Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Lakini mkuu MziziMkavu, kwa maelezo ya oldd vampire, si kwamba shida yake ni choo?

Manake hata akifanyiwa operesheni na bado choo yake ni ngumu, si atatoka vingine? Mimi maoni yangu ni kutibu choo ngumu ya OV kwa ukwaju may be (nilisikia unatibu). Kama unajua mambo ya ukwaju mpe dozi alainishe choo na hiyo ishu itapotelea mbali
Mkuu Mwana Mtoka Pabaya Matatizo ya kutopata choo mwisho wake ndio hutokea hiyo haemorroids Bawasiri.

UKOSEFU WA KUTOPATA CHOO TIBA YAKE HII HAPA SOMA

UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’

muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya

kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
Last edited by a moderator:
kwanza usipaniki hilo tatizo la vinyama kutokeza sehemu za sili linatibika.kitaalamu hilo tatizo linaitwa <strong>Haemorrhoid.kuna matibabu ya aina kama nne, matibabu ya kwanza ni kwa njia ya kukalia maji ya uvuguvugu yaliyo kwenye beseni.chemsha maji yamimine kwenye beseni yapooze kidogo kwa maji ya baridi ili yasikubabue.kalia maji hayo ya UVUGUVUGU yakiwa kwenye beseni kwa muda wa angalau dakika ishilini,fanya hivyo kutwa mara tatu.ndani ya siku tano mpaka kumi hivyo vinyama vitapotea.matibabu ya aina ya pili ni kwa njia ya LIGATION ni vyema njia hii ukafanyia na mtaalamu wa afya.njia hii vile vinyama vinavyo ning'inia hufungwa na uzi kwenye shina na kukwazwa ili damu isifike sehemu ya chini kitu kitacho sababisha vile vinyama kukatika vyenyewe.matibabu ya tatu ni kwa njia ya kuvikausha hivyo vinyama kwa kutumia sindano.njia ya nne ni upasuaji.Angalizo usivikate hivyo vinyama mwenyewe,pia nakushauli nenda hospitali kwa ushauli zaidi&nbsp;</strong>
 
Habari zenu the great thinkers!
Ninaomba kujua kama kuna dawa ya uvimbe sehemu ya tundu la haja kubwa ambao wakati mwingine husababisha mpaka damu kutoka wakati wa kujisaidia,
chanzo chake ni nini na mwisho wa siku kuna madhara gani makubwa??msaada!
 
Kuna vitu vingine vya ajabu sana, hujui hospitali? Tumia akili ya kawaida, chochote kinachosumbua mwili wako pata ushauri kwa daktari.
 
Hii link itakusaidia kuujua huo ugonjwa "http://www.medicinenet.com/hemorrhoids/article.htm" lakini nakushauri upitia pia jukwaa la JF Doctor mara kwa mara watu wamekuwa wakiileta hii mada.
 
Nenda hospital utapewa dawa ya kuchomeka hapo kila siku.dawa yenyewe ni ndefu ndefu kama uume.
 
chanzo chake ni kuliwa tigo kwa muda mrefu na madhanra yake ni kinyeo kufutuka na utumbo kutoka nje ...na mwisho wake ni kifo kibaya sana
mKUU Yaya Toure hapa si mahali pa kuleta matusi hapa ni mahali pa kupeana mawazo mazuri je unayemjibu naye akikujibu kwa matusi Je utafurahi?Tafadhali usirudie tena kuleta matusi yako hapa. Kama huna cha kumjibu bora uisome Thread na kunyamaza tu inatosha kuliko kuleta maneno ya matusi tafadhali sana.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu Babu mchumi Kwa maelezo yako uliyoyatoa inaonyesha una ugonjwa wa Hemorrhoids Bawasiri angalia hizo picha chini.

Image of External Hemorrhoids

85_320x320.jpg

89_320x320.jpg

Picture of piles or internal hemorrhoids. The image shows the rectum with an internal hemorrhoid exposed. Internal hemorrhoids can be very painful and often burn or itch.

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje:

Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?

Bawasiri husababishwa na;

  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri

  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

Vipimo na uchunguzi

  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy

Njia za kuzuia Bawasiri

  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa. http://www.tanzmed.com/component/k2/item/62-bawasiri-hemorrhoids.html

Last edited by a moderator:
Kuna ugonjwa mwingine unaitwa - Perianal Festula
kama kuna mtaalam wa ugonjwa huu atufafanulie manake unafanana na huo!

Tiba nyingine kwa hospital ni kwa kutumia vidonge vya Annusal Suppossitory na cream ya Annusal Ointment. Pia unaweza kuweka maji ya moto kwenye besini na kuchanganya na chumvi kisha kaa ndani ya beseni kwa dakika kama 15 hv kabla ya kutumia dawa hizo. Kikubwa katika kutibu tatizo la bawasiri ni kuacha vyakula ambavyo vitasababisha kupata choo kigumu, papai ni zuri sana kutumia kwa mtu mwenye tatizo hilo, mboga za majani, maji mengi na ndizi zilizopikwa sana kama mtori.
 
>>Husababisha maumivu wakati wa kujisaidia
>>yanayoendana na kutokwa na damu
>>hali hi hutokea na si lazima iwe ya kuridhi.
>>Vinyama ivi huondoka na tiba inayotokana na mimea ya asili bila operation
>>0713297066-kwa maelezo zaidi

images
 
>>Husababisha maumivu wakati wa kujisaidia
>>yanayoendana na kutokwa na damu
>>hali hi hutokea na si lazima iwe ya kuridhi.
>>Vinyama ivi huondoka na tiba inayotokana na mimea ya asili bila operation
>>071329706-kwa maelezo zaidi

images

sikutii hofu, ni tatizo baya,linadhoofisha,unajisikia sometimes huna nguvu kabisa,halitibiki kirahisi hospitalini, ukitibiwa kwa sindano utaumiza uzima wako,si utani,sijuwi ulipo,lakini wataalam wa tatizo lako wengi wapo Bariadi,wanakomesha kabisa
 
Kuna mtaalam pia hospitali ya wasabato Pasiasi Mwanza, ni Daktari lakini hutumia dawa za kimila,vinginevo nasisitiza, usitumie sindano za hospitali kutibu, wengi hawaponi hapo.kama vipi ni pm, niakudirect sawasawa. Vilevile kuna mtumishi pale halmashauri ya jiji la Mwanza alitibiwa Bariadi unaweza kuwasiliana nae, pm me
 
Vinyama "HEMORRHOIDS".
siku hizi vinatibiwa kienyeji?
Usikute huyo anayetibu hajui anatibu nini na sababu ya tatizo ni nini?
Kila la kheri mnaopenda kutibiwa na local/herbs.
 
Vinyama "HEMORRHOIDS".
siku hizi vinatibiwa kienyeji?
Usikute huyo anayetibu hajui anatibu nini na sababu ya tatizo ni nini?
Kila la kheri mnaopenda kutibiwa na local/herbs.

achana na waganga wa kienyeji na wabongo walivyo wajinga wanakimbilia huko wasijue kadri anavyozidi kuchelewa ndo tatizo linazidi kuwa kubwa. All the best hata babu wa Loliondo alianza hivihivi na matokeo yake mmeyaona
 
Back
Top Bottom