Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Sasa mtu kama Mshana Jr anasafiri na ungo kutoka Msata hadi Commoro usiku na kurudi
Watamwambia aonyeshe tiketi?😁
 
Ndio ukifika hiyo stage ukaombe uone kama utaikosa.... sioni kama kuna kunyimwa passport, ni utaratibu tuu
Halafu mrangi kwani yako imesha eksipaya!?

Passport ni haki ya kila raia Halali kama kilivyo kitambulisho cha uraia!

Short of that Is just bureaucracy!
 
Kama huna matumizi nayo usiombe , tumia National ID kufanya mambo yako.
 
Sasa utaombaje passport kama huna matumizi nayo?

Si unakua na mpango wa safari ndio unatafuta passport!? Au nakosea ndugu zangu[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Mama D, inaenda zaidi ya hapo. Wanataka barua kuthibitisha unachoenda kufanya na hata ukitoa - si lazima wakupatie passport. Ukisema unaenda kutibiwa wataka barua ya rufaa kuthibitisha huwezi kutibiwa hapa. Vipi kama anayeenda kukusaidia matibabu ni ndugu anayekaa nje?? Ukisema umepata kazi huko ndio kabisaaaa - wanataka contract!!

Ninafahamu nchi ambazo hutoa passport wakilinganisha na vitambulisho vya taifa kwetu - ni kwa sababu passport haikupi wema au ubaya, haiwezi ikakuokoa au kukufungisha. Ni kitambulisho kinachokupa uwezo wa kutafuta opportunities popote zilipo duniani!
 
Ushamba gani???? Umetaka pasport ukiwa na safari ukaikosa?
Serikali imekupunguzia mzigo wa kuwa na vitu usivyo na matumizi yake... pata safari upewe pasport

If only kila jambo lingesubiri dharura ndio uweze kulipata then even vifaa/ silaha vya / za vita vingesubiri dharura!

Arming your citizens with uncertainty is as much wise as vaccinations before diseases!
 
Hawa nyau kuna siku watasema sisi ambao hatuna magari hatutakiwi kuwa na leseni.

Sifahamu utaratibu kwa nchi nyingine upo vipi juu ya passport ila huu wa lazima uwe na safari haupo sawa. Kuna watu wanatafuta kazi au scholarship na zote hizo wanaitaji passport ID ndio uwe kuwa sehemu ya ombi lako kufanyiwa kazi. Sasa sijui wanasaidia vipi watu wa aina hii!!! Ni kweli hawa maboss wa uhamiaji hawawezi kujiuswali jepesi kama ilo na kujijibu then watengeneze sera ya maana au wanafanya makusudi tu.
Kiasi kwamba niliposikia taarifa kutoka uhamiaji; nikajua wameona ni vyema kuondoa huo utaratibu ili iwe rahisi kwa kila mtanzania kupata pasi ya kusafiria. Kumbe ndio wameamua kugongelea msumari kabisa kautaratibu hako ambako binafsi naona kama vile kanakinzana na haki ya kuwa na pasi ya kusafiria kwa kila raia wa Tanzania.

Hivi kwani wanavyodhani wao mtu anaweza kutoa pesa yake Tshs. 150,000/- bila kuwa na fikra au mpango wa mbele wa safari? Kinachofanyika ni mtu anaamua kufanya maandalizi ya awali ili kurahisisha safari zake huko mbeleni ikiwa ni pamoja na kupunguza mizunguko ya safari.

Watendaji wa serikali jikiteni katika kuona namna ya kumrahisishia raia wa Tanzania mambo badala ya kila siku kuja na mambo ambayo yanamkatisha tamaa huyu raia daaaah, mpaka tunajiuliza hivi lengo la hii serikali ni nini hasa mbona kila kitu kinawekewa mazingira magumu tu iwe ni mawasiliano kila siku sheria ngumu tu iwe ni umiliki wa biashara mazingira badala ya kurahisishwa unaletewa sera na sheria ngumu ngumu tu. Ndio maana wananchi wanakosa furaha na serikali yao. Fikirieni zaidi sio mpaka rais aje aibuke na kulitolea tamko
 
Sasa hii ni pass yangu ya tano. Na utaratibu ninao tumia ndio huo. Lazima kuonyesha kusufio la safari au tiketi ndio upewe passport.
Kwamba kila unaposafiri unapewa pasi mpya au sijakuelewa ?
 
