Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Tunataka mama aendelee na kazi ya Magufuli, kwanini aliruhusu mikutano ya siasa kabla uchaguzi, Mwamba alisema No.
Hapo 👆👆unasherehesha nn? Unadai aendelee na nn? Yaan unasapoti uvunjwaji wa sheria, then nakwambia unapinga hujasema. Wee jihadist una matatizo san!!!
 
Tulieni kwanza ili 💉 dawa iwaingie. Ilikuwaje hamkuamua kuwauzia hao ndugu zenu Waarabu bandari zenu za Zanzibar? Na badala yake mkaona muwauzie bandari zetu za Tanganyika?

Na kama mlikula hela zao, mtazitapika kudadek zenu.
Kwanza kumbuka, mimi ni Mtanganyika kuliko wewe. Nimezaliwa Tanganyika, kabla haijawa Tanzania. Naitafuta sana Tanganyika yangu siioni.

Nenda mahakamani ukalalamike, hapa hatujaona bandari iliyouzwa.
 
Weka ushahidi. Wacha porojo.
Kauli zako na michango yako hapa JF ni ushahidi tosha. Comments za wengi humu zimekuwa zikikusihi uache udini. Wewe ni mtu hatari sana kwa mshikamano wetu kama Taifa. Huna kabisa audacity ya kuwasema wengine. ACHA UDINI.
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi.

Haya yanayoendelea si maoni tena bali ni vunjifu wa amani uliokusudiwa. Uhuru wa maoni ni lazima uwe na mipaka.

Mtu anajiita mwanasheria msomi au wakili msomi , mwanasiasa, anasimama kwenye majukwaa ya habari na kurusha matangazo yaliyojaa chuki kuwa nchi inauzwa, au bandari inauzwa, Wazanzibari waniuza nchi. Na cha kushangaza sana waziri wa habari amekaa kimya. Waziri wa sheria amekaa kimya. Waziri wa mambo ya ndani amekaa kimya, waziri wa ulinzi amekaa kimya.

Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria. Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.

Mpaka sisi tuliozowea mitandao ya kijamii tunawashangaa moderators wapo kimya, watu wanaporusha matusi na kejeli mpaka kwa Rais na mawaziri wake. Hivi hatuyaoni? Au tunapenda huu uchokozi uendelee mpaka uzae madhara?

Kuuwasha moto ni kwepesi sana, kazi inakuja katika kuuzima.

Mimi nadhani wale wote wanaodai nchi imeuzwa waende mahakamani au kwa wao kupeleka madai au serikali iwaite mahakamani waje kuonesha nchi imeuzwa wapi na kwa lipi zaidi?

Nahisi kuna watu wapo nyuma ya pazia amabao wanadhani labda yataishia kiwepesi wepesi yakiachiwa yaendelee. Sasa hivi tayari chuki za wazi zinajionesha kati ya Wasio EWaisslam na Waislam, wasio Waarabu na Waarabu, Wabara na Wazanzibari. watu wa pwani na wasio wa pwani.

Hivi hayo yote kweli yamesababishwa na makubaliano ya Dubai na Tanzania yaliyopitishwa bungeni au kuna yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo hatuyaelewi?

Tunaionmba serikali ichukuwe hatua za dhati, kila anaerusha au kuongea chuki akajieleze kwa ushahi wa hayo ayasemayo, kama hana ushahidi aseme ukweli ni na nani yupo nyuma yake anaemlipa au kumchochea kufanya hivyo.

Serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama ili kulinda raia wa nchi hii kujiingiza katika chuki na migogoro isiyo ya lazima. Huu ni mtego wa panya watania waliokuwemo na wasiokuwemo.

Naamini katika uwazi na ukweli na naamini katika uhuru wa maoni na habari, lakini kila uhuru ni lazima uwe na mipaka yake. Naona au Tanzania hatuna mipaka ya kujielezza maoni yetu aukama tunayo ama hatuijuwi au tunaiwachiie makusudi mipaka inavukwa?

