Uhalisia wa mahusiano mengi ya kimapenzi unatisha, wanaume tuwe macho

Uhalisia wa mahusiano mengi ya kimapenzi unatisha, wanaume tuwe macho

Nina dogo mmoja hapa. Alikuwa na pisi yake hivi kutoka familia ya kishua shua hivi. Walikutana kwenye kozi fulani hivi ya mwaka mmoja. Hakuwa na malengo nayo wala nini isipokuwa tu kuchovya na kusonga mbele kama injili.

Miezi mitatu akajitokeza jamaa hivi anazo. Ndinga kali na madoido kibao. Mahari tu akamwaga milioni 15 cash. Binti akaolewa. Akafunguliwa na mduka mkubwa wa vipodozi jumla ili asikae tu nyumbani. Jamaa karudi kwenye mishe zake Dubai; na huwa anakuja kwa mwezi angalau mara moja au mbili.

Sasa binti anahaha kishenzi. Anasema hana hisia na huyu mumewe hata tone. Eti hata akilala naye anajikaza lakini kimsingi ni kama anabakwa tu kihisia. Wiki jana kaja Dar kupokea mizigo kutoka China. Siku 4 wana huyu dogo wamejifungia lodge dogo anapeleka moto. Binti anamlazimisha dogo ampige angalau mimba maana kuzaa na huyo mumewe wa Dubai anasema itakuwa disaster.

Dogo kaniomba ushauri nikamchana kuwa kwa vile binti ameolewa basi aachane naye mazima. Dogo akasema binti hataki katakata na amesema atakuwa anakuja Dar japo kwa mwezi mara mbili mpaka atakapopata mimba. Dogo anapewa hela kweli kweli. Yaani kutumiwa milioni 1+ ya kutumia siyo ishu. Eti oooh leo unataka ule nini mume wangu? Chukua hii laki moja ule kitimoto leo.

Mwanamke ni kiumbe wa hisia aisee na kama hana hisia na wewe hata uwe na hela kumzidi Elon Musk ni kazi bure. Hata umpe dunia nzima kama hakupendi anaweza akaishi na wewe lakini hisia zake ziko kwingine. Na hapo ni lazima ujiandae kulea watoto ambao sio wako!
Aisee 🤔
 
Mimi ni Faraja Mdeya kwenye comments hapo nipo live kabisa 😂
panajaa kwa hasira ila wanawake ni hatari sana kikubwa na cha muhimu kwa sisi wanaume ni kutokujimaliza. Unaplay part yako kwa kiasi ukijimaliza likitokea la kutokea unaweza wehuka.
 
Back
Top Bottom