Uhaba wa umeme nchini: Kwanini serikali ya CCM chini ya Marais wao watatu Kikwete, Magufuli na Samia imeshindwa kupata Suluhu ya kudumu?

Mabadiliko ya tabia ya nchi yaliathiri sana hali ya uzalishaji wa umeme katika nchi yetu. Ambapo ukame ulioikumba nchi yetu ulipelekea kina cha maji kushuka chini na hivyo kuathiri uzalishaji wa umeme.mfano bwawa la Mtera lenye uwezo wa kuzalisha megawati 80 lilijikuta likizalisha megawatts 40 tu.

Vivyo hivyo kwa bwawa la kidatu linalopakana pale mkoani Morogoro lenye uwezo wa kuzalisha megawati 204 nalo lilijikuta likishindwa kufikia uwezo wake wa kutoa megawati hizo za umeme.

Hata pale mvua zilipokuwa zimeanza hususan mwishoni kwa mwezi wa kumi na mbili ilikuwa changamoto katika kujaza maji mabwawa haya kwani mikoa tegemeo katika kupokea mvua na kupelekwa katika mabwawa haya ilikuwa ni hafifu na yenye kutawaliwa na vipindi vingi na virefu vya jua japo maeneo mengine ya nchi mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha kwa wingi.

Tatu ni suala la ongezeko kubwa sana tena sana ya shughuli za kiuchumi hapa nchini zinazotegemea Umeme. Ndugu zangu ni kuwa Mheshimiwa mama Samia Suluhu Hasssan mara baada ya kuingia madarakani amefanya kazi kubwa sana ya kuvutia wawekezaji katika Secta mbalimbali hapa nchini ,lakini pia kuongezeka kwa idadi kubwa ya wajasiriamali wanaotumia umeme katika shughuli zao za kiuchumi.

Ninyi wenyewe ni mashahidi kuwa wakati huu wa Rais Samia hakuna kiwanda cha aina yoyote ile kilichofungwa na wawekezaji kutokana na mazingira magumu ya biashara,bali tumeshuhudia shughuli za uwekezaji zikiongezeka sana hapa nchini.hali iliyopelekea na kuchochea ongezeko la mahitaji ya umeme hapa nchini ,wakati kwa kiasi kikubwa tulikuwa tunatumia na kutegemea chanzo kimoja tu cha kuzalisha umeme ambao ni umeme wa maji.

Lakini pia kumekuwa na ongezeko ya mikoa ambayo hapo awali ilikuwa haijaunganishwa katika grid ya Taifa ,ambapo mara baada ya kuingia madarakani kwa mama wa shoka , chuma cha reli na jasiri muongoza njia mama Samia Suluhu Hasssan aliunganisha mikoa hiyo katika grid ya Taifa na hivyo kuongeza mahitaji ya umeme kwa kiasi kikubwa wakati vyanzo vya kuzalisha umeme vilibaki kuwa vile vile

Hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na Changamoto hii ya umeme ni pamoja na kufanya mchakamchaka katika kukamilisha ujenzi wa bwawa la mwalimu Nyerere ambalo litatupatia megawati 2115 pale litakapokuwa limekamilika.na kwa sasa lipo katika hatua za mwisho kabisa katika kuanza kuzalisha umeme kwa kuwasha mtambo wa kwanza ambao muda siyo mrefu utawashwa.

Pili ni kutumia umeme wa gas.ambapo serikali yetu imejaribu kutumia nakizalisha umeme unaotokana na gas ili kuongeza megawati ambazo zimekuwa zikiunganishwa katika grid ya Taifa..

Nitaendelea kutoa majibu mengine .ngoja niishie hapa kwanza ili andiko lisiwe refu sana.
Katika kipindi cha utawala wake ndio huo ukame umetokea na kuleta shida kwenye uzalishaji umeme, lakini pia katika kipindi chake ndio mafuta yakapanda bei duniani na kufanya gharama za maisha kuwa juu.

