PreGE2025 Uhasama wa kisiasa Milllard Ayo apoteza wafuasi laki tatu ndani ya masaa 12

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Minard Ayo kafanyaje hadi wamsusie? Juzi kuna Nabii wa nchini Kenya alitoa ushauri kwa Rais na akamwambia afungulie kanisa la Gwajima na asitakebkugombana na Mungu. Pia akasema hakuna mtu anayeweza kuzuia wazo ambalo muda wake umefika!
Na hii ndiyo shida kubwa ya chama changu. Tunapaswa kuona na kukubali kuwa nyakati zimebadilika sana, mbinu za kisiasa tunazotumia ni za karne iliyopita. Tumelewa madaraka na hatuoni hali halisi, ni suala la muda tu na tutashtuka tukiwa tumechelewa.
 
Sasa utamlaumu mtu kama millad ayo kwa kipi watu wanatishwa na yeye ameangaika kuijenga online tv yake kwa miaka..
Ata kama ni wewe ungefanyaje
 
No reforms No election. Na tutauzuia siyo kususia....Nione kimama kinajipendekeza kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi. Kitajuta kuzaliwa!
 
Na hii ndiyo shida kubwa ya chama changu. Tunapaswa kuona na kukubali kuwa nyakati zimebadilika sana, mbinu za kisiasa tunazotumia ni za karne iliyopita. Tumelewa madaraka na hatuoni hali halisi, ni suala la muda tu na tutashtuka tukiwa tumechelewa.
Hapana kwa chama chetu sio swala la mjinu wanazotumia kisaikolojia ukiona mtu yupo teyari kuumiza mtu au ata kuuwa tena bila woga au kuficha ujue huyo mtu amefanya jambo la ovyo hivyo anataka kuficha uchafu wake kwa gharama yyte ile..na kisingizio kikubwa wanasema wanafanya sababu ya uzalendo uzalendo.

Mimi ni ccm ila sikubaliana na yanayoendelea sasa tunafanya mambo mabaya ambayo yanaharibu legacy nzuri aliyoanza nao mama washauri na machawa aliyonao karihu sio watu wanzuri kabisa.
 
Na hii ni dalili kuu ya anguko letu. Tumeshindwa kujifunza toka vyama vingine vikongwe vya Afrika vilivyoanguka bila kutarajia. Tumefikia hatua ya kutaka kubaki madarakani kwa gharama yoyote ile. Kuna mambo yanafanyika dhidi ya watanzania wenzetu yanasikitisha na kutia hasira.
 
Umenikumbusha na Mimi huyu CHAWA wa CCM nikapige tofali
 
Miaka yote chadema wamekuwa wakifanya hivyo ila kwenye uchaguz wanafanyiwa vituko, unyama na mifumo. Kwa nini waendelee na niia hiyo hiyo?

Chadema wana point, bila mabadiliko ya sheria za uchaguz ni sawa na kucheza ngoma ile ile miaka nenda rudi

Chauma na act wana safar ndegu kufikia kukubalika kwa chadema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…