pona,epuka kutumia vyakula vitavyo pelekea kupata choo kigumu.ahsante
 
Bawasiri ni ugonjwa katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa kiingereza hujuliakana kama haemorrhoids au piles.

Bawasiri inaweza kupelekea upungufu wa damu mwilini. Bawasiri inaweza kutibika ama kwa upasuaji ama kwa matumizi ya dawa mbadala kwa kipindi kirefu wiki hata 6 au hata zaidi kutegemea ilikuwa imejijenga kiasi gani.

Bawasiri husababishwa na nini

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kupelekea wewe kupatwa na ugonjwa huu:

Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
Kuharisha sana kwa muda mrefu
Kutumia vyoo vya kukaa
Kunyanyua vyuma vizito
Mfadhaiko/stress
Uzito na unene kupita kiasi nk
Dalili za bawasiri

Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote
Matibabu ya bawasiri:

Kutegemea na umri wako na namna ugonjwa ulivyojijenga na kudumu, unaweza kuhitaji dawa moja au mbili au hata tatu kwa pamoja kati ya hizi zifuatazo. Kumbuka kumshirikisha daktari wako kabla ya kuamua kuzitumia hizi dawa.

Dawa ya bawasiri

1. Habbat-Sawdaa

Chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa ukoroge ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara mbili kwa wiki mbili mpaka tatu hivi.

2. Habbat-Sawdaa na Asali

Changanya gm 500 za unga wa Habbat-Sawdaa na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila baada ya masaa manne. Ukimaliza kulamba kunywa glasi moja ya maji ya kunywa ya joto la kawaida.

3. Aloe Vera Fresh

Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata kama utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu. Jipake nyingi tu na uiache hivyo masaa kadhaa au mpaka utakpaoenda kuoga tena.

Tengeneza pia juisi freshi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi 1 kutwa mara mbili kwa wiki 3 hadi 4. Juisi freshi ya aloe vera ni nzuri kwa kuongeza kinga ya mwili na kutoa taka zote za ndani ya mwili.

4. Juisi ya limau (lemonade)

Chukua juisi ya limau na upake sehemu iliyoathirika. Juisi ya limau sifa yake kuu hapa ni kuondoa sumu na kuongeza kinga ya mwili kwakuwa ina vitamin C kwa wingi. Pia unywe glasi moja ya juisi hii kutwa mara kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau na asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

*Chukua asali nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12, zikate katikati kila moja. Tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji Lita 3, chemsha mpaka limau ziive (zisiive sana), ipua utowe zile nyama nyama za ndani za liamau moja baada ya nyingine, ganda la nje tupa na uchuje kupata juisi ambayo itakuwa na ujazo wa lita 2 na nusu hivi.

Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya ile asali nusu Lita na hiyo juisi ya limau Lita 2 na nusu, ongeza maji Safi ya kawaida Lita 2 ili kupata lemonade ya ujazo wa lita 5. Ihifadhi katika friji au kama huna friji andaa kiasi kidogo kidogo cha kutumia siku 3 kisha unaandaa nyingine.

Kunywa robo Lita kutwa mara 2 kwa siku 10 hadi 11 hivi.
Unaweza kuongeza vijiko vikubwa vitatu vya mdalasini ya Unga ndani ya hii juisi ya LEMONADE

5. Siki ya tufaa

Chukua kipande cha pamba na ukichovyo ndani ya siki ya tufaa (apple cider vinegar) na ujipake kidogo kidogo eneo lenye uvimbe taratibu. Unaweza kusikia maumivu zaidi lakini jipe moyo taratibu yatapotea. Hakikisha unapata siki ya tufaa ile ya asili kabisa siyo ile iliyopita viwandani.

Pia kama una bawasiri ya ndani yaani ile isiyojitokeza nje na ukaiona kwa macho moja kwa moja unashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa ndani ya glasi ya maji na unywe yote kutwa mara 2. Hii husaidia pia kupunguza maumivu.

6. Mafuta ya nyonyo

Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne hivi.