Serikali, hususa Waziri wa habari, Nape Nnauye tueleze tupo bado ndani ya mipaka ya sheria au tumekiuka? Kama bado upo ndani ya mipaka ya sheria za uhuru wa maoni, tunaomba shertia zikafanyiwe ukarabati. Ili tuwe nchi yenhe kuheshimu utowaji mapni yetu uwe wa kuheshimiana.

Wewe kama hupendi nilichosema au kufanya mimi nifahamisheni usinitukane.

Moderators wa JF tunaomba majukwa haya siasa na habari mchanganyiko yapewe kipa umbele ili yasiwe ni chimbuko la maafa.
Amelikoroga sasa anaaza kulinywa. Itaanza kunyesha na panapovuja patajulikana tu. Ukisikia yalaa inaweza kuwa imempata! Ni zamu yetu ni zamu yetu sawaaa lakini tuwe makini basiiii, wasije stukia mchezo, na ni kama vile wameshtukaaaa.
 
Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria. Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.
Mleta mada unaamini ktk udikteta na ukandamizaji wa haki ya kutoa maoni, ndiyo maana unapendekeza wanaotoa mawazo usiyopenda kuyasikia wakamatwe.

Kuna namna tofauti ya kutoa dukuduku, wapo wanaonuna, wanaolia, wanaotukana na wanaopiga kelele. Katikati ya kelele na fujo zote hizi kiongozi makini huchambua na huzingatia hoja za wanaotoa dukuduku .

Acha kuhubiri vitisho.
 
Hapo 👆👆unasherehesha nn? Unadai aendelee na nn? Yaan unasapoti uvunjwaji wa sheria, then nakwambia unapinga hujasema. Wee jihadist una matatizo san!!!
Kqsome vizuri, au huelewi unachokisoma?Nilianza kwa kukumbusha kipindi cha magufuli. Kisha nikamtaka mama Samia afanye nini?

Huko kivyako ndiko kusherehekea?
 
Kwanza kumbuka, mimi ni Mtanganyika kuliko wewe. Nimezaliwa Tanganyika, kabla haijawa Tanzania. Naitafuta sana Tanganyika yangu siioni.

Nenda mahakamani ukalalamike, hapa hatujaona bandari iliyouzwa.
Unataka niende mahakama gani kulalamika? Ile ile iliyosemwa na kada wenu maarufu Rostam Aziz, au kuna mahakama nyingine?
 
Mleta mada unaamini ktk udikteta na ukandamizaji wa haki ya kutoa maoni, ndiyo maana unapendekeza wanaotoa mawazo usiyopenda kuyasikia wakamatwe.

Kuna namna tofauti ya kutoa dukuduku, wapo wanaonuna, wanaonalia, wanaotukana na wanaopiga kelele. Katikati ya kelele na fujo zote hizi kiongozi makini huchambua na huzingatia hoja za wanaotoa dukuduku .

Acha kuhubiri vitisho.
Naamini katika haki ya kujieleza isiyovuka mipaka. Ikivuka mipaka inaweza kuvuruga amani. Kwa hiyo vyombo vyetu vya kiusalama vichukuwe hatua.
 
Kugawa bandari zetu kwa wajomba zenu milele hapo tu mmeshavuruga amani za mioyo yetu. Tumechafukwa mbaya kabisa.
 
Kwanza kumbuka, mimi ni Mtanganyika kuliko wewe.
Ahaa, unakiri wewe ni Mtanganyika na katika msingi huo huo unajua kuwa Dr. Samia si Mtanganyika. Sasa Mtanganyika akidai Wazanzibari ndio wamehusika katika agano au makubaliano au mkataba wa bandari za Tanganyika na DP World ya Dubai, je ni kweli au si kweli?
Nimezaliwa Tanganyika, kabla haijawa Tanzania. Naitafuta sana Tanganyika yangu siioni.
Lakini unawaona wabunge wa Tanzania Mainland kama alivyoiita mzaliwa wa Zanzibar Dr. Samia au naye ulimi uliteleza? Kwa tamko lake yeye Dr. Samia je unakiri kuwa tunao viongozi wa Tanzania Mainland (Tanganyika) na tunao viongozi wa Zanzibar, je ni kweli au si kweli?
Nenda mahakamani ukalalamike, hapa hatujaona bandari iliyouzwa.
Je una hakika? Okay, sawa haikuuzwa...sasa kwa maneno machache ni nini kilifanyika na neno lipi hapa lingetoshelesha na kukuridhisha? Bandari kumilikishwa kwa DP? Bandari kukodishwa kwa DP? Bandari kubinafsishwa kwa DP? Au Bandari kugawiwa bure kwa DP!

