Pole Laura,
Matibabu ya Haemorrhoids (vivimbe vya damu njia ya haja kubwa) yanategemea na grade ya hilo tatizo. Daktari anakuexamine na kukuuliza maswali kisha anadetermine ni grade ngapi.
- Grade 1: Zinatoka damu wakati wa haja kubwa lakini hakuna kivimbe kilichotokeza nje ya mk*nd* (kumradhi kwa lugha)
Hapa matibabu ni kutumia vidonge maalum vinawekwa kwenye njia ya haja kubwa (rectal suppositories (scheriproct)), na pia kula chakula chenye roughage ya kutosha mfano moboga za majani, matunda kama mapapai, parachichi, embe etc, na maji kwa wingi.
- Grade 2: Zinatoka damu na kuna kivimbe/vivimbe kilichotokeza hasa baada ya haja kubwa lakini kinarudi chenyewe ndani baada ya haja.
Hapa matibabu ni rectal suppositories, chakula chenye roughage na sclerotherapy (sina uhakika kama tiba hii ipo Tanzania tayari).
- Grade 3: Zinatoka damu na kuna kivimbe/vivimbe hasa baada ya haja kubwa, na havirudi vyenyewe..mpaka urudishe kwa kusukuma na kidole/vidole.
Hapa matibabu ni upasuaji tu hamna jinsi.
- Grade 4: Zinatoka damu, kuna vivimbe hata bila haja, vivimbe havirudi hata vikisukumwa na vidole, wakati mwingine maumivu na hata damu kuvilia kwenye vivimbe.
Hapa matibabu ni upasuaji tu hamna jinsi. Na inawezekana hata upausuaji zaidi ya mara mbili au tatu.
Ushauri: Kamuone daktari bingwa wa upasuaji haraka, akuexamine kupata grade, kisha akushauri matibabu gani ni stahiki.