Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Mkuu tunaweza kuona hio ramani yake
 
Hapa mnachanganya wadau, mtu ana ela inayoweza kujenga nyumba ya vyumba viwili, inawezekanaje hio hio ela ijenge nyumba ya vyumba vitatu?
Ni kweli kabisa. Mimi binafsi nimegundua kujenga vyumba viwili haina tofauti sana na vyumba vitatu. Yaani ongezeko la chumba kimoja ni dogo kifedha ila ni kubwa sana kwenye thamani na matumizi ya nyumba yako.
 
Hii ni nzuri mkuu lakini uwe na uhakika wa kipato endelevu.
Kwa mfano hata huku bongo kuna watumishi wa serikali wanakopeshwa nyumba na NHC then wanakatwa kwenye mshahara.
Lakini kumbuka maumivu yake ni makali zaidi ya kujenga mwenyewe polepole.
Imagine unapokea mshahara wa laki 7 take home halafu ukakopa nyumba ya milioni 60,sasa piga hesabu ukatwe laki tatu kila mwezi utamaliza hilo deni baada ya miaka mingapi?
Kujenga ni kazi ngumu kweli.. Wenzetu wazungu hawajengi.. Nyumba wananunua kwa mkopo kwa kulipia kidogo kidogo huku unaishi ndani.. So pesa ya kulipa rent ndio inalipa mkopo.
 
Ni kweli mkuu ukijenga nyumba ya vyumba vitatu ni standard kwa familia hadi utapumzika kwa miaka mingi bila kuwaza ujenzi mwingine.
Ila ya vyumba viwili baada ya miaka 5 mbele utaanza kuwalaza sebuleni baadhi ya watoto ambayo itakupa stress tena.
ila ya vyumba vitatu umemaliza maana unakuwa na chumba master chako mwenyewe na mkeo,chumba cha watoto wa kike,chumba cha watoto wa kiume.
Mgeni akija kama ni wa kiume atajimix na watoto wa kiume,na kama ni wa kike atajimix na watoto wa kike akiona kero baada ya wiki ataaga aondoke zake
Ni kweli kabisa. Mimi binafsi nimegundua kujenga vyumba viwili haina tofauti sana na vyumba vitatu. Yaani ongezeko la chumba kimoja ni dogo kifedha ila ni kubwa sana kwenye thamani na matumizi ya nyumba yako.
 
Maneno mengi lakini sababu ni moja tu.. Fedha.
 
Haraka ya nini? Unakimbizwa na nani? Kujenga kwa kukimbia kupanga kunaongeza makazi holela na nyumba zisizokuwa na mpangilio wa kueleweka. Kujenga ni mipango na kwa kipato cha kawaida hakuna namna utajenga nyumba kwa mwaka mmoja.
 
Una mentality za kimaskini sana, usiwarithishe watoto wako hiyo hali, na dunia ingekuwa na watu wengi kama wewe kamwe isingeendelea
 
Wewe ndio umeongea point sana maana umetoa ushauri ambao umeufanyia kazi na ukazaa matunda kuliko hao motivational speakers wanaojifanya wataalamu wa biashara kulinganisha nyumba au kiwanja kinachokaa milele kwa biashara ambayo haitoboi hata miaka 3.
Na uzuri pia umetupa na mifano ya wafanyakazi wenzako waliokimbilia kufungua vibiashara hadi leo hii hakuna cha maana walichonacho.
Hapo mtu asipoelewa hii mifano yote huyo basi ni sikio la kufa.
 
Kazi ipo kwenye finishingi mzee hapo akili lazima itanuke
Ukishapaua chagua vyumba viwili vipige finishing tia madirisha/grill nyumba yote na milango ya mbele na nyuma then hamia kwako baada ya hapo endelea na finishing vyumba vingine taratibu ukiwa kwako. Kuliko kujenga mara tatu tatu kiwanja kinajaa nyumba kibao mpk unakosa hewa
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Eti kupishana hovyo na wapangaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…