lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,485
Ukweli Ni kwamba Sasa tunapata vionjo tofauti kabisa katika hotuba za Samia.
Kwa kweli sionglei kabisa maudhui ya liyomo kwa hotuba za Samia, kwa leo naongelea tu Uhutubiaji wa Samia, kuwa anahutubia kiungwana Sana, kwa lugha ya kushawishi zaidi yenye maneno yenye staha,Radha nzuri ya Kiswahili, sio kwa sababu anatokea Pwani tu, bali anaongea huku akijua Watanzania Wakubwa na wadogo wanamsikiliza, wazazi na watoto majumbani kwao wanamsikiliza.
Samia anahutubia Taifa, hafokei Taifa.
Samia anahutubia wananchi, hafokei wananchi.
Kabla ya Samia tulikua hatuhutubiwi, tulikua tunafokewa.
Kabla ya Samia wengine tulikua tunaogopa kusikiliza hotuba na Mama zetu, Baba zetu, Dada zetu.
Hapa tulikua tunaogopa Mambo mawili, kufokewa, na baadhi ya "maneno".
Samia anahutubia kwa kushawishi,zamani tulikua tunapewa matamko na kufokewa.
Kutoka kwenye kufokewa hadi kushawishiwa.
Kwa kawaida Wananchi au wapiga kura ndio waajiri, lakini tuligeuzwa hayawani, kupokea tamko lolote limtokalo mtu kinywani.
Mungu katupenda Sana Watanzania.
Mungu Fundi.