Dada sky hii ni hadithi au based on true story?
Hiyo ni false story kwa sababu nyingi tu lakini moja kama chizi aliweza kupata Passport na nauli kwenda Ulaya ndugu wenye akili timamu walishindwa nini, pili Wazungu hawaziki kwa sababu Ardhi ni ghali sana kwa hiyo ni rahisi kuchoma maiti na ndugu wakapewa majivu kwenye kopo.
 
Si kweli , kama huo ndio utaratibu tangazo hili la nini ?
Huo sasa ubishi tu. Labda iwe ni msisitizo lakini hicho kipengele kwenye application kipo siku zote. Labda uniambie tajiri, bado haumiliki pasipoti.
 
Huo sasa ubishi tu. Labda iwe ni msisitizo lakini hicho kipengele kwenye application kipo siku zote. Labda uniambie tajiri, bado haumiliki pasipoti.
Katika kuomba passport mpya sikuwahi kuzingatia vitu vingine zaidi ya kupata passport tu , sasa sijui kwa vile wananijua kuwa ni msafiri wa mara kwa mara au la .
 
Pasi ya kusafiria sio kitambulisho kusema mtu achukue abaki nayo ndani ni lazima kuwe na dhumuni la safari, kama hauna safari hatuwezi kukupa pasi ya kusafiria
Mawazo ya kikomunisti hayo, passport kiilivyo ni nyaraka kama ID si lazima mtu awe na dhumuni la safari.
 
Itoshe kuwa Passport ni haki ya kila raia kuwa nayo. Yaani mtu apate safari ya hafla aanze kusubirishwa miezi kupata passport? Nchi ina mfumo mbovu huu.

Wanatia hasira pale unapotaka kurenew, details zako zote wanazo, lakini bado unaanza maombi upya kama vile ndio kwanza mara ya kwanza kuomba.
 
Sema umetumia huu mwanya kuwatambia watu kuwa una passport ya nchi nyingine, wala halihusiani na topic iliyo mezani. Hiyo nchi nyingine ni ipi unayoomba passport bila hata kuwa na ushahidi wa kusafiri!?.. taja nchi tukushushie data usilete sifa za kijinga hapa..
Ndio nmetumia vp ume umia?
 
Katika kuomba passport mpya sikuwahi kuzingatia vitu vingine zaidi ya kupata passport tu , sasa sijui kwa vile wananijua kuwa ni msafiri wa mara kwa mara au la .
Lazima ujaze unataka kwenda wapi na hiyo passport hata kama ni fix. Na kama ni ya mtoto lazima supporting document ya lengo la safari..Hata kama ni fix.
Mwisho tajiri, hawakujui kihiiivyo,
 
kwani ukimpa mtu passport akakaa nayo unapungukiwa na nini? Kwani unampa bure?
tanzania pekee ndo tunaona passport NI MALI.nchi nyingi haya mambo hayapo.
Nchi zinazotuzunguka huulizwi unataka passport ya nini utajijua mradi una kitambulisho cha taifa wanakupa


Kifupi passport ni chanzo kizuri.cha uhakika cha kuingiza mapato ya serikali

Wangesema kila mwenye kitambuñisho cha NIDA achukue passport wangepata mabilioni ya pesa ndani ya muda mfupi tu

Passport haitakiwi tu kwa ajili ya safari wamekaa kizamani mno mitihani mingi ya online hutaka uwe na passport kuna sehemu ya kujaza pia ukiomba scholarship online zinataka ujaze passport details pia ukiomba kazi za nje au tenda nje ya nchi online unatakiwa kujaza passport details

Hata ukienda tu british council ukitaka kufanya mitihani yao online kuna sehemu ya kujaza passport details

Hata ukikutana na mwekezaji wa maonyesho ya biashara wanaokuja nchini ukita kuingia ubia naye au biashara atakudai nyaraka za biashara lakini pia lazima umuonyeshe passport yako achukue details


Uhamiaji wako nyuma mno wanadhani psssport kwa sasa unatakiwa kuwa nayo ukiwa na safari tu!!!

Wizara mpya ya teknolojia hebu nenfeni mkawaeleweshe hao uhamiaji kazi ya passport kwenye ulimwengu wa leo wa kidigitali kawapeni semina hawaelewi wako kule enzi za kutaka passport kwa ajili ya safari
 
Wazungu wameshatufungia kwamba tunatoka nchi ambayo haishiriki kwenye vita ya koona, sasa na nyinyi mnatuwekea komeo.....maskini watanzania wanyongeee...
 
Back
Top Bottom