Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

nakusalimu sana Dr.nina kaswali nakuomba sana unijibu
Mbona ujenzi wa hii barabara ya feri kibada via tungi umesimama kabisa au inasubiriwa 2015 kampeni hii barabara ya katini faraja kwa wengi ila ndio mbaya sana

Natambua umuhimu wa barabara hii. Mwaka huu wa fedha hatukupata fedha kutokana na ufinyu wa bajeti na sintofahamu kuhusiana na matokeo ya barabara toka Daraja la Kigamboni. Nimeomba tena kwenye bajeti inayokuja.
 
Mh Mbunge ni vyema Ukuaji huu wa Kigamboni ukaenda sambamba na miundo mbinu..
 
Mh Mbunge,nina viwanja vyangu maeneo ya kisarawe II na mwansonga ila napata hofu ya kuyaendeleza kutokana na sintofahamu ya kigamboni kwa sasa. Je, naweza anza ujenzi kwa sasa?
 
Dr F. Ndugulile nina eneo langu pale toangoma ccm (swapi) ni mkono wa kulia ukitokea kongoe. bila shaka unalijua. ni eneo ambalo halijapimwa. naomba unifahamishe kama serikali ina mipango gani na eneo hilo.
 
Ndugu mbunge!nina Kiwanja changu mwasonga !!!je hivi Eneo hili naruhusiwa kuliendeleza???
 
Jamani huyo ni Iqbal mdogo wake na Bahgdad aliyefungwa kwa rushwa.

Iqbal ni kijana mdogo tu na ndiye aliwahi kupewa eneo la Mnazi Mmoja. Alikuwa rafiki mkubwa mno na meya wa Dar wakati huo, Kitwana Kondo.

Hayo mambo ya kampuni ya Azimio ni mchongo tu, mradi wa mji wa kisasa wa Kigamboni ni wa George Bush mtoto. Na amekuwa akija hapa nchini kimya kimya hadi anamaliza siku sita kufuatilia mradi wake.

Mradi huu unaouzungumzia, wa NSSF na Azimio ni magumashi kama yale ya Manji na NSSF. TUSUBIRI.

Jiulizeni huko Kigamboni huyo mwarabu Iqbal na mwenzake Manji wamenunua maeneo makubwa mno ya ardhi na ndiyo ati wanaingia ubia na miradi ya mashirika ya umma.

Wanachukua ardhi ya umma wanaiuzia serikali, nchi hii!

Kwa taarifa yenu, ukanda wote wa Pwani (karibu kilometa 300) toka Kigamboni hadi Mtwara umeshanunuliwa WOTE na vigogo serikalini ili kuvizia wawekezaji na kuwinda ule mradi mfu wa Mtwara Dev. Corridor.
 
Binafsi ninawashukuru sana NSSF kwa uwekezaji mkubwa katika Jimbo la Kigamboni. Ujenzi wa Daraja, ujenzi wa nyumba 600 za Toangoma, mradi wa Azimio na ule utakaoanza hivi karibuni eneo la Dungu ni mchango mkubwa sana kwa wana-Kigamboni.
Nitakuwa mchoyo wa Fadhila kama sitawapongeza NHC pia kwa uwekezaji wa kasi maeneo ya Kibada na hivi karibuni kwenye eneo la Mwongozo.Ukweli lazima tuuseme na tutoe pongezi panapostahili.

Faustine waambie NHC na NSSF wasifikiria kujenga vibanda kama vikotazi wanavyoita "nyumba za gharama nafuu" huko kigamboni, baada ya mika 20 vitaonekana ni takataka. They have to think BIG toward the FUTURE! Wajenge nyumba kubwa na ndefu kuanzia ghorofa tano na kuendelea mpaka vikwangua anga. Space za mabarabara waache zenye ukubwa kama za njia nane. Biashara ya njia mbili au nne zitaonekana vichochoro baada ya miaka 50 labda kama ziwe feeder roads. Think Big toward the Future.
 
Wakuu je maeneo ya mwembe mdogo inakuwaje haya maeneo yapo powa kununua au hayafai kununua???na maeneo gani ambayo kwa sasa yanafaa kununuliwa???

Naombeni msaada wenu
 
Ni mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 7000. Mradi huu ni ubia kati ya kampuni ya Azimio na NSSF. Bw Iqbal ni mwenye eneo hilo na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Azimio.
Dkt Faustine Ndugulile MB-Mbunge Kigamboni

Bwana Akbaru ndio mmemshindwa kabisa anafuga mapori anatunyima fursa wakulima wadogo kwa sasa kisarawe,kijaka,kimbiji,mbutu ,mwasonga yote kahodhi maeneo!! Si mbunge si tibahijuka si kikwete wote mmewekwa mifukoni na Akbaru! Huyu Akbaru ni nani asiyeguswa? Huyo shombe shombe kawarubuni wazee na kununua ekari moja kwa laki moja hadi laki na nusu hayaendelezi kwa zaidi ya miaka 10 anaweka mapori tu na mbunge pamoja na tibahijuka wanamshangilia!!! Kwa sasa ardhi ya kulima hakuna tumekimbilia tundwi na huko bagamoyo kuna akbaru mwingine wa msoga yani sheeedaa!
 
Si Kweli! Uvumi unaotoka na kutakuwa na taarifa sahihi. Mradi wa Mji Mpya wa Kigamboni ni mradi wa Serikali wa kujenga Mji mbadala pembezoni mwa DSM. Wazo la Mji Mpya wa Kigamboni ni zuri na wananchi wanaliunga mkono. Matatizo yapo kwenye utekelezaji. Matatizo yenyewe ni kama yafuatayo:
1. Sheria zinazosimamia mchakato huu ni nzuri (Sheria ya Ardhi na.4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji na.8 ya 2007). Wanaovunja Sheria ni watendaji wa Wizara ya Ardhi na sio wananchi. Wananchi wanataka Serikali ifuate Sheria.
2. Ushirikishwaji: Watendaji wa Wizara ya Ardhi wanataka haki ya mwananchi kama mmiliki wa ardhi ianze na kuishia katika kulipwa fidia pekee. Wananchi wanataka wawe wadau katika mradi huu na kupewa kipaumbele cha kwanza kwenye ardhi yao.
3. Kumekuwa na usiri na sintofahamu kuhusu haki, Stahili na hatma za wananchi wa Kigamboni: Wananchi wanataka washirikishwe kikamilifu na haki zao ziwekwe wazi na waziafiki.
4. Ucheleweshaji mkubwa wa mradi: Kwa muda wa miaka Sita wananchi wa Kigamboni hawajanipa, hawakarabati, hawawezi kuuza Nyumba wala viwanja vyao na hawakopesheki kwenye mabenki. Hali inayoletea unyonge na kudumaza maendeleo yao binafsi.

Matatizo haya yakitatuliwa, mradi unaweza kupokelewa vizuri zaidi na wananchi.

Mh. MBunge @Dr F. Ndungulile kulikuwa na hoja hii ya Mhe.Waziri mkuu Bungeni ,lakini majuzi tena Waziri Tibaijuka ameibuka na hoja tofauti.Swali langu je unataarifa na mwenendo wa hii shughuli ya Wizara na nini maoni yako kwenye ukinzani wa misimamo hii ya Serikali.


Tanzania: Minister Trumps Fairness in Land Allocation in Dar

19 August 2014
Tanzania: Minister Trumps Fairness in Land Allocation in Dar
Summary NEPOTISM will not be entertained in the land allocation programme as the allotment will be carried out in transparency, the Minister for Lands, Housing and Human Settlements, Prof Anna Tibaijuka, has stated. "Yono Auction Mart won the tender to allocate the lands to Kigamboni and Kurasini following the announcement by the ministry," she said adding; "Residents should not listen to propaganda from people who have been discouraging others from buying shares." Prof Tibaijuka said when completed, the Kigamboni project would tremendously benefit people who reside in the area and that the government was seeking the fund for the project.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Govt suspends plans on Kigamboni satellite city - IPP Media
By Felix Andrew

30th May 2014

Kigamboni Satelite city
Prime Minister Mizengo Pinda told the August House here on Wednesday evening that the process will resume after issued that have to do with involvement of the key stakeholders, including the residents in the area and leaders of Temeke Municipality have been solved.

Pinda was contributing to the budget estimate debate for the Ministry of Lands, Housing and Human Settlement Development which was tabled on Tuesday.

The Premier said there was a need to look again into the whole process of establishing Kigamboni satellite city in order to enable it to be implemented well.

“Let us take this issue and involve a wider section of the people like the councilors and other stakeholders so that they become aware of the entire process,” he said.

CC. Prof Anna Tibaijuka
 
Last edited by a moderator:
Mh. MBunge Dr F. Ndugulile kulikuwa na hoja hii ya Mhe.Waziri mkuu Bungeni ,lakini majuzi tena Waziri Tibaijuka ameibuka na hoja tofauti.

Swali langu je unataarifa na mwenendo wa hii shughuli ya Wizara na nini maoni yako kwenye ukinzani wa misimamo hii ya Serikali.

CC. Prof Anna Tibaijuka

Hoja za Kamati ya Bunge hazijafanyiwa kazi. Kauli ya Waziri Mkuu haijafanyiwa kazi. Maagizo ya Spika hayajafanyiwa kazi

Kuna tatizo la baadhi ya viongozi wanaopenda kutumia vyombo vya habari "kushughulikia na kutatua" matatizo ya wananchi bila kushirikisha wananchi wenyewe.

Inashangaza sana viongozi hawa wanashindwa kuelewa "ushirikishaji wa umma" ni moja ya msingi muhimu kabisa katika dhana ya utawala bora.
 
Hoja za Kamati ya Bunge hazijafanyiwa kazi. Kauli ya Waziri Mkuu haijafanyiwa kazi. Maagizo ya Spika hayajafanyiwa kazi.
Kuna tatizo la baadhi ya viongozi wanaopenda kutumia vyombo vya habari "kushughulikia na kutatua" matatizo ya wananchi bila kushirikisha wananchi wenyewe.
Inashangaza sana viongozi hawa wanashindwa kuelewa "ushirikishaji wa umma" ni moja ya msingi muhimu kabisa katika dhana ya utawala bora.

Mkuu naomba ujibu hii hoja hapa chini maana ina mashiko

Bwana Akbaru ndio mmemshindwa kabisa anafuga mapori anatunyima fursa wakulima wadogo kwa sasa kisarawe,kijaka,kimbiji,mbutu ,mwasonga yote kahodhi maeneo!! Si mbunge si tibahijuka si kikwete wote mmewekwa mifukoni na Akbaru! Huyu Akbaru ni nani asiyeguswa? Huyo shombe shombe kawarubuni wazee na kununua ekari moja kwa laki moja hadi laki na nusu hayaendelezi kwa zaidi ya miaka 10 anaweka mapori tu na mbunge pamoja na tibahijuka wanamshangilia!!! Kwa sasa ardhi ya kulima hakuna tumekimbilia tundwi na huko bagamoyo kuna akbaru mwingine wa msoga yani sheeedaa!
 
Mkuu naomba ujibu hii hoja hapa chini maana ina mashiko

Sheria ipo wazi mtu asipoendeleza eneo kwa mda wa miaka mi3 ananyang'anywa huyu akbaru ana mapori kayafuga zaidi ya miaka 10 bila kuendeleza hata hasipojibu ujumbe kaupata vizuri.
 
Sheria ipo wazi mtu asipoendeleza eneo kwa mda wa miaka mi3 ananyang'anywa huyu akbaru ana mapori kayafuga zaidi ya miaka 10 bila kuendeleza hata hasipojibu ujumbe kaupata vizuri.

Then haina maana kuja mbele ya public kujifanya unajibu hoja za wananchi halafu unaishia kujibu hoja nyepesi ambazo unaona zina kuongezea umaarufu halafu unaacha hoja nzito na zenye msingi zaidi.

Hatupo hapa kusifia mazuri sababu kufanya mazuri ni wajibu wa kiongozi na binadamu yoyote yule kwahiyo haihitaji kusifiwa.Sisi tunataka kuongelea maovu na ukiukwaji wa taratibu kama hili swala lako.

CC Dr F. Ndugulile
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom