Ndugu zangu wanajf nakuja kwenu kuleta tatizo langu kwenu kuomba ushauri. Mimi ni msichana umri wa miaka 24 nina tatizo sehemu ya haja kubwa kuna kanyama kameota ambako kamedumu zaidi ya miaka 3. Kalianza kama kauvimbe kasikouma wakati sikuchukua hatua yoyote nikidhani kanaweza kupotea lakini kameendelea kukua kuefuka ukubwa kama punje ya haragwe na kuwa na maumivu makali hasa ninapoingia bleed wakati mwingine cwezi hata kukaa. Nilikutana na dr, wa tiba asilia akanambia hiki kinyama kinaitwa BAWASILA kwamba kinahusiana na matatizo ya uzazi akanipatia dawa za kunywa na kupaka lakin hazkunisaidia nilienda hospitali moja hapo dar ambayo inaubia na shule hivyo gharama ni juu ya shule dr, alinichunguza na kuniandikia dawa iitwayo ANUSOL na kwamba ningefanyiwa upasuaji nikapangiwa tarehe lakini haikuwezekana nikawa nasumbuliwa ndani ya miezi 3 mpaka nikaingia kufanya mtihani wa kidato cha sita wakati huo maumivu ni makali. Baadaye nilirudi Mbeya na kumweleza mama tukaenda hospital Dr akasema ni ANAL TAG hivyo akanambia nitumie dawa niliyoandikiwa Dar ANUSOL nimetumia lakin hali ni ileile. Siku moja nilikuwa sehem tumbo la bleed likaniuma sana hapo palikuwa na huduma ya kwanza nikamuona Dr akanichoma sindano ckujua ni dawa gani alitumia tumbo lilitulia na kale kanyama hakajauma tena ndani ya miezi 4 lakini sina amani hivi nilivyo najiona tofauti na wengine nakataa wachumba kwa ajili ya tatizo langu. Nilivyozidi kumdadis mama akanambia amewahi kusikia kuwa hili tatizo lipo katika ukoo wa baba pia kaka yetu wakwanza ashapatwa na hili tatizo lakini alipona mama hakumbuki walitumia nini mpaka akapona. Naombeni msaada wenu sina furaha kama watu wengine wakati mwingine kinaniuma ugenini nashindwa jinsi ya kujieleza. Nawasilisha