Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Fikiria taifa liloweza kuendeshwa kwa miaka zaidi ya mia mbili kama demokrasia bila kuwa na katiba iliyoandikwa na bado raia wake wanaweza kupata haki zao zote, mihimili iko huru na jamii haifarakani kwa sababu ya dhulma au uhuni wa kiutawala wa kisiasa. Wanaingia mawaziri wakuu na kuondoka wakati wowote kwa matakwa ya raia ila serikali iko stable.
Mataifa mengine yanakuwa na katiba iliyoandikwa kuanzia siku ya kwanza yanapoanza kujitawala, haki na wajibu wa kila mtu unainishwa ila haifiki hata miaka 10 watu tayari wameshapoteza kuelewana pamoja, dhulma na uonevu vimetamalaki watu wamepoteza imani kwa watawala na watawala wanafanya hila tu kuendelea kubakia madarakani.