Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ni kweli mkuu,
Wengi wanalichukulia jengo Kama Ni kupanga tofali na kufunika na cement.

Ila Kuna vitu vidogo vidogo vinapukuta Ela Sana.

Hasa hasa wakati wa FINISHING.
Hakuna lolote,hiyo finishing ina vitu gani vya ajabu tusivyovijua ,(icheki hiyo nyumba ambayo magu analalamika kujengwa kwa mil 143)

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Gharama iliyotumika ni sahihi kabisa ,sababu kuna vitu vya ndani kama vile mtandao wa simu,internet na CCTV camera hapo sio chinii ya milion 40,Bado kuna viyoyozi na umeme.watu wanaongea tu ,mfano sisi tunaojenga kijengo kidogo tu cha tawi la benki ina kugharimu zaidi ya ml 350 hadi 400 ila watu wasiojua masuala ya ujenzi watajua kwamba pesa imepigwa hapo,mzee wetu tunajua kipindi hiki cha kampeni anataka kukosoa tu ila ukweli anaujua
Sasa mzee alikuwepo kwenye wizara ya ujenzi miaka mingapi? Kuna vitu vingine muwege mnatumia akili. Sasa hiyo nyumba hapo umeona ina hivyo vitu? Au unanena kwa kwa lugha....

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Hapa ndo unapata tasfiri halisi ya mtu
Deepond waweza kuwa unamiliki mjengo ambao unadhani umetumia gharama kwelikweli,lakini akija mbobezi ukimtajia atakukubalia hawezi pinga,lakini moyoni atajisemea," hapa umepigwa". Mafundi wana siri nyingi hasa kama ulijenga bila kuwa mfatiliaji wa ujenzi husika,hizo nyumba tiles ni za mkuranga tu sio spain,hakuna kitu hapo. Fundi ndio anaelewa.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Kwa standard ya majengo ya serikali hata wakisema wamejengea 200M wala sishangai.

Kwangu binafsi hata 30M najenga kama hiyo.

*Ramani yakugongea.
*Hakuna jamvi.
*Tofali za kuchoma.
*Concrete beam "Lenta" nondo moja inalala
*Mbao siyo treated (zinapakwa oil chafu) tena mix na mirunda.
*Bati brand za kichina tena 30g
*Mafundi wote wa mitaani tu.
*Nasimamia mwenyewe A to Z.
*Napiga Ceiling boards.
*Tiles mchina (Goodone)
*Milango siyo mbao ngumu.
Miradi ya serikali ndio hutumia mafundi wa mtaani kumbe [emoji1]
 
Kama kuna finishing touches nzuri huko ndani, na structure ilijengwa kwa viwango stahiki, no way hiyo nyumba ni less than 100m.. mnaosema milioni sijui 60, 70 mnaongelea very low qualoty houses...
Na hapo ndiyo wengi tunapokwenda arijojo kwa kuthaminisha ndani pekee. Wengi tumekosa jicho la valuation ya ndani. Gharama tajwa ni ndani na nje mpaka samani.
 
Mie nakubaliana na mjenzi wa milioni 100 kwasababu nyumba hiyo inategemea material aliyotumia, mbona sie tunajenga na milioni mbili inakwenda kwa madirisha tu ya alluminium? jamani mnyonge mnyongeni haki yake mpeni hebu tumuogope Mwenyezi Mungu tuwe wakweli na kuacha kuitusi taasisi yetu ambayo inatusaidia jamani.
 
Nyumba ni finishing hivyo siwezi ku judge chochote. Kutumia au kutotumia hiyo hela inawezekana.
Naungana na wewe maana hata tofali zinalazwa kwa nyumba za Serikali sio kusimamisha kama za kwetu.

Bado kuna vile vikao vya hao wapigaju[emoji1787][emoji1787]
 
Aliyelalamika kua hapo kuna upigaji hayuko serikalini?,hayajui haya?,kumbuka amekaa wizara ya ujenzi zaidi ya miaka 10 so maswala ya ujenzi na thamani zake anazijua sana

Ndio maana siku zote watu wa manunuzi uwa wanaonekana wezi kutokana na sheria na namna ya utaratibu.

Hiyo nyumba ukienda kimfumo wa sheria ya manunuzi (watu wa procurement) mara kutangaza tender sijui nini na nini lazima uone kuna upigaji.

Lakini ikijengwa kawaida kama ya nyumbani kwako hata mimi naungana kuwa hiyo hela ni nyingi.
 
Wengi humu mnaongelea lakini hamuelewi masuala ya ujenzi. Iyo nyumba hata mil 200 ni sawa. Cost ya nyumba inategemea na finishing na method utakazoyumia
 
Milioni arobaini hapana, ila kwa mil 100 au zaidi nakubali. Hapo hujui tiles wameka za viwango gani, bati hiyo ni gauge 28 , ratio ya zege hapo ni kama ya madaraja. Mi nadhani kama imefuata standard zile za serikali kabisa inaweza kufika hata mil 120 au zaidi. Tusiwe emotional Sana kwenye haya mambo, tuwe logical. Hapo huenda kila kona ya nyumba kuna nguzo, hapo tayari gharama inaongezeka, huenda katikati ya msingi na lintel kuna ring beam nyingine.
Umeongea FACT[emoji123]
 

Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Iyo million 56.8
 
Huwezi mkuu, nyumba za serikali hazijengwi na vifaa vya ujenzi vya hovyo hovyo.
Tofali grade one tena za kulaza mara nyingi, ratio ya cement ya hali ya juu na bati gauge 26.
Huwa mnakurupuka mnalinganisha na vibanda vyetu vya mtaani.
Pili huwa kuna bei ya elekezi ya ujenzi mfano mdogo...
...majengo ya hospitali cost/sqm huwa ni 850,000
...magodauni cost/aqm ni 500,000
Msiwe mnakurupuka kama rais wetu.

Huwezi kuzunguka nyumba eti ukapata gharama za ujenzi.
Pitia manunuzi na pitia kitabu cha consultants uone mapendekezo yao katika ujenzi pamoja na samani zilizopo ndani
RAIS KATUDANGANYA?
 
Back
Top Bottom