Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Yaani mpaka aibu. Dunia ya leo passport imekuwa ni kitu cha kawaida lakini sio Tanzania. Tena huyo jamaa anatamba kabisa.
Inasikitisha, tupo nyuma sana.
 
Nilishaacha kufuata habari za uhamiaji tanzania, nikitaka natumia shortcut mchezo umeisha. Hao uhamiaji ni taasisi naichukia kuliko zote tanzania, wanaendesha kizamani sana. One day hao wazee wataondok kitakuja kizazi kingine hapo uhamiaji na milango itafunguka.

Uhamiaji wanaongeza umasikini tanzania kwa kuwanyima raia wake passport. Yaani kama unataka kwenda kufundisha kiswahili afrika kusini unaanza kuhangaika nao tena badala ya wao kuweka mazingira mazuri kwa kila mtanzania.
 
Hayo maswali ya unaenda wapi kwa sababu gani uhamiaji manchi mengi walishayaacha nchi kama Kenya,Uganda na Rwamda hawauñizi.Hayo sio madwali ya uhamiaji kuuliza ni ya ubalozi mtu anokoenda kuomba visa.Eamejiongexea kazi isiyo na sababu.Uhamiaji wao ni kama NIDA wao watoe passport .Mtu ukimpa passport sio kuwa ndio safari kapata .Hayo maswali a anaenda nchi ya watu kufanya nini wawachie mabalozi wa nchi husika.Mwenye passport atakutana nayo akienda kuomba visa
 
kwa hiyo kwa uelewa wako passport inahitajika kwa ajili ya kusafiri tu? Pole

Iko haja kitengo cha passport wazee wote wastaafishwe au watumbuliwe wawekwe vijana
Nitajie matumizi mengine ya passport mbali na kusafiri!?.. (Kama hujawahi safiri nchi nyingine utanijibu hutumika Kama kitambulisho).
 
Uhamiaji ukiwauliza mbona mnakuwa wazito kutoa passport kwa kila anayetaka wanajwambia ohhhh mtu aweza kwenda kufanya uhalifu nje !!!

Wabasahau kuwa Kule pia Kuna serikali,Polisi na mahakamani pia atashughulikiwa akikosea huko huko

Kwa hiyo uhamiaji mumejibebesha jukumu.la Polisi na mahakama ya dunia uwiii mbavu zangui Mimi.Hamuamini nchi zingine kuwa Ziko vizuri kupambana na wahalifu?

Mambo ya kimataifa yanatakiwa kuaminiana Mfano wewe umempa mtu passport anaenda marekani.Wewe hujampa Visa ya kuingia Marekani unaogopa Nini?

Wao ndio waliompa baada ya kujiridhisha wenyewe kuwa Ni mtu Safi.Sasa akiuza bangi kule wewe yanakuhusu Nini wewe hukumpa visa .Hata ukihojiwa unasema Mimi nilitoa passport sio visa
Lakini ukijitia ohhh mimi najua aliniambia anakuja huko na ushahidi fomu hii hapa aliyojaza Ina maana akidakwa na madawa ya kulevya wewe ndio mbeba lawama Kama facilitator kwa kukiri Mwenyewe


Nchi nyingi Wana avoid Hilo kuepuka
Hilo.Wewe toa passport usiulize anaenda nchi gani kufanya Nini sukumia Risk ubalozi unaotoa Visa
 
Sasa utaombaje passport kama huna matumizi nayo?

Si unakua na mpango wa safari ndio unatafuta passport!? Au nakosea ndugu zangu😃😃😃😃
Acha ujinga,kama hujui lolote bora ukae kimya na usubiri wengine wachangie!Mfano kuna mitihani ya IELTS,hii huwezi kufanya bila kuwa na passport!Mitihani hii ni ya lugha ya kiingereza na vyuo vingi vya ughaibuni hutaka ambatanisho la grade ya mtihani huo wakati wa application!
Miaka ya nyuma ilinibidi nimtumie mtu aliye nje ya nchi anipe mualiko ili niambatanishe kama kusudio la safari ilimradi nipate passport ili nikaitumie kufanya huo mtihani wa IELTS pale british council!
Pia ukiwa unaapply vyuo vya nje,kuna sehemu lazima ujaze namba ya pasi ya kusafiria!
 
Baadhi ni hizi hapa


kuombea scholarship

kuombea kazi online

kufanya mitihani ya kimataifa online

kuomba tenda online lazima personal particulars za passport ujaze
Nasisitiza passport ni kwa ajili ya kusafiria tu, yote uliyoorodhesha details za passport zinahitajika endapo inabidi kusafiri kwenda huko, sema tulizoea kutumia passport sababu hatukuwa na kitambulisho kingine rasmi. Muulize mtu yeyote nchi yoyote hata ulaya matumizi ya passport ni kwa ajili ya kusafiria tu. Mifano uliyotoa inaendana na kusafiri Kama scholarship ya kusoma Uk, uhamiaji unawapelekea forms za kuombea scholarship wanabaki na kopi. Swala linarudi palepale lazima uwe na sababu kuomba passport. Huwezi kuwa unaomba scholarship ya chuo cha mzumbe ukahitaji passport. Logic!?..
 
Miaka yote tangu uhuru mbona tumeenda vizuri tu?shida imetokea wapi mpaka sasa hivi kuwa na pasi ya kusafiria kuwe kugumu?

Hii naifananisha na lile tamko lililotolewa na waziri fulani miaka ya nyuma pale alipotangaza kupandisha ushuru mara dudu kwa yeyote atakayeingiza gari used toka nje ya nchi
 
Naongelea kuomba scholarship.vyuo.vya nje ya nchi.Sasa fomu ya kuomba scholarship inakutaka ujaze passport number na hiyo fomu iko online .Unaambiwa kalete ushahidi kuwa unasafiri ili tukupe passport .Mimi sisafiri niko kwenye computer nyumbani naomba vyuo mbalimbali scholarship online wanataka namba ya passport sisafiri niko kwenye computer au huelewii maana ya online?


Pili naomba kazi nje ya nchi online najaza taarifa zangu kwenye maombi wanataka kila mwombaji aambatanishe taarifa za passport .Hiyp safari sijapata ndio tu nipo online nahangaika kuomba kazi mtandaoni wewe nikija kuomba passport unaanza kuniambia kalete barua ya mwaliko na ushahidi unaenda nchi gani hivi unaona uko sawa hapo?

Ninacholiona ni uelewa mdogo wa maafisa passport ndio maana naiomba wizara ya teknologia ituondolee aibu ya huu uelewa mdogo wa maafisa passport.Kuwa kuna mabadiliko mengi lakini wao bado wanashilia masharti ya kutoa pasport ya miaka ya Tanzania toka ipate uhuru !!!
 
Sisi tunatafuta scholarships, kwenye Application wanataka namba za passport.. itakuaje
Ukiashafanya application ukipewa form inataka uandike namba ya passport unachukua hizo application form unaenda uhamiaji kuomba passport ili upate namba yako ujaze.
 
Vipi kama unapata dharura kama kwenda na mgonjwa nje ya nchi kwa matibabu na huna passport?Iweje pasi ya kusafiria ionekane kama anasa?Kila mtu mwenye uwezo anapaswa kuwa nayo kwa ajili ya dharura!
 
Back
Top Bottom