Ni laana, gundu au bahati mbaya tu?
 
bila shaka Wewe ulipokuwa mdogo uliugua ugonjwa wa utapia mlo uliosababishwa na kula sana ugari !!!
akili yako imeishia hapo kwenye umeme wa maji miaka 50 + madarakani??? mvua isiponyesha TANZANIA haitapata umeme????
 
Kwa ujumla hizi ndizo sababu ambazo utawala na CCM unazitoa miaka yote tangu Mkapa na Kikwete.

Hayati Rais John P. Magufuli, alizikataa na kuja na namna nyingine ya kufikiri.

Cha ajabu wewe (bila shaka kwa ujinga tu) umekubali kulishwa na kuziimba kama chorus ya wimbo ambao wasikilizaji umeshawakinai.

Hizi hatutaki kuzisikia!!

Hamna akili ya kulijua hili? Ina maana CCM hamna akili ya kujua haya kabla na kuja mbadala (alternative)? Hiyo climate change iko na kuiathiri Tanganyika pekee?

Hebu fikiri vizuri!

CCM na serikali yenu hamkujua haya? Akili na ufahamu umefungwa katika njia hizi tu za uzalishaji umeme?

Hili tatizo ni la miaka na miaka (miongo 3 sasa), yaani zaidi ya miaka 35 na linadumu hata sasa. Halikuanza mwaka jana km unavyojaribu kusema hapa. Bila shaka CCM hawana akili na maarifa zaidi ya hapa unavyofikiri wewe. Wamechoka na wanapaswa kuondoka kwenye viti vya mamlaka na maamuzi!

Lakini pia kumekuwa na ongezeko ya mikoa ambayo hapo awali ilikuwa haijaunganishwa katika grid ya Taifa ,ambapo mara baada ya kuingia madarakani kwa mama wa shoka , chuma cha reli na jasiri muongoza njia mama Samia Suluhu Hasssan aliunganisha mikoa hiyo katika grid ya Taifa na hivyo kuongeza mahitaji ya umeme kwa kiasi kikubwa wakati vyanzo vya kuzalisha vikiwa vilevile bila kuongezeka
Hivi Lucas mwashambwa, unaelewa maana ya nchi kuwa na mipango ya muda mfupi na mrefu?

Unaelewa kwanini huwa tuna sensa kila baada ya miaka 10?

Je, si ni ili ku - project mahitaji ya nchi na watu ya miaka 5, 10 na hata 50 ijayo ktk kila sekta ya kijamii na kiuchumi kwa kigezo cha ongezeko la watu (population) na shughuli zao za kiuchumi?

Sasa unapotaja sababu za ongezo la watu, shughuli za kiuchumi na kuongezeka mikoa unakuwa unafikiri nini? Je, si unathibitisha tu kuwa huko CCM hakuna watu wenye akili za kufikiri na wakati wote mnawaza kupiga propaganda za kisiasa zenye malengo kulinda utawala na mamlaka ya serikali hii chini ya CCM isiyo na manufaa tena kwa nchi na wananchi
Hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na Changamoto hii ya umeme ni pamoja na kufanya mchakamchaka katika kukamilisha ujenzi wa bwawa la mwalimu Nyerere ambalo litatupatia megawati 2115 pale litakapokuwa limekamilika.na kwa sasa lipo katika hatua za mwisho kabisa katika kuanza kuzalisha umeme kwa kuwasha mtambo wa kwanza ambao muda siyo mrefu utawashwa.
Sawa.

Huu ulikuwa mpango wa muda mrefu wa Hayati Rais Magufuli. Huyu mama yako ambaye badala kukaa ofisini kuumiza kichwa kufikiri namna atakavyokabiliana na changamoto zinazoikabili nchi, yeye Yuko bize kukata mitaa huko duniani na kufanya sherehe ya kuzaliwa (birthday) kwake. Hivi kwa kiongozi mwenye uchungu na mzalendo wa nchi yake atakuwa ana furaha gani ya kusheherekea huku nchi na watu wake wakiwa kwenye shida nyingi ikiwemo hii ya umeme?
Pili ni kutumia umeme wa gas.ambapo serikali yetu imejaribu kutumia nakizalisha umeme unaotokana na gas ili kuongeza megawati ambazo zimekuwa zikiunganishwa katika grid ya Taifa..
Uko wapi huo umeme wa gas? Kwanini Kuna uhaba na mgawo kama upo? Si CCM iliumiza na kuua watu miaka ya Jakaya Kikwete Ili kuanzisha mradi huu miaka karibu 20 iliyopita kwa ahadi kuwa anakwenda kutatua tatizo la umeme nchini na kubaki kuwa historia?

Badala yake kukatokea nini? Ni uongo na shida hiyohiyo Iko mpaka Sasa? Wewe unadhani ni kwanini?
Nitaendelea kutoa majibu mengine .ngoja niishie hapa kwanza ili andiko lisiwe refu sana.
Hatuhitaji propaganda. Huna lolote unaloweza kujibu zaidi ya drama za miaka yote.

Jibu ni hili: Akili iliyotengeneza tatizo la umeme nchi hii, haiwezi kuwa akili hiyohiyo inayoweza kutatua tatizo hilo!!
 
Wakati Magu analeta suluhisho mlimsimanga mkamuita mshamba hana exposure. Bwawa aliloliacha mnalihujumu makusudi ili muuze solar na majenereta ya kutosha
 
bila shaka Wewe ulipokuwa mdogo uliugua ugonjwa wa utapia mlo uliosababishwa na kula sana ugari !!!
akili yako imeishia hapo kwenye umeme wa maji miaka 50 + madarakani??? mvua isiponyesha TANZANIA haitapata umeme????
Huyu Lucas mwashambwa, ni kijana mjinga na mpumbavu fulani. Hakana hoja. Ni kapiga propaganda tu ktk maswala serious yanayohitaji akili kufikiri kabla ya kuandika au kusema.

Vyeo vya madaraka vinatafutwa kwa nguvu zote ikiwemo kutumia matatizo ya wengine kujipatia uteuzi.

Haka kadogo Lucas mwashambwa, kameshajitoa ufahamu na akili kusema na kuandika chochote Ili mradi kinawa - please wakubwa zake kwa matatajio ya kupata upendeleo (favour).
 
Wakati Magu analeta suluhisho mlimsimanga mkamuita mshamba hana exposure. Bwawa aliloliacha mnalihujumu makusudi ili muuze solar na majenereta ya kutosha
Hatukumtuma ateke watu bwana wee! Sasa Umeme aliweza?
 
Wakati Magu analeta suluhisho mlimsimanga mkamuita mshamba hana exposure. Bwawa aliloliacha mnalihujumu makusudi ili muuze solar na majenereta ya kutosha
CCM hao, bila shaka. Au siyo?

Yes, The late John P. Magufuli was a good and a great leader

However, it's an undeniable fact pia kuwa, ana upande wa mabaya mengi.

Elements za ushamba alikuwa nazo. Kukosa exposure lilikuwa tatizo pia. Mbaya zaidi, hakuwa tayari kujikosoa na kujifunza toka kwa wenzake. He was a selfish leader.

He absolutely believed in himself alone na ndio maana akafa kifo cha kizembe kabisa akiwa Rais wa nchi.

Hata hivyo, hatupaswi kumlaumu Magufuli. Tulaumu mfumo mbovu wa kisheria na kikatiba unaotengeneza mtu kutawala nchi badala ya taasisi imara.

Laiti kama tungekuwa na taasisi imara za kikatiba, zingemtengeneza Rais Magufuli na kuwa the best president ever kuwahi kutokea Tanzania na angekuwa hai mpaka leo!!
 
Kwa ujumla hizi ndizo sababu ambazo utawala na CCM unazitoa miaka yote tangu Mkapa na Kikwete.

Hayati Rais John P. Magufuli, alizikataa na kuja na namna nyingine ya kufikiri.

Cha ajabu wewe (bila shaka kwa ujinga tu) umekubali kulishwa na kuziimba kama chorus ya wimbo ambao wasikilizaji umeshawakinai.

Hizi hatutaki kuzisikia!!

Hamna akili ya kulijua hili? Ina maana CCM hamna akili ya kujua haya kabla na kuja mbadala (alternative)? Hiyo climate change iko na kuiathiri Tanganyika pekee?

Hebu fikiri vizuri!

CCM na serikali yenu hamkujua haya? Akili na ufahamu umefungwa katika njia hizi tu za uzalishaji umeme?

Hili tatizo ni la miaka na miaka (miongo 3 sasa), yaani zaidi ya miaka 35 na linadumu hata sasa. Halikuanza mwaka jana km unavyojaribu kusema hapa. Bila shaka CCM hawana akili na maarifa zaidi ya hapa unavyofikiri wewe. Wamechoka na wanapaswa kuondoka kwenye viti vya mamlaka na maamuzi!

Hivi Lucas mwashambwa, unaelewa maana ya nchi kuwa na mipango ya muda mfupi na mrefu?

Unaelewa kwanini huwa tuna sensa kila baada ya miaka 10?

Je, si ni ili ku - project mahitaji ya nchi na watu ya miaka 5, 10 na hata 50 ijayo ktk kila sekta ya kijamii na kiuchumi kwa kigezo cha ongezeko la watu (population) na shughuli zao za kiuchumi?

Sasa unapotaja sababu za ongezo la watu, shughuli za kiuchumi na kuongezeka mikoa unakuwa unafikiri nini? Je, si unathibitisha tu kuwa huko CCM hakuna watu wenye akili za kufikiri na wakati wote mnawaza kupiga propaganda za kisiasa zenye malengo kulinda utawala na mamlaka ya serikali hii chini ya CCM isiyo na manufaa tena kwa nchi na wananchi

Sawa.

Huu ulikuwa mpango wa muda mrefu wa Hayati Rais Magufuli. Huyu mama yako ambaye badala kukaa ofisini kuumiza kichwa kufikiri namna atakavyokabiliana na changamoto zinazoikabili nchi, yeye Yuko bize kukata mitaa huko duniani na kufanya sherehe ya kuzaliwa (birthday) kwake. Hivi kwa kiongozi mwenye uchungu na mzalendo wa nchi yake atakuwa ana furaha gani ya kusheherekea huku nchi na watu wake wakiwa kwenye shida nyingi ikiwemo hii ya umeme?

Uko wapi huo umeme wa gas? Kwanini Kuna uhaba na mgawo kama upo? Si CCM iliumiza na kuua watu miaka ya Jakaya Kikwete Ili kuanzisha mradi huu miaka karibu 20 iliyopita kwa ahadi kuwa anakwenda kutatua tatizo la umeme nchini na kubaki kuwa historia?

Badala yake kukatokea nini? Ni uongo na shida hiyohiyo Iko mpaka Sasa? Wewe unadhani ni kwanini?

Hatuhitaji propaganda. Huna lolote unaloweza kujibu zaidi ya drama za miaka yote.

Jibu ni hili: Akili iliyotengeneza tatizo la umeme nchi hii, haiwezi kuwa akili hiyohiyo inayoweza kutatua tatizo hilo!!
Umemjibu vyema sana...

Nilitaka kuongea Lakini ni kama umemaliza..

Nashangaa mpaka sasa hajaja kujibu hoja hizi..

Hello Lucas mwashambwa njoo ujibu huku
 
1. Tatizo lilianza seriously wakati wa utawala wa Jakaya Kikwete (2005 - 2015). Alijaribu kulitatua lakini serikali yake haikuwa na nia ya kutatua bali viongozi wa serikali kutumia tatizo hilo kufanya ufisadi ili kuiba pesa ya umma tu. Rejea kashfa ya Richmond.

2. Tatizo hili limedumu kwa miongo mitatu na ushee sasa. Lugha na staili ya kulitatua ni ileile ambayo mtu makini akichunguza hataona nia ya kweli ya kutatua zaidi ya viongozi wa serikali kutumia tatizo hilo kama fursa ya kupiga pesa (kufanya ufisadi) huku nchi na wananchi wakitaabika Kwa uchumi wao mdogo kujeruhiwa na wengine kufa kabisa..

Haiwezekani tatizo dogo kama hili la umeme lidumu kwa zaidi ya miaka 35 huku serikali kongwe ya CCM ikiwa madarakani kwa miaka 63+ tangu 1961 ikiwa imeshindwa kupata ufumbuzi wa kudumu kiasi cha watu kujiuliza wanafanya nini ofisini kama hawatumii vichwa vyao vyema kufikiri?

Swali kuu la kujiuliza ni; Je, ina maana nchi hii haina watu wenye akili wanaoweza kufikiri vyema na kuja na Suluhu ya kudumu kuondoa tatizo hili? Kama wapo, kikwazo ni nini?

Hebu nyie chawa wa mama, wana CCM kindandaki kina Lucas mwashambwa, Paul Makonda, ChoiceVariable chiembe, FaizaFoxy, MamaSamia2025, Tlaatlaah Pascal Mayalla na wengine hebu tupeni maelezo tuwaelewe..!!

3. Wakati wa utawala John P. Magufuli (2015 - mwanzoni mwa 2021), kulikuwa na mwanga kidogo wa uelekeo kutatuliwa kwa changamoto hii. Huyu Mzee alianzisha mradi mkubwa wa kujenga bwawa la kuzalisha umeme ktk maporomoko ya Stigler Gorge yaliyopo katika mto Rufiji mkoa wa Pwani. Mradi huo umepewa jina Julius Kambarage Nyerere Hydro Electric Power Station (JKNHP)..

4. Pamoja na kuanzishwa kwa mradi huu, wakati wote wa u - Rais wa John P. Magufuli (2015 - 2021), hakukuwa na mgawo wa umeme kabisa ulio rasmi nchi nzima na kiasi cha kudumu kwa muda mrefu. Kama kulikuwa na kukatika umeme, basi ilikuwa ni kwa sbb za kiufundi na kwa muda mfupi tu..

John P. Magufuli alikuwa na ubaya wake. Lakini ktk eneo hili pamoja uchumi alifanya vyema sana. Mimi nampa maua yake[emoji257][emoji257][emoji257]huko alikohifadhiwa...

5. Cha kushangaza, Mara baada ya kifo Cha Magufuli na nchi kutwaliwa na Makamu wake kikatiba, ghafla everything turned upside down. Maisha yakawa magumu. Thamani ya shilingi ikaporomoka kwa kasi. Mafuta ya petrol yakapaa kupita kiasi ktk muda mfupi sana ikiwemo kuadimika. Ghafla tatizo la umeme likaanza na linadumu hadi sasa..

Tunajiuliza kulikoni? Mbona lilishatatuliwa na Rais Magufuli imekuwaje ghafla linaanza tena? Bila shaka huu ni mchezo mbaya wa serikali kuhujumu wananchi wake wenyewe..!

Cha kushangaza ni kuwa huyu Rais anaonesha wazi kuwa hajali na hajui taabu wanayokumbana nayo wananchi. Yuko bize kukata mitaa huko duniani. Ameshindwa kabisa kuonesha uongozi katika haya. Madume aliyoyateua mwenyewe yanatumia udhaifu wake wa kuwa mwanamke kumhujumu. Yakitaka kuiba, yanampangia safari kwenda ughaibuni kutembea. Kuna siku yatampangia ziara kwenda Somalia kuomba msaada[emoji849][emoji848] ili mradi tu yapate mwanya wa kupiga..!

Tunataka serikali ituambie shida ya hii kitu iko wapi? Mbona tatizo ni la miongo zaidi ya mitatu? Kama CCM mmeshindwa kutatua, mnafanya nini kwenye ikulu yetu???
Waache waendelee na upigaji!
Si uneona kule maeneo ya Tabora Jana jamaa mmoja anajidadavua anajua sana kuliko mTanzania yeyote akiwaambia watu wawashe touching za simu zao ili alone mwanga aendelee na mkutano kuwahadaa matatizo ya wananchi wake.
Akili hovyo.
 
Back
Top Bottom