Mambo mhimu ya kuzingatia ili upone bawasiri:

Kula vyakula vingi vyenye faiba
Kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha mwili na kuepuka kufunga choo
Kula sana mboga majani na matunda
Tumia mafuta ya mzeituni (olive oil) kwa wingi kwenye vyakula vyako
Epuka mapenzi kinyume
 
Jf doctor. Pole nakazi , kwanza napenda kuwapongeza sana kwa kazi yenu hii ya kurekebisha afya na mungu awasaidie .

Mimi nina hili tatizo la kuota vinyama ktknjia ya haja kubwa tatizo hili lilinianza mda mrefu sana sana tangia nikiwa na miaka 17, na nimedumu na mpaka na hisi kukata tamaa kabisa .

Mwanzo ilionekana ni kama sehemu ya haja kubea kama inatokeza wakati wa kutoa taka nilikuwa sielewi niksendahospitali waganga wakaniangali wakaniambia nina kiupele ambapo walinipa dawa fulan sijui jina niwe napaka.lakini haikusaidia kitu baada ya kupita kipindi kirefu kikaota kipere kingine hapo ndio tatizo la kutoa haja kubwa ilikuwa shida zaidi mpaka ikaniperekea sehemu ya mkundu kubaki nje ikaniperekea shida ya kukaa nawakati mwingi kutembea ilikuwa inaniletea shida, nikamua kwenda hospitali moja hivi ambapo wakajadiliana na kuamua kunikata vinyama kimoja baada ya kingine baadaye nikajisikia kama nimepona kabisa.
Ilipita kama mika 6 ikarudia tena ndio mpaka leo kuna kinyama kidogo kinanisumbua sana msaada wenu madoctor kama kuna dawa au ni tatizo lisilodawa naomba nijue maana kelo ninayopata ni ya kukatisha tamaa
Msada bamutu.
 


Kwa ushauri nasaha, nenda kamuone Daktari husika si hapa JF kwani kwa sasa JF imeharibika kwa kuwa na vijana wengi wa Insta na Fesibuku na bongo fleva type. Usipo angalia watakuomba namba yako ya simu wakutongoze na kukushikisha ukuta wakijidai wao ni wajuzi wa hili gonjwa.
 
Oophf!!![emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
JIFAHAMU HUENDA UNATATIZO LA KUTOKUPATA CHOO KWA MDA MREFU(CONSTIPATION) NA UGONJWA WA KUTOKWA NA KINYAMA KWENYE HAJA KUBWA.

WATU wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu ya kuelezea na kushindwa hata kwenda hospitali kupata tiba.

JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI?

~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na Inje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles

~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50

AINA ZA BAWASIRI

~Kuna Aina mbili za bawasiri

(A) BAWASIRI YA NDANI

~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili

~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa

~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne

(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika

(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.

(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.

(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi

(B)BAWASIRI YA NNJE

~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

CHANZO CHA TATIZO

~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambavyo ni ÷

i) KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

ii) KUHARISHA KWA MUDA MREFU

iii) TATIZO LA KUTOPATA CHOO

iv) MATATIZO YA UMRI

v) KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU

vi) UZITO KUPITA KIASI

vii) MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU

DALILI ZA BAWASIRI

i) Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa

ii) kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia

iii) kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa

iv) kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo

v) kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana.

MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI

i) kupata upungufu wa damu (anemia)

ii) Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo

iii) hupunguza nguvu za kiume kwa wanaume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake

iv) kuathirika kisaikolojia

v) kukosa morali ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali

*KWA USHAURI ZAIDI JUU YA UTATUZI WA TATIZO HILI*

WASILIANA KWA 0621068486/0658825141
 
Habari wanajukwaa,
Kama heading inavyojieleza, nilikuwa nasumbuliwa na ugonjwa wa bawasiri :nilijaribu kutumia dawa mbalix2 za kienyeji bila mafanikio ndio ikabidi niende hospital ya Nkinga iliopo tabora na nilifanyiwa operation ambayo ilienda vzur tu kwan tatzo lilikwisha kabisa.
Baada ya miezi miwili (2) tangu operation hiyo damu imeanza kutoka kila nikienda kujisaidia haja kubwa. Ingawa sisikii maumivu ya aina yoyote.
Nilienda hospital ya wilaya wakasema sina tatzo lakn damu inatoka.
Naomba msaada wenu wanajukwaa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…