Uhuru Kenyatta taswira ya Rais wa Afrika

Sikiliza, niraisi was taifa gani afrika atakuwa tayari kuikubali hukumu ya mahakama ya kurejea uchaguzi kirahisi tu, ilhali uwezekana wa kuamua kuivunja katiba na kutotii Wala kuipa nafasi mahakama kufanya kazi yake, tuweni wakweli kwetu wenyewe na hata Kwa aliyetuumba. Viwango vya unafiki wa walio watanzania maslahi nafikiri una zidi vile vya shetani.
 
Uhuru Kenyatta? Kabisa?
Nyie watu sijui mna matatizo gani
Hakuna raisi wa ajabu kama Uhuru, Ni mla rushwa na muuaji
Alihonga judges wa the Hague, Ila uhalisia aliua sana na alistahili hukumu.
Yani Kenyatta ali honga hiyo mahakama wewe noma
 
Nyie watu wa ajabu sana yani nyie kila atakae fanya vizuri hamtaki!!..Umewahi kwenda Kenya miaka 15 iliyopita na ukaenda miaka ya hivi karibuni?!!..Umeona utofauti?
 
Peleka uongo wako huko
 

Alikubali? Hakukubali. Alilazimishwa na katiba. Alimtishia jaji mkuu aliyeongoza jopo lililoamua kufuta uchaguzi. Na hakumpa ushirikiano mpaka jaji anamaliza muda wake, Kenyatta aligoma kushirikiana na mhimili wa mahakama kama inavyotakiwa.

Sema taasisi sa Kenya zinajitahidi kusimamia katiba siyo Kenyatta
 
Ukiangali shida ya wakenya ni siasa za ukabila wakati ule, ndio maana hata yeye alilalamika kuhujumiwa ila alikuwa na uwezo wakufanya kama wanavyofanya wengine iwe kwa nguvu au vyovyote, ila hakufanya hivyo
 
Uhuru Kenyatta? Kabisa?
Nyie watu sijui mna matatizo gani
Hakuna raisi wa ajabu kama Uhuru, Ni mla rushwa na muuaji
Alihonga judges wa the Hague, Ila uhalisia aliua sana na alistahili hukumu.
Acha porojo. Uhuru Kenyatta hakuua mtu japo ni kweli kulikuwa na maovu yaliyofanywa na wafuasi wake.

Kenya, hata ukiwa Rais unashtakiwa wakati wote, na mahakama ipo huru 100%. Kama angekuwa mla rushwa asingekosa kushtakiwa. Kenya hata raia wa kawaida una uhuru wa kumfungulia mashtaka kiongozi.

Msiwe mnaokoteza maneno ya mitaani, wakati mmekosa uelewa. Watanzania acheni porojo. Jadilini hoja.
 
Kwa chuki na porojo, Uhuru anaweza kusemwa vibaya, lakini kwa hoja, ukweli na uhalisia, Kenya kwa sasa ja Uhuru Kenyata, ni mfano wa kuigwa katika uongozi na kidemokrasia Afrika.

Kuna wakati Tanzania tulikuwa tunaenda vizuri, lakini mwaka 2015 balaa liliingia, nchi ikarudi nyuma kabisa. Na leo Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongozwa kidikteta. Taasisi zote za usalama na utoaji haki zimeparanganyika. Kwa kupitia tu mtu mmoja, nchi iliharibika, Taifa likagharimika vibaya.
 
Endelea kujifariji. Mjinga hawi mjinga mpaka pale anapoufurahia ujinga.

Watanzania wengi ni wajinga, na wajinga wengi ni wafia CCM (CCM inapendwa na wajinga - TWAWEZA). Hawa wanaona fahari kuwa wajinga.

Sisi tuendelee na mambo yetu ya kijinga ya kutekana, kubambikiana kesi, kufungia vyombo vya habari na mikutano, wenzetu wanasonga mbele katika nyanja zote. Dunia ya leo ni ya watu waliostaarabika. Ile primitive leadership aliyoianzisha Magufuli, ya kuswaga watu kama ngiri, haina nafasi katika Ulimwengu wa wastaarabu.

Uhuru Kenyata, Mungu azidi kukubariki kwa sababu unajua thamani ya utu na uongozi wa kidemokrasia. Mlikuwa nyume yetu lakin sisi baada ya kutumbukizwa kwenye dimbwi la takataka, tunahangaika, na njia haijaonekana bado.
 
Uhuru is matured, educated, down to earth person. Hana ulimbukeni na uongozi, anaheshimu sana watu. Ni fahari ya Africa
Ni ukweli ambao mwenye akili yeyote ja mkweli wa nafsi yake, hawezi kupinga.
 
Saivi anampiga vita Makamu wake W. Ruto kisa ukabila unasema mtu wa Demokrasia unai-definije DEMOCRASIA?
Usiwe unaandika vitu ambavyo huna uhakika. Uhuru anamwunga mkono Raila. Raila ni kabila la Uhuru?

Kama hamwungi mkono Ruto, ni kwa sababu nyingine, siyo ukabila. Makabila hasimu Kenya ya zamani ni Wakikuyu na Wajaluo. Leo Uhuru (mkikuyu), anamwunga mkono Raila (mjaluo), halafu wajinga wanasema Uhuru ni mkabila. Ujinga mkubwa!
 
Alikuwa tayari ana kesi kule ICC na alikuwa anaogopa asiue watu kama 2007
 
Kenyata ndiye rais bora kwasasa katika bara la Afrika.
Ana madhaifu yake lakini kubwa alilo nalo ni mapenzi kwa nchi yake na watu wake.
Huyu jamaa halali anasaka fursa kila kona.
Anazijua diplomasia za kiuchumi.

Labda mwingine ni rais mpya wa Zambia tumpe muda.
Hangaya...mmmh???????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…