Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Inatibika kwa opareshein ya upasuaji nenda kamuone Daktari atakusaidia.

(Hemorrhoids)

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri:
i. Nje
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
ii. Ndani
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;
• Tatizo sugu la kuharisha
• Kupata kinyesi kigumu
• Ujauzito
• Uzito kupita kiasi (obesity)
• Ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
• Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
• Umri mkubwa
Dalili za bawasiri;
• Damu kuchanganyika na kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
• Maumivu au usumbufu
• Kinyesi kuvuja
• Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
• Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
• Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri:
• Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
• Strangulated hemorrhoids

Vipimo na uchunguzi:
i. Digital rectal examination
ii. Proctoscope
iii. Sigmoidoscope
Matibabu :
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
i. Rubber band ligation- Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
ii. Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
iii. Coagulation (infrared, laser and bipolar)
iv. Upasuaji;
-Hemorrhoidectomy
-Stapled hemorrhoidopexy
Jinsi ya kuzuia Bawasiri:
• High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
• Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
• Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
Chanzo :Bawasiri (Hemorrhoids) – TanzMED(old) - Afya Kwa Wote
 
dawa yake ni operesheni,na unakatwa hicho kinyama.ukisha katwa ni vizuri kula vyakula vyenye kulainisha choo,kwani saa nyengine hata ukikatwa tatizo linarudi.
 
we ushakatwa kinyama???
dawa yake ni operesheni,na unakatwa hicho kinyama.ukisha katwa ni vizuri kula vyakula vyenye kulainisha choo,kwani saa nyengine hata ukikatwa tatizo linarudi.
 
Mungu niepushe ningekunyaje mie ninavyopenda kunya lol
 
hiyo picha hapo juu rinda limekamata kisawasawa! lolest!
 
Ndugu yangu hili tatizo lipo sana na binafsi nililipata, mwanzoni nilikuja humu nikapata ushauri ila bado halikuisha, kuna dawaitwa Anusol nazo hazisaidii... kiujumla dawa za hospitali haziwezi kukusaidia hii ishu. sijui uko mkoa gani but kama uliko kuna migomba basi maji maji ya kwenye mgomba ndo dawa ya hii kitu.. unakamua yale maji ya kwenye mgomba na kuweka kwenye ******.. ntafufua moja ya threa ambayo ilikua na ushauri mzuri sana kuhusu hii ishu. pole sana mkuu

asante sana wambuzi,loh inanikosesha amani hii hali japo cpati maumivu kwa sasa lakin mwanzo yalikuwepo,ni miez ming imepita niliwah kutumia anasol ya tube,sasa najishaur nitumie ya muundo wa kidonge cha kutumbukiza uko sehemu,nakiri kuwa itakuwa ilisababishwa na ujauzito km mjumbe hapo chini alivoelezea.chondechonde niwekee hiyo thread,au unibainishie khs hayo maji ya mgomba ni part ipi ya mgomba?maana nina migomba hapahapa nyumban.asante
 
Asante bayo,hakika kilichonipata ni kama hiyo picha ilivobainisha,ila hayo matibabu mhm nayaogopa upasuaji tena?hakuna mitishamba unayofahamu?
 
Jaribu kukaa kwenye beseni la maji ya moto(si ya kuunguza lakini moto zaidi ya vuguvugu) asubuhi na jioni baada ya kuoga for 15-20 minutes inaweza saidia. Nilipata tatizo hilo baada ya kujifungua na daktari ndo alinishauri kufanya hivyo na tatizo liliisha. Pia kula vyakula laini ili usijikamue wakati wa kwenda haja kubwa, achana na wali kula viazi, ugali laini, supu, ndizi n.k.
 
Ndugu yangu bwana Solarpanel cheki hii thread kwa ushauri zaidi wa ishu yako boss wangu.. soma kwa makini humu utapatta maelezo ya tiba boss
 
Jaribu kukaa kwenye beseni la maji ya moto(si ya kuunguza lakini moto zaidi ya vuguvugu) asubuhi na jioni baada ya kuoga for 15-20 minutes inaweza saidia. Nilipata tatizo hilo baada ya kujifungua na daktari ndo alinishauri kufanya hivyo na tatizo liliisha. Pia kula vyakula laini ili usijikamue wakati wa kwenda haja kubwa, achana na wali kula viazi, ugali laini, supu, ndizi n.k.

asante
 
Aise kaka Bayo umeelezea vizuri sana kijana cha kufanya asikwambie mtu yeyeote kwenda kutumia miti shamba nenda hospital kafanyiwe operation hata mim ilishawahi kunitokea na nikafanyiwa operation pale Aga Khan hospital.
 
inatibikaje hivi wazee mana nimeskia ipo external na internal, how is it going?

Mimi ninapata kazi kidogo kukuelewa. Misuli imefanyaje sasa mpk itibiwe? Imelegezwa?

Ulikuwa unafanya nini mpk misuli ya uwani ikusumbue?

No, wait! Hili jukwaa gani kwani?
 
Nenda hospitali kamuone Daktari atakufanyia oparesheni ndogo ya Upasuaji wa hivyo Vipele kwenye sehemu zako za siri hiyo ni kawaida tu lakini ukiachia huenda vikazidi na ukapata maradhi makubwa mungu akunusuru fanya upesi kumuona Daktari atakusaidia tu.

Lakini mkuu MziziMkavu, kwa maelezo ya oldd vampire, si kwamba shida yake ni choo?

Manake hata akifanyiwa operesheni na bado choo yake ni ngumu, si atatoka vingine? Mimi maoni yangu ni kutibu choo ngumu ya OV kwa ukwaju may be (nilisikia unatibu). Kama unajua mambo ya ukwaju mpe dozi alainishe choo na hiyo ishu itapotelea mbali
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom