Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Katika kipindi cha utawala wake ndio huo ukame umetokea na kuleta shida kwenye uzalishaji umeme, lakini pia katika kipindi chake ndio mafuta yakapanda bei duniani na kufanya gharama za maisha kuwa juu.Mabadiliko ya tabia ya nchi yaliathiri sana hali ya uzalishaji wa umeme katika nchi yetu. Ambapo ukame ulioikumba nchi yetu ulipelekea kina cha maji kushuka chini na hivyo kuathiri uzalishaji wa umeme.mfano bwawa la Mtera lenye uwezo wa kuzalisha megawati 80 lilijikuta likizalisha megawatts 40 tu.
Vivyo hivyo kwa bwawa la kidatu linalopakana pale mkoani Morogoro lenye uwezo wa kuzalisha megawati 204 nalo lilijikuta likishindwa kufikia uwezo wake wa kutoa megawati hizo za umeme.
Hata pale mvua zilipokuwa zimeanza hususan mwishoni kwa mwezi wa kumi na mbili ilikuwa changamoto katika kujaza maji mabwawa haya kwani mikoa tegemeo katika kupokea mvua na kupelekwa katika mabwawa haya ilikuwa ni hafifu na yenye kutawaliwa na vipindi vingi na virefu vya jua japo maeneo mengine ya nchi mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha kwa wingi.
Tatu ni suala la ongezeko kubwa sana tena sana ya shughuli za kiuchumi hapa nchini zinazotegemea Umeme. Ndugu zangu ni kuwa Mheshimiwa mama Samia Suluhu Hasssan mara baada ya kuingia madarakani amefanya kazi kubwa sana ya kuvutia wawekezaji katika Secta mbalimbali hapa nchini ,lakini pia kuongezeka kwa idadi kubwa ya wajasiriamali wanaotumia umeme katika shughuli zao za kiuchumi.
Ninyi wenyewe ni mashahidi kuwa wakati huu wa Rais Samia hakuna kiwanda cha aina yoyote ile kilichofungwa na wawekezaji kutokana na mazingira magumu ya biashara,bali tumeshuhudia shughuli za uwekezaji zikiongezeka sana hapa nchini.hali iliyopelekea na kuchochea ongezeko la mahitaji ya umeme hapa nchini ,wakati kwa kiasi kikubwa tulikuwa tunatumia na kutegemea chanzo kimoja tu cha kuzalisha umeme ambao ni umeme wa maji.
Lakini pia kumekuwa na ongezeko ya mikoa ambayo hapo awali ilikuwa haijaunganishwa katika grid ya Taifa ,ambapo mara baada ya kuingia madarakani kwa mama wa shoka , chuma cha reli na jasiri muongoza njia mama Samia Suluhu Hasssan aliunganisha mikoa hiyo katika grid ya Taifa na hivyo kuongeza mahitaji ya umeme kwa kiasi kikubwa wakati vyanzo vya kuzalisha umeme vilibaki kuwa vile vile
Hatua zilizochukuliwa na serikali yetu kukabiliana na Changamoto hii ya umeme ni pamoja na kufanya mchakamchaka katika kukamilisha ujenzi wa bwawa la mwalimu Nyerere ambalo litatupatia megawati 2115 pale litakapokuwa limekamilika.na kwa sasa lipo katika hatua za mwisho kabisa katika kuanza kuzalisha umeme kwa kuwasha mtambo wa kwanza ambao muda siyo mrefu utawashwa.
Pili ni kutumia umeme wa gas.ambapo serikali yetu imejaribu kutumia nakizalisha umeme unaotokana na gas ili kuongeza megawati ambazo zimekuwa zikiunganishwa katika grid ya Taifa..
Nitaendelea kutoa majibu mengine .ngoja niishie hapa kwanza ili andiko lisiwe refu sana.
Ni laana, gundu au bahati mbaya tu?