Mtenda akitendewa huona kaonewa, he huko shule ulienda kufundhishwa ujinga? kwa kweli unanchekesha. Kumbuka hata mbwa chini ya meza ya karamu hunenepa kwa makombo anayotupiwa. Kalaghabaho!
 
Enzi za utawala wa marehemu watu kama hawa ni kula chuma tu mtasikia fulani haonekani tu mtaani.
 
Tulifundishwa na mwalimu Nyerere tuwe wakali linapofika suala la uvamizi wa ardhi ya nchi yetu, Idd Amin aliitwa majina mabaya mfano NDULI mlanyama za watu, Leo hii watu wanamega Kipande Cha ardhi yetu ninyi mnataka waelezwe kwa lugha za kupakwa rangi?
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi.
Nakubaliana na wewe. Elimu itumike kuelimisha na si vinginevyo

Haya yanayoendelea si maoni tena bali ni vunjifu wa amani uliokusudiwa. Uhuru wa maoni ni lazima uwe na mipaka.
Uko sahihi kabisa. Tuheshimu Katiba ya nchi tuendelee kuishi kwa amani.

Katiba ya JMT (1977) Ibara ya 30(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

Mtu anajiita mwanasheria msomi au wakili msomi , mwanasiasa, anasimama kwenye majukwaa ya habari na kurusha matangazo yaliyojaa chuki kuwa nchi inauzwa, au bandari inauzwa, Wazanzibari waniuza nchi. Na cha kushangaza sana waziri wa habari amekaa kimya. Waziri wa sheria amekaa kimya. Waziri wa mambo ya ndani amekaa kimya, waziri wa ulinzi amekaa kimya.
Elimu ni kuelemisha, siasa ni shughuli zinazohusiana na utawala wa nchi au eneo zinazolenga kuboresha hali ya maisha ya watu na maendeleo.

Kwa nini hao Mawaziri wamekaa kimya, hatuwasemei, ila inajenga hisia kuwa kinachodaiwa kina ukweli.

Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria. Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.
Hoja yako hiyo itachochea zaidi kuelekea uvunjifu wa amani. Moto hauzimwi kwa moto

Kuuwasha moto ni kwepesi sana, kazi inakuja katika kuuzima.
Wewe unapendekeza moto uchochewe, du?[/QUOTE]
 
Ahaa, unakiri wewe ni Mtanganyika na katika msingi huo huo unajua kuwa Dr. Samia si Mtanganyika. Sasa Mtanganyika akidai Wazanzibari ndio wamehusika katika agano au makubaliano au mkataba wa bandari za Tanganyika na DP World ya Dubai, je ni kweli au si kweli?

Lakini unawaona wabunge wa Tanzania Mainland kama alivyoiita mzaliwa wa Zanzibar Dr. Samia au naye ulimi uliteleza? Kwa tamko lake yeye Dr. Samia je unakiri kuwa tunao viongozi wa Tanzania Mainland (Tanganyika) na tunao viongozi wa Zanzibar, je ni kweli au si kweli?

Je una hakika? Okay, sawa haikuuzwa...sasa kwa maneno machache ni nini kilifanyika na neno lipi hapa lingetoshelesha na kukuridhisha? Bandari kumilikishwa kwa DP? Bandari kukodishwa kwa DP? Bandari kubinafsishwa kwa DP? Au Bandari kugawiwa bure kwa DP!

Mtenda akitendewa huona kaonewa, he huko shule ulienda kufundhishwa ujinga? kwa kweli unanchekesha. Kumbuka hata mbwa chini ya meza ya karamu hunenepa kwa makombo anayotupiwa. Kalaghabaho!
Amesema amezaliwa before 1964 au kabla ya 26/04/1964, Kuna uwezekano mkubwa elimu yake eidha ni form four au diploma.

Hata advance diploma ilikuwepo wakati huo naamini hakufika.
 
Umri mkubwa then hujitambui
Amezaliwa kabla ya 26/04/1964, elimu aliyokuwa nayo si sawa na uliyokuwa nayo wewe, nakumbuka msemo wake wa " shuleni ulienda kujifunza ujinga" nafikiri ana wivu na wasomi wa sasa ila umri umemtupa mkono.
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi.

Haya yanayoendelea si maoni tena bali ni vunjifu wa amani uliokusudiwa. Uhuru wa maoni ni lazima uwe na mipaka.

Mtu anajiita mwanasheria msomi au wakili msomi , mwanasiasa, anasimama kwenye majukwaa ya habari na kurusha matangazo yaliyojaa chuki kuwa nchi inauzwa, au bandari inauzwa, Wazanzibari waniuza nchi. Na cha kushangaza sana waziri wa habari amekaa kimya. Waziri wa sheria amekaa kimya. Waziri wa mambo ya ndani amekaa kimya, waziri wa ulinzi amekaa kimya.

Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria. Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.

Mpaka sisi tuliozowea mitandao ya kijamii tunawashangaa moderators wapo kimya, watu wanaporusha matusi na kejeli mpaka kwa Rais na mawaziri wake. Hivi hatuyaoni? Au tunapenda huu uchokozi uendelee mpaka uzae madhara?

Kuuwasha moto ni kwepesi sana, kazi inakuja katika kuuzima.

Mimi nadhani wale wote wanaodai nchi imeuzwa waende mahakamani au kwa wao kupeleka madai au serikali iwaite mahakamani waje kuonesha nchi imeuzwa wapi na kwa lipi zaidi?

Nahisi kuna watu wapo nyuma ya pazia amabao wanadhani labda yataishia kiwepesi wepesi yakiachiwa yaendelee. Sasa hivi tayari chuki za wazi zinajionesha kati ya Wasio EWaisslam na Waislam, wasio Waarabu na Waarabu, Wabara na Wazanzibari. watu wa pwani na wasio wa pwani.

Hivi hayo yote kweli yamesababishwa na makubaliano ya Dubai na Tanzania yaliyopitishwa bungeni au kuna yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo hatuyaelewi?

Tunaionmba serikali ichukuwe hatua za dhati, kila anaerusha au kuongea chuki akajieleze kwa ushahi wa hayo ayasemayo, kama hana ushahidi aseme ukweli ni na nani yupo nyuma yake anaemlipa au kumchochea kufanya hivyo.

Serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama ili kulinda raia wa nchi hii kujiingiza katika chuki na migogoro isiyo ya lazima. Huu ni mtego wa panya watania waliokuwemo na wasiokuwemo.

Naamini katika uwazi na ukweli na naamini katika uhuru wa maoni na habari, lakini kila uhuru ni lazima uwe na mipaka yake. Naona au Tanzania hatuna mipaka ya kujielezza maoni yetu aukama tunayo ama hatuijuwi au tunaiwachiie makusudi mipaka inavukwa?

Serikali, hususa Waziri wa habari, Nape Nnauye tueleze tupo bado ndani ya mipaka ya sheria au tumekiuka? Kama bado upo ndani ya mipaka ya sheria za uhuru wa maoni, tunaomba shertia zikafanyiwe ukarabati. Ili tuwe nchi yenhe kuheshimu utowaji mapni yetu uwe wa kuheshimiana.

Wewe kama hupendi nilichosema au kufanya mimi nifahamisheni usinitukane.

Moderators wa JF tunaomba majukwa haya siasa na habari mchanganyiko yapewe kipa umbele ili yasiwe ni chimbuko la maafa.

We nae pimbi kama pimbi wengine tu.

Kwani mtu kutoa maoni yake ni kosa mbona ninyi wazazibar mna mdomo sana.

Enzi za Magu mbona alikuwa anatukanwa lakin mlikuwa hamuongei wala kumtetea.

Emu weka kalio lako chini nyambavu wew
 
Back
Top Bottom