Hakuna lolote,hiyo finishing ina vitu gani vya ajabu tusivyovijua ,(icheki hiyo nyumba ambayo magu analalamika kujengwa kwa mil 143)Ni kweli mkuu,
Wengi wanalichukulia jengo Kama Ni kupanga tofali na kufunika na cement.
Ila Kuna vitu vidogo vidogo vinapukuta Ela Sana.
Hasa hasa wakati wa FINISHING.
Sasa mzee alikuwepo kwenye wizara ya ujenzi miaka mingapi? Kuna vitu vingine muwege mnatumia akili. Sasa hiyo nyumba hapo umeona ina hivyo vitu? Au unanena kwa kwa lugha....Gharama iliyotumika ni sahihi kabisa ,sababu kuna vitu vya ndani kama vile mtandao wa simu,internet na CCTV camera hapo sio chinii ya milion 40,Bado kuna viyoyozi na umeme.watu wanaongea tu ,mfano sisi tunaojenga kijengo kidogo tu cha tawi la benki ina kugharimu zaidi ya ml 350 hadi 400 ila watu wasiojua masuala ya ujenzi watajua kwamba pesa imepigwa hapo,mzee wetu tunajua kipindi hiki cha kampeni anataka kukosoa tu ila ukweli anaujua
Deepond waweza kuwa unamiliki mjengo ambao unadhani umetumia gharama kwelikweli,lakini akija mbobezi ukimtajia atakukubalia hawezi pinga,lakini moyoni atajisemea," hapa umepigwa". Mafundi wana siri nyingi hasa kama ulijenga bila kuwa mfatiliaji wa ujenzi husika,hizo nyumba tiles ni za mkuranga tu sio spain,hakuna kitu hapo. Fundi ndio anaelewa.Hapa ndo unapata tasfiri halisi ya mtu
Ndio kwenye wizi humo.Msisahau na contractor lazime aweke faida yake hapo kama 30% ya gharama za nyumba yenyewe, msipige mahesahu ya material na mafundi wenu vinega
Miradi ya serikali ndio hutumia mafundi wa mtaani kumbe [emoji1]Kwa standard ya majengo ya serikali hata wakisema wamejengea 200M wala sishangai.
Kwangu binafsi hata 30M najenga kama hiyo.
*Ramani yakugongea.
*Hakuna jamvi.
*Tofali za kuchoma.
*Concrete beam "Lenta" nondo moja inalala
*Mbao siyo treated (zinapakwa oil chafu) tena mix na mirunda.
*Bati brand za kichina tena 30g
*Mafundi wote wa mitaani tu.
*Nasimamia mwenyewe A to Z.
*Napiga Ceiling boards.
*Tiles mchina (Goodone)
*Milango siyo mbao ngumu.
Kwa standard za serikali hiyo thamani ni sahihi kabisa kama imefuata standard zote
Na hapo ndiyo wengi tunapokwenda arijojo kwa kuthaminisha ndani pekee. Wengi tumekosa jicho la valuation ya ndani. Gharama tajwa ni ndani na nje mpaka samani.Kama kuna finishing touches nzuri huko ndani, na structure ilijengwa kwa viwango stahiki, no way hiyo nyumba ni less than 100m.. mnaosema milioni sijui 60, 70 mnaongelea very low qualoty houses...
Naungana na wewe maana hata tofali zinalazwa kwa nyumba za Serikali sio kusimamisha kama za kwetu.Nyumba ni finishing hivyo siwezi ku judge chochote. Kutumia au kutotumia hiyo hela inawezekana.
Aliyelalamika kua hapo kuna upigaji hayuko serikalini?,hayajui haya?,kumbuka amekaa wizara ya ujenzi zaidi ya miaka 10 so maswala ya ujenzi na thamani zake anazijua sana
Umeongea FACT[emoji123]Milioni arobaini hapana, ila kwa mil 100 au zaidi nakubali. Hapo hujui tiles wameka za viwango gani, bati hiyo ni gauge 28 , ratio ya zege hapo ni kama ya madaraja. Mi nadhani kama imefuata standard zile za serikali kabisa inaweza kufika hata mil 120 au zaidi. Tusiwe emotional Sana kwenye haya mambo, tuwe logical. Hapo huenda kila kona ya nyumba kuna nguzo, hapo tayari gharama inaongezeka, huenda katikati ya msingi na lintel kuna ring beam nyingine.
Iyo million 56.8Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.
Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.
Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
unabishana na yesu?Nyumba ni finishing hivyo siwezi ku judge chochote. Kutumia au kutotumia hiyo hela inawezekana.
RAIS KATUDANGANYA?Huwezi mkuu, nyumba za serikali hazijengwi na vifaa vya ujenzi vya hovyo hovyo.
Tofali grade one tena za kulaza mara nyingi, ratio ya cement ya hali ya juu na bati gauge 26.
Huwa mnakurupuka mnalinganisha na vibanda vyetu vya mtaani.
Pili huwa kuna bei ya elekezi ya ujenzi mfano mdogo...
...majengo ya hospitali cost/sqm huwa ni 850,000
...magodauni cost/aqm ni 500,000
Msiwe mnakurupuka kama rais wetu.
Huwezi kuzunguka nyumba eti ukapata gharama za ujenzi.
Pitia manunuzi na pitia kitabu cha consultants uone mapendekezo yao katika ujenzi pamoja na samani zilizopo ndani
Fundi màikoMimi ukinipa 20 nakujengea.
Angeunda tume ya wataalamu nyumba haikadiriwi kwa machoRAIS KATUDANGANYA?
wezi utawajua tuWell said....