Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Uislamu haujakataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani, siungi mkono wasio waislamu kuzuiwa kula mchana

Tatizo wamenyimwa vichogo! Hivyo akili zao zote zimegeuka na kuwa urojo. Yaani usiku mzimu ni kusindilia tu! Sijui futari, wali maharage, chai, soda, vitafuno mbalimbali! Mpaka saa 11 alfajiri!

Halafu mchana wanajifanya eti wamefunga! Wizi mtupu. Huko ni kubadilisha tu ratiba ya chakula.
Jaribu na wewe tuone
 
kuna tofauti Kati ya usiku na mchana.
Ndo maana usiku tunalala na mchana tunatafuta maisha.
Ni rahisi kulala na njaa kuliko kushinda na njaa kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Alafu kufunga na kushinda njaa tofauti.
Kushinda njaa unaweza ukakuta maji ukanywa.ila kufunga unafunga kula mpaka kunywa maji
Tatizo wamenyimwa vichogo! Hivyo akili zao zote zimegeuka na kuwa urojo. Yaani usiku mzimu ni kusindilia tu! Sijui futari, wali maharage, chai, soda, vitafuno mbalimbali! Mpaka saa 11 alfajiri!

Halafu mchana wanajifanya eti wamefunga! Wizi mtupu. Huko ni kubadilisha tu ratiba ya chakula.
 
tokea jana naona watu wanabwabwaja wasiyoyajua

ungewaacha tu waendelee kujifurahisha
 
Ni kweli mkuu.

Ila nadhani uelewa finyu wa baadhi ya waislamu juu ya imani zingine.
Hakuna hijabu huko Ulaya, huo Uhuru unauzungumzia wapi!?.. Arabuni wakiristo wapo huru tu mpaka Iran huko
 
Utukufu ni kuwapa thamani watu.

Nikisema uraisi ni cheo kitukufu maana yake nakusudia ni cheo chenye thamani.

Nikisema mitume ni watukufu maana yake wana au wenye thamani.

Hivyo mtu akisema watukufu waislamu anakusudia "wenye thamani waislamu".

Na neno utukufu mpaka Mungu ni mtukufu lakini utukufu wa Mungu ni mpana kuliko wetu sisi.

Utukufu kwa binadamu tukiitana tunakusudia ni thamani tu.
Aisee wewe unauelewa uislamu.

Kuna baadhi ya watu wanauhusianisha uislamu na matendo ya ukatili, chuki na kibuir...mfano wafuasi wa Al shabab, Boko Haram, Isis. Kwa haraka waweza jua hii ndio falsafa ya uislamu. Kumbe sio, ni watu na malengo yao binafsi
 
Hakuna hijabu huko ulaya,huo Uhuru unauzungumzia wapi!?..arabuni wakiristo wapo huru tu mpaka Iran huko
Sikuelewi unachojibu wala unachouliza

Jaribu kuwacha papara na andika kitu chenye kuelewa
 
Mkuu kafiri maana yake ni kila asiyekuwa muislamu.

Kwa maana ni jina la jumla kwa kila asiyekuwa muislamu, badala ya uislamu kutamka dini zote ikaona iweke kwa ufupi tu kuwa wasiokuwa waislamu ni makafiri.

Hili jina linaonekana baya kwa sababu ya mindset zetu zimejengeka na tunalisikia likitajwa katika maeneo hatarishi.

Kama vile katika mambo ya kuuana utaskia anatajwa kaafiriii, mtu ataona hee kumbe kafiri hii ni jitu la kuuawa kabisa kumbe sivyo kabisa.

Hivyo kafiri ni jina la utambulisho kwa wasiokuwa waislamu mkuu.

Ni kama ukienda kwenye fani ya afya mgonjwa ataitwa mteja, utajiuliza kwamba mimi naumwa alafu naitwa mteja?


Kumbe Maana yake mteja ni mtu ambaye anakuja pale kutaka huduma.

Hivyo neno mteja ni jina la jumla kama ambavyo neno kafiri ni la jumla
Hilo neno kafiri asili yake ni wapi na lina maana gani ya ndani kwa maana ya hiyo asili yake?
 
Habarini za kutwa nyote.

Naomba niseme kwamba katika dini yetu ya uislamu hakuna pahala mtume kamkataza asiyekuwa muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna pahala qurani imekataza asiye muislamu kula mchana wa ramadhani.

Na wala hakuna sehemu wakati wa mtume imeonesha kwamba walikatazwa wasiokuwa waislamu wasile mchana wa ramadhani.

Katika masharti ya mtu kulazimika kufunga kwanza awe muislamu.

Kwa maana asiyekuwa muislamu hailazimiki kufunga,kama halazimiki kufunga maana yake ana uhalali wa kula mchana wa ramadhani kwa sababu sio muislamu.

Mtu anaweza akasema kwamba wamekatazwa wasile hadharani ?

Hadharani kwanza ni wapi kwa mujibu wa sheria ya dini ?

Watu wanakula kwenye migahawa hakuna anayekunywa chai na chapati anatembea pale kariakoo.

Hivyo kuhusu kula hadharani uislamu pia haujakataza kwa sababu neno hadharani ni pana katika muktadhwa huu.

Uislamu umekataza kwa muislamu ambaye hana udhuru wowote alafu akala mchana wa ramadhani,huyu anapata dhambi.

Lakini kuwakataza watu wasile mchana na kuwashambulia sio katika adabu za kiislamu kwa sababu

Kuna wagonjwa hawatakiwi kufunga.
Kuna wanawake wako kwenye siku
Kuna watoto
Kuna wazee
Kuna wasafiri
Kuna wasiokuwa waislamu

Hawa wote ruhusa kula mchana kwa mujibu wa ssheri ya uislamu wetu.

Sasa kama wanaruhusiwa kula mchana vipi wasiruhusiwe kula hadharani wakati hakuna katazo lolote la kula hadharani katika uislamu.

Allah anasema..

"Hakuna kulazimishana katika dini"

Asiye muislamu kumkataza asile mchana maana yake unamlazimisha akae na njaa jambo ambalo sheria ya dini imekataza.

Tutaheshimu sheria itakayowekwa na serikali lakini tunaomba sheria hizo zisinasibishwe na uislamu.

Ni bora uislamu ulaumiwe kwa sheria ambayo kweli imeiweka kama vile viboko kwa wazinifu n.k

Kuliko uislamu kulaumiwa kwa sheria ambayo haijaiweka kama hizi kukataza kula mchana wa ramadhani

Nakaribisha maswali.

Naomba kuwasilisha.
Waambieni wenzenu wanaotesa watu mitaani kulazimisha ana wote tusile

Actually hata hao wanaozuia wengine wasila hakuna Swaumu hapo ni waste of time tu
 
Hilo neno kafiri asili yake ni wapi na lina maana gani ya ndani kwa maana ya hiyo asili yake?
Kafiri ni neno lenye asili ya kiarabu yaani كافر.

Neno hilo kaafir asili yake katika kiarabu ni mtu aliyepinga au kukataa kitu fulani yaani
أَنْكَرَ (ankara) amepinga.
 
Mnahangaika sanaaaaaaaaa lakini sharia yaja ukila hadharani viboko 12,

[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Back
Top Bottom