Kuna familia moja ya kisua dada yao mkubwa aliolewa na Mzungu na waliishii Ulaya. Baada ya miaka mingi yule dada alipata saratani. Walimuuguza mpaka mauti yalimfika. Mzungu aliamua mke wake anazikwa Ulaya ili watoto na wajukuu waone kaburi kila wakimkumbuka. Alipiga simu akawaambia anatuma mwaliko wenye passport waende kuomba visa ya kwenda msibani.
Familia nzima hakuna aliyekua na passport kasoro chizi wao mmoja aliyeshindikana. Katika mihangaiko yake alipata pass akaiweka ndani. Siku walizopewa zilikua chache sana ku ku process pass. Mchizi alikua mwanafamilia pekee aliyepata viza na kukwaa pipa kwenda kwenye mazishi ya sister wao.