Ujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida itapitia maeneo gani?

Ujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida itapitia maeneo gani?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Nimemsikia Waziri Ujenzi, Profesa Mbarawa akisema kunaujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida.

Hii barabara mpya itapitia maeneo gani au wilaya zipi ndani ya hiyo mikoa mitatu aliyoitaja?

Mwenye uelewa tafafhali ninahisi Prof. ametupiga changa la macho.

Au ilani ya CCM inasemaje kuhusu hiyo barabara?
 
Dodoma na Singida zipo katikati ya Tanzania,Tanga ipo pembezoni mwa Nchi huwezi kufika Dodoma na Singida pasipo kupitia Mikoa ya Iringa,Morogoro,Manyara,Tabora na Mbeya.

Waziri atakuwa anadhani bado yupo huko Kwao Zanzibar.
🤝
 
inawezekana according to hii ramani
images.jpg
 
Kwa kifupi ccm wakikuambia huko nje ni usiku toka nje ukajiridhishe.

Hiyo barabara haipo ni bara bara ya kisiasa ya kuomba kura mwaka 2025.

Pia nina shauri ile mikataba 15 iliyosainiwa huko tunakopajua ya kupeleka matunda fuatilieni wandugu, tunapigwa
 
Swali ni moja tu, barabara inapitia wilaya ipi na ipi kutoka tanga hadi singida?
Yaani wewe Ni kiazi, hayo maeneo yaliyotajwa yako wilaya tofauti kuanzia Korogwe, Handeni, Kilindi, Kiteto, Kondoa/Chemba Hadi Singida.

Kama umewahi pita Barabara ya Singida-Babati nje kidogo ya Mji wa Singida utaona Kibao kinaonesha uelekeo wa Dodoma(Kondoa eneo la Kwa Mtoro)

Na kwa taarifa yako hii Ni Barabara kuu ya ku serve Bandari ya Tanga na iko ndani ya Central Corridor na ni miongoni mwa Barabara za kimkakati za Afrika Mashariki.

Hivi nyie Chadomo huwa mnaleta ubishi wa Nini hasa?👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221123-081636.png
    Screenshot_20221123-081636.png
    138.4 KB · Views: 19
  • Screenshot_20221123-081531.png
    Screenshot_20221123-081531.png
    29.3 KB · Views: 20
Kumbe SINGIDA ndo mkoa ulio katikati ya nchi na si Dodoma
 
Nimemsikia waziri ujenzi , Prof Mbarawa akisema kunaujenzi wa barabara inayounganisha mikoa mitatu ya Dodoma, Tanga na Singida .
Hii barabara mpya itapitia maeneo gani au wilaya zipi ndani ya hiyo mikoa mitatu aliyoitaja?

Mwenye uelewa tafafhali ninahisi Prof ametupiga changa la macho.

Au ilani ya ccm inasemaje kuhusu hiyo barabara?
Sio changa la macho mkuu,iko barabara inaingilia maeneo ya Dumila kama sikosei,inakwenda kutokezea Handeni then inakutana na barabara ya Dar-Tanga maeneo ya Mkata,ni shortcut nzuri sana ila kwa sasa ni rough road,badala ya kutokea Dodoma ukaenda Morogoro mpaka chalinze ndio uanze kuitafuta Tanga...
 
Yaani wewe Ni kiazi, hayo maeneo yaliyotajwa yako wilaya tofauti kuanzia Korogwe,Handeni,Kilindi,Kiteto,Kondoa/Chemba Hadi Singida..

Kama umewahi pita Barabara ya Singida-Babati nje kidogo ya Mji wa Singida utaona Kibao kinaonesha uelekeo wa Dodoma(Kondoa eneo la Kwa Mtoro)..

Na kwa taarifa yako hii Ni Barabara kuu ya ku serve Bandari ya Tanga na iko ndani ya Central Corridor na Ni miongoni mwa Barabara za kimkakati za Afrika Mashariki.

Hivi nyie Chadomo huwa mnaleta ubishi wa Nini hasa?👇
Wewe ni MWEHU, swali nimeulizwa , Je kuna uwezekano wa ujenzi wa barabara kutoka Tanga kupita Dodoma kwenda Singida bila kupitia mikoa mingine?

Wewe ulipata Geography zero. Kiteto ipo mkoa wa Manyara na sio Dodoma.

Prof Mbarawa, tukusaidie .

Hiyo barabara inatakiwa ipitie mikoa ya Dodoma na manyara ndipo ifike Singida kwa kutokea Tanga.

vinginevyo huku bara hupajui vizuri na utakuwa kila siku kwenye ziara ya Rais unamdanganya.
 
Back
Top